STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 26, 2015

LIGI MISRI KUCHEZWA BILA MASHABIKI

http://3.bp.blogspot.com/-t4ePdv0h2pE/TypkYVXlrAI/AAAAAAAACNA/-DEbAVzj4Mw/s1600/Ahly+5.jpg
Picha ya baadhi za vurugu za soka nchini Misri
CAIRO, Misri
LIGI Kuu ya Misri ambayo ilisimamishwa, itaendelea tena mwezi ujao lakini bila ya kuruhusiwa mashabiki kuishuhudia michezo hiyo kutokana na kukithiri kwa matukio ya vurugu yaliyoleta maafa ya mashabiki hivi karibuni.
Ligi hiyo ilisimamishwa baada ya kutokea vurugu uwanjani na kuua watu karibu 19 kutokana na vurugu hizo za mashabiki na polisi nje ya uwanja jijini hapa Februari 8 mwaka huu.
Baada ya kikao cha Jumatano, Baraza la Mawaziri la Misri katika taarifa yake lilisema kuwa, ligi inaweza kuendelea "bila ya mashabiki baada ya kumalizika kwa siku 40 za maombolezo ".
Hata hivyo, taarifa hiyo haikusema bayana ni lini hasa ligi hiyo itaanza kuchezwa huku mashabiki wakizuiwa kushuhudia mechi hizo.
Maafa hayo yalitokea kabla ya mchezo kati ya klabu za jijini hapa ya Zamalek na ENPPI wakati polisi na mashabiki walipopambana.
Polisi walilipua mabomu ya machizo na kurusha silaha nyingine kwa mashabiki hao, ambao walikuwa wakilazimisha kuingia uwanjani kushuhudia pambano hilo.
Hiyo iliuwa ni mara ya kwanza kwa idadi maalum ya mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi za ligi tangu Februari 2012, wakati mashabiki 72 wa Al Ahly walipokufa walipokuwa wakipambana na wenzao wa Al Masry kwenye uwanja wa Port Said.

Madonna akipiga mwereka jukwaani akitumbuiza London

madonna
Muunganiko wa picha zilizochapishwa katika Daily Mail zikimuonyesha Madonna akiwa chini baada ya kuanguka wakati wa kutumbuiza
She fell over: Madonna still had a look of composure when she knew she was heading for the bottom of the stepsLONDON, England
NYOTA wa muziki wa Pop duniani, Madonna amejikuta akipiga mwereka akiwa jukwaani wakati wa kutumbuiza katika hafla za utoaji wa tuzo za muziki za BRIT 2015.
Muimbaji huyo alipiga mweleka kutoka jukwaa na kuangukia mgongo baada ya mcheza shoo wake mmoja kuvuta `shela’ (mfano wa kofia ndefu aliyoivaa kutoka kichwani) mwanzoni mwa onesho hilo.
Hata hivyo, mwanamuziki huyo mkongwe alikuwa fiti na alirejea tena stejini na kumalizia kibao chake, `Living For Love’.
Baadae mwanamuziki huyo alitoa taarifa rasmi na kusema kuwa "yuko fiti" na `shela’ lake hilo lilikuwa limebana sana.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwishoni mwa hafla hiyo ambayo Ed Sheeran na Sam Smith wote walishinda tuzo.

Kili Marathon kufunga barabara J'pili Moshi

http://www.blackmarathoners.org/wp-content/uploads/2013/11/Mt-Kilimanjaro-Marathon-Logo-WP.jpgNa Tariq Ticotico, Moshi
BAADHI ya barabara za mji wa Moshi zitafungwa ili kuhakikisha usalama wa wanariadha wataoshiriki mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2015 zitakazofanyika Jumapili hii.
Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo, John Addison, amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imetoa kibali cha kufunga na takribani kilometa kumi za barabara kuu iendayo Dar es Salaam zitafungwa kuanzia saa 12.15 asubuhi hadi saa 2.00 asubuhi.
Barabara ya Sokoine kutokea Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara, (MOCU) hadi KCMC na kona barabara ya Kibosho na kutoka barabara ya Lema hadi Chuo Kikuu cha Ushirika, kupitia barabara ya Kilimanjaro, zitafunguwa kuanzia saa 12.30 asubuhi hadi saa 2.00 asubuhi.
Addison alisema kutakuwa na udhibiti utakaofanywa na askari wa usalama barabarani kwenye barabara ya kutoka YMCA hadi Mnara wa Saa, Barabara ya Boma, mzunguko wa barabara ya Arusha, Barabara ya Uru hadi ile ya Chuo Kikuu cha Ushirika, zitafungwa kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi za 2.15 asubuhi.
“Madereva wote watakaotumia barabara hizi punde zitakapofunguliwa wanaombwa kuendesha magari yao kwa uangalifu na tahadhari kubwa kwa ajili ya usalama wa wale wanariadha ambao bado watakuwa wanaendelea na mbio hizo,” alisema.
Kampuni za kusafirisha na kuongoza watalii watakaokuwa na makujukumu ya kuwasafirisha wateja wao kutokea Mweka, zinashauriwa kuanza safari zao baada ya saa 3.00 asubuhi kwa kupitia barabara za Mweka na Sokoine kwa vile wanariadha watakuwa washapita maeneo hayo.
Waendesha magari na wale wa vyombo vingine vya moto wanashauriwa kuepuka kutumia barabara za Lema, Kilimanjaro na ile ya lango kuu la kuingilia Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara kadiri itakavyowezekana ili kuepuka usumbufu.
Alisema mabasi ya mikoani yanashauriwa kuanza safari zao za kutoka Moshi kuelekea Dar es Salaam baada ya saa 2.00 asubuhi, hata hivyo aliongeza kuwa yale ya kutoka Moshi kuelekea Arusha yanaweza kufanya hivyo kwa kupitia barabara ile ya mzunguko wa barabara ya kwenda Arusha.

Nyambui ataka riadha ianzie shuleni

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/NyambuiMbio(1).jpg 
Na Rahim Junior, Morogoro
MAOFISA michezo na maofisa elimu wa mikoa ya Tanzania wameombwa kushirikiana na wenyeviti wa mchezo wa riadha kufufua mchezo huo kutoka ngazi ya shule za msingi na sekondari.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa tathmini wa mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISSETA) yanayosimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) .
Alisema mchezo huo ambao zamani uliitangaza Tanzania duniani unazidi kupoteza umaarufu kwa sababu hakuna mikakati madhubuti ya kufuatilia wanamichezo wenye vipaji kutoka ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu.
Nyambui alisema kwa mara ya mwisho mwaka jana Tanzania ilishiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Scotland ikiwa ni baada ya miaka 40 tangu mkimbiaji Basil John aliposhika nafasi ya nane kati ya 12 walioingia fainali za mbio za mita 1,500.
Alisema mchezo wa riadha hauna wafadhili kama ilivyo michezo ya soka lakini amejitahidi kuishawishi kampuni ya Isere Sports isaidie kuwauzia wachezaji wa riadha vifaa kwa bei ya chini.
"Tumekubaliana na Kampuni ya Isere Sports iagize na kuwauzia wetu vifaa vya michezo kwa bei ya kawaida ili wamudu kununua viatu na jezi," alisema Nyambui.
Meneja Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally Isere, alisema ni kweli wamefikia makubaliano hayo na yeye kama Mtanzania anayehitaji vipaji vionekane atajitahidi kuhakikisha vifaa vya riadha anaviagiza na kuviuza kwa bei ya chini.
Mikoa inayotamba kutoa wanariadha wengi ni Manyara, Arusha, Mara, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Kanda ya Ziwa na mikoa nyingine.

Mtoto wa Hemed Maneti aibuka na 'Doli Samwela'

MUIMBAJI anayekuja juu nchini wa bendi ya Vijana Jazz, Komweta Maneti 'Chiriku Mtoto', amefyatua wimbo mpya wa miondoko ya Bongofleva uitwao 'Doli Samwela'.
Katika wimbo huo msanii huyo ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa muziki wa dansi nchini, marehemu Hemed Maneti 'Chiriku', ameimba kwa kushirikiana na msanii aitwaye J-Sseni.
Wimbo huo ambao umeanza kusikika hewani umerekodiwa katika studio za C 9 na Komweta amesema kuwa ni kati ya nyimbo saba anazorekodi kwa ajili ya albamu yake binafsi nje ya bendi anayofanyia kazi ya Vijana Jazz.
Mwanadada huyo amewaomba mashabiki wa muziki nchini kuunga mkono ikizingatiwa hiyo ni kazi yake ya kwanza katika ulimwengu wa muziki.
"Naomba mashabiki wanisapoti kupitia wimbo huu na nyingine ambazo ninazitengeneza kabla ya kuitoa hadharani albamu yangu," alisema.
Hemed Maneti alikuwa mmoja wa magwiji wa muziki wa dansi nchini aliyedumu na bendi ya Vijana Jazz na kujijengea jina kubwa kabla ya kukumbwa na mauti miaka 25 iliyopita.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa mtunzi mahiri alifariki Mei 31, 1990 na ni Komweta anayeonekana kufuata nyayo za baba yake huyo katika fani ya muziki.
Usikilize hapa chini

Chelsea bado yamlilia Matic, kuikosa Spurs

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/02/22/25EAB80700000578-0-image-a-28_1424611025691.jpgLICHA ya kiungo klabu ya Chelsea Nemanja Matic amepunguziwa adhabu yake kutoka mechi tatu mpaka mbili lakini bado anatarajiwa kukosa mchezo fainali ya Kombe la Ligi Jumapili hii. 
Chama cha Soka cha Uingereza-FA kiliamua kupunguza adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na utetezi uliotolewa na Chelsea. 
Matic mwenye umri wa miaka 26 alitolewa nje Jumamosi iliyopita wakati Chelsea walipotoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Burnley baada ya kumchezea vibaya Ashley Barnes. 
Katika taarifa yake, klabu hiyo imedai kushtushwa na kusikitishwa kuwa Matic bado atatakiwa kutumikia adhabu. 
Matic sasa atakosa mchezo wa fainali wa Kombe la Ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs ambao utafanyika katika Uwanja wa Wembley na mchezo mwingine dhidi ya West Ham United utakaochezwa Machi 4.

FIFA yazitunishia misuli klabu kisa WC 2022

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2014/04/fifa-logo-design-history-and-evolution-wkuq7omm-2161994.jpg
SHIRIKISHO la Soka la Duniani (FIFA) limechimba mkwara kwa kutangaza kuwa hawatarajii kufidia klabu yeyote kwa kuwakosa wachezaji wao na kuleta mkanganyiko katika ligi kutokana na michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar kuandaliwa majira ya baridi.
Siku moja baada ya kikosi kazi cha FIFA kutoa mapendekezo ya michuano hiyo kufanyika Novemba na Desemba, Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Jerome Valcke amewaambia wana habari kuwa hakuta kuwa na malipo yeyote ya kifedha kwa usumbufu utakaojitokeza katika ligi.
Valcke amesema hawatalipa fidia kwa sababu ligi zote zina miaka saba mpaka kufikia muda wa mashindano kupanga mikakati yao kuhakikisha michuano hiyo haileti mvurugano katika ligi zao.
Tarehe halisi ya kuchezwa michuano hiyo inatarajiwa kupangwa na FIFA katika kikao chake cha kamati ya utendaji mwezi ujao huku kukiwa na uwezekano wa timu kupungua kutoka 32 hadi 28 kutokana na muda watakaokuwa nao.

Arsenal 'Majanga' yafa nyumbani 3-1 kwa Monaco

Monaco are jubilant after Kondogbia fired the Ligue 1 outfit into a lead which they never looked like relinquishing
Monaco wakishangilia moja ya mabao yao waliyoitungua Arsenal
Dimitar Berbatov rolled back the years with a glorious finish after Anthony Martial hit Arsenal on the break with a classic counter-attack
Berbatov akiitungua Arsenal
Mtokea benchi Chamberlain akiifungia Arsenal bao la kufutia machozi
Olivier Giroud akikosa bao la wazi kwa kupaisha mpira wa kichwa
Mwenye bahati ya kuwaua Arsenal, Dimitar Berbatov akishangilia bao lake
KLABU ya Arsenal ya Uingereza imejiweka katika nafasi finyu ya kufuzu Robo Fainali baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 ikiwa nyumbani toka kwa Monaco ya Ufaransa.
Arsenal wakiwa uwanja wa Emirates mjini London, walitawala pambano hilo, lakini Wafaransa waliwapeleka puta na kuandika mabao hayo yaliyowapa nafasi kubwa ya kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Geoffrey Kondogbia aliifungia Monaco bao la kuongoza katika dakika ya 38′, goli lililodumu hadi wakati wa mapumziko kabla ya Dimitar Berbatov kukwamisha bao la pili kimiani katika dakika ya 53.
Wenyeji walijitutumua na kufunga bao la kufutia machozi dakika ya 90 kupitia kwa Alex Oxlade Chamberlain kabla ya Yannick Ferreira-Carrasco kumkatisha tamaa Arsene Wenger kwa bao la dakika za lala salama.
Kwa matokeo hayo, Arsenal wanahitaji ushindi wa mabao 3-0 ugenini ili kuweza kuitoa Monaco.

Atletico Madrid na Torres wao wafa Ujerumani

The Spanish striker continues his protests as he asks the official behind the line why his goal was ruled out
MABINGWA wa Hispania, Atletico Madrid wakiwa uwanja wa ugenini walikumbana na kipigo cha bao 1-0 toka kwa wenyeji wao Bayer Leverkusen katika mechi ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bao pekee la washindi liliwekwa kimiani na Hakan Calhanoglu dakika ya 57.
Dakika ya 75 Fernando Torres 'El Nino' aliipatia Atletico bao la kichwa lakini lilikataliwa na mwamuzi Pavel Kralovec kutoka Jamhuri ya Czech na kumzonga.
Katika pambano hilo wenyeji walionyesha kiwango cha hali ya juu cha soka kwa kumiliki kwa asilimia zaidi ya 60 na ushindi huo umewaweka katika nafasi nzuri ya kupenya kuingia robo fainali kutegemea na matokeo ya pambano la marudiano wiki mbili zijazo.
Pambano hilo litachezwa kwenye uwanja wenye rekodi nzuri kwa wenyeji kutofungika kirahisi wa Vicent Calderon mjini Madrid.