STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