STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 9, 2014

Rais Kikwete awaongoza maelfu kumlilia Mzee Small

Rais Kikwete akishiriki kwenye dua ya kuuombea mwili wa Mzee Small nyumbani kwa marehemu
Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba akiwa na Juma Mbizo
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akiwa na Mkwere Original

Wazee wa Mizengwe walikuwapo
Mbembe akilia huku akitulizwa na Mafumu BIlal 'Bombega'
Wazee walikuwa makini kuhakikisha hali ya usalama

Kitwana Manara akiwa na wadau wenzake wa sanaa kwenye msiba huo
Nyota wa filamu, Shamsa Ford, Deo Shija, Cathy na Sandra nao walikuwapo

Issa Kipemba naye alikuwapo
Mashaka aliyeipa kamera mgondo akiteta jambo na Steve Nyerere na MC, Mkwere Original

Ramsey akiteta jambo na Niva
Mama Abdul na waombolezaji wengine

Mzee JKengua na Mzee Jangala walikuwapo bega kwa bega kwenye msiba huo

Maskini mzee wetu tangulia 'ticha' sisi tu nyuma yako
Shamsa Ford na wenzake








Masheikh wakiendesha kisomo kumuombea Mzee Small katika safari yake ya Ahera

Mtoto wa Marehemu, Muhidini Said

JB akiwa na George Kayanda
JB akihojiwa na wanahabari
Pole sana kijana, Rais Kikwete akiteta na mtoto wa marehemu Mzee Small


Rais akisaini kitabu cha maombolezo
 



Rais Kikwete akiteta na Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba

Mzee Jangala akihojhiwa

Richie naye akihojiwa na Saida Mwilima wa Star TV

Mwili ukiombewa dua baada ya kuswaliwa

Mwili ukiswaliwa swala ya Jeneza kabla ya kupelekwa kuzikwa

Mtoto wa marehemu akisoma wasifu wa marehemu

Wazee wa Ze Comedy Show nao walikuiwapo

Safari ya kwenda kuzikwa inanza

Add caption




RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza kwenye makazi ya milele aliyekuwa mchekeshaji maarufu na mkongwe nchini, Said Ngamba 'Mzee Small'.
Rais Kikwete aliwaongoza waombolezaji hao waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Mzee Small, Tabata Kisiwani jijini Dar es Salaam wakiwamo wasanii mbalimbali nyota na wanamuziki majira ya mchana wakati wa kisomo cha kumrehemu marehemu kabla mwili wake haujaenda kuzikwa jioni.
Rais Kikwete alipokewa kwenye msiba huo na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Nyerere na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani kwenda kumpa pole mjane wa marehemu.
Baada ya robo saa alitoka na kwenda kuungana na waombolezaji wengine kwa kutia saini kitabu cha rambirambi kabla ya kuteta na mtoto wa marehemu Muhidini Said na kumkabidhi bahasha yenye risala yake na kisha kuondoka msibani hapo.
Mbali na Rais Kikwete, Rais wa TAFF na Mwenyekiti wa Bongo Movie, msiba huo ulihudhuriwa na nyota mbalimbali wa fani ya sanaa wakiwamo wacheza filamu kama JB, Richie, Dk Cheni, Shamsa Ford, Deoi Shija, Niva, Nova, Slim Omar, Mzee Chillo, Mzee Jangala, Sandra na wengine.
Miongoni mwa wanamuziki waliokuwepo kwenye msiba huo ni pamoja na Roman Mng'ande 'Romario' wa Msondo Ngoma, Cosmas Chidumule, Mafumu Bilal 'Bombenga' na waigizaji waliowahi kufanya kazi na marehemu enzi za uhai wake pamoja na Rais wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher'.
Baadhi ya wasanii akiwemo Steve Nyerere na Mzee Jangala waliuelezea msiba huo kuwa ni pigo kubwa siyo kwa familia ya marehemu bali wasanii wote kutokana na ukweli Mzee Small alikuwa mmoja wa waasisi wa michezo ya kwenye runinga na mkongwe aliyewasaidia vijana wengi akiwa kama mwalimu.
Pia walisema kifo cha Mzee Small umekuja kuwatonesha donda ambalo bado halijapona la kuondokewa na wasanii mfululizo ndani ya muda wa mwezi mmoja sasa.
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Marehemu Mzee Small alizaliwa mwaka 1955. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mingumbi, Kilwa mkoani Lindi. 

Mbali na ukongwe, Mzee Small kila alipozungumza na watu hakuona sababu ya kuficha kusema yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.?
Mzee Small alianza sanaa hiyo miaka ya sabini akifundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono’ ambaye ni marehemu kwa sasa.
Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small ametumika katika vikundi vya mashirika mbalimbali nchini.
Marehemu kila alipotajiwa Bi. Chau alisema ni mkewe wa ndoa wa kwenye maigizo kauli ambayo wengi hawakuiamini wakijua anakwepa kumtambulisha moja kwa moja.
Kuna wakati mke wake, Fatuma Ngamba aliwahi kusema kwamba, hana wivu na Bi. Chau kwa vile anajua anaigiza na marehemu na ndiyo kazi inayowafanya waishi.
Katika kipindi cha mateso ya ugonjwa wake, wadau mbalimbali walijitokeza kumsaidia kwa hali na mali huku wito mkubwa ukitolewa kwamba, watu zaidi wajitokeze badala ya kusubiri kutoa rambirambi.
Mzee Stori alianza kuigiza mwaka 1980 na kupitia makundi kadha kabla ya kuanzisha lake liitwalo Afro Dance.

