KLABU ya Mbeya City imewapa tuzo wachezaji wake pamoja na Kocha Juma Mwambusi kwa kuiwezesha timu hiyo kukamata nafasi ya nne katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.Tuzio hizo zilitolewa mara baada ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu kati yao ya Polisi Moro ambapo Mbeya iliibuka washindi wa bao 1-0.
Kwenye tuzo hizo Kocha mkuu Juma Mwambusi alipata tuzo kama kocha mwenye mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha city na ligi kwa ujumla Paul Nonga, Deus Kaseke, Themi Felix walipata tuzo ya heshima kwa kufanya vizuri misimu miwili Rafael Alfa na Kenny Ally walipata tuzo ya wachezaji chipukizi waliofanikiwa Haningtony Kalyusubula alipata tuzo ya mlinda lango bora na Juma Nyosso, Hassan Mwasapili na Peter Mwalyanzi walipata tuzo ya uchezaji bora

Halikadhalika wachezaji wengine 18 nao walipata zawadi ikumbukwe kuwa zawadi na tuzo hizo walizopata wachezaji wa City zimeambatana na bahasha iliyonona vizuri kutoka uongozi na mashabiki wa Mccfc.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini kikosi chake kinaweza kugeuza matokeo ya mabao 2-1 waliyochapwa na Juventus na kutinga hatua fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
AMENOGEWA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Meneja wa klabu ya Real Sociedad, David Moyes amezipasha klabu za Ligi Kuu zinazomuwinda kuwa hana mpango wa kwenda popote kufuatia tetesi kuwa atarejea nchini Uingereza.
Na Rahim Junior