Ameacha mjane na watoto sita pamoja na wajukuu saba.
Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu Mzee Small. Amina.

Mzee Small kuzikwa leo Tabata

Mzee Small enzi za uhai wake
Mzee Small (kati) akimpa tuzo Man Walter huku Bi Chau akiwa pembeni yake kulia

Mzee Small akiwa na Bi Chau enzi za uhai wake, wawili hawa walikuwa wakiigiza kama mke na mume
MSANII maarufu wa maigizo, Said Ngamba 'Mzee Small' anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kufariki juzi usiku akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anatibiwa.
Msiba wa msanii huyo nguli uko nyumbani kwake Tabata nyuma ya Ofisi za Mwananchi, jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizotolewa jana mchana na mtoto wa marehemu, Muhiddin Said, zilieleza kuwa maandalizi ya kukamilisha safari ya mwisho ya marehemu yalikuwa yanaendelea vizuri na wanatarajia maziko yatafanyika saa 10 jioni.
"Tunatarajia maziko yatafanyika kesho (leo) saa 10 huku huku Tabata," alisema mtoto huyo.
Mzee Small jina lilitokana na ufupi wake alikuwa ni miongoni mwa waigizaji wa mwanzoni nchini waliofungua njia kwa wengine wengi wanaotamba kwa sasa.
Msanii huyo alipata umaarufu zaidi wakati alipokuwa akiigiza kama mume wa Chausiku Salum ‘Bi Chau’ kuanzia katika maigizo ya redioni hadi kwenye vituo vya televisheni.
Mzee Small alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza na kusababisha kuacha kufanya kazi zake za sanaa kwa muda wa miaka miwiki.

Maisha na sanaa
Kwa historia fupi ya maisha yake, Mzee Small alizaliwa mwaka 1955 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, pia Mzee Small kila alipozungumza alikuwa na kawaida ya kujitamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha katika luninga.
Pamoja na kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa kuonyesha vichekesho kupitia luninga, lakini bado alisimama kufanya maigizo ingawa alianza sanaa hiyo miaka 30 iliyopita na akiwa amefundishwa na Said Seif ‘Unono’ (ambaye kwa sasa ni marehemu).
Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, pia Mzee Small alicheza sanaa katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.

Kuanza kupata umaarufu
Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo unaojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini Shule unaomwelezea mwanamke mmoja wa kijijini aliyeolewa mjini.
Pia aliibuka na kitu kingine kiitwacho “Nani Kama Shule" huku akiwa amewashirikisha Majuto, Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba sasa nchini Tanzania.

Kundi binafsi na usanii wake
Mzee Small alikuwa akimiliki kundi lake la sanaa linalojulikana kama Afro Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kupata usajili rasmi mwaka huo huo wa 1994.
NIPASHE

Didier Drogba kurudi Chelsea?

DIDIER Drogba anajiandaa kurejea Chelsea katika kipindi hiki cha usajili. Mshambumbuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa yuko na klabu ya Galatasaray ya Uturuki lakini kocha Jose Mourinho hajapoteza mapenzi yake ya kutaka kumsajili tena nyota huyo aliyeondoka Stamford Bridge 2012.
Mshambuliaji huyo kwa sasa yupo nchini Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazoianza Alhamisi ambapo timu yake ya Ivory Coast imepanbgwa katika kundi C pamoja na Japan, Colombia na Ugiriki

Golden Bush kupeleka ujuzi wao Makambako

Kikosi cha Golden Bush Veterani
Benchi la ufundi la klabu hiyo likiongozwa na atakayekuwa mkuu wa msafara, Wazir Mahadhi, Madaraka Suleiman na Godfrey Chambua
WAKALI wa soka la maveterani, Golden Bush inatarajiwa kwenda mjini Makamabno kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao, Makambako Veterani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico', inasema kuwa mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Juni 22 kupimana ubavu na wazee wenzao wa huko, huku wakitamba kuwa wanaenda kugawa 'dozi' kama kawaida wanavyofanya jijini Dar na hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Ebu tiririka na taarifa hiyo ya Ticotico kama ilivyo hapo chini;

Tunapenda kutoa taarifa kwamba ile timu tishio upande wa veterans hapa nchini yaani Golden bush veterans ambao ndio mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Bara na visiwani watakuwa Makamboko siku ya tarehe 22 June 2014 kwa mualiko wa Makambako Veterans wakishirikiana na Serengeti Breweries. Mwaliko huu umetokana na historia ndefu ya timu yetu ambayo imejijengea heshima ya kuwa na ushirikiano wa karibu na timu nyingi za veterans wakiwemo Makambako Veterans ambao ndio watakuwa wenyeji wetu siku ya tarehe 22. Aidha tunapenda kutumia nafasi hii kama sehemu mojawapo ya kutengeneza urafiki wa karibu Zaidi na timu za nyanda za juu kusini.

Maandalizi yamekamilika kwa asimia 95 ambapo mkuu wetu wa msafara bwana Waziri Mahadhi Mandieta akishirikiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi bwana Yahaya Issa wanakamilisha baadhi ya mambo madogo madogo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Njombe.

Kesho tutakuwa na mechi ya kirafika na Wizara ya afya ikiwa na sehemu mahususi kabisa ya kupasha misuli kabla ya kuanza safari ndefu kabisa ya kuelekea Makambako. Karibuni sana, game ya kesho itapigwa katika uwanja wa Kinesi ali maarufu kama St James’ park kuanzia saa saa mbili kamili asubuhi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Onesmo Waziri “Man of the match” “Ticotico” “player Maker” Msemaji wa timu na Mchezaji Mwandamizi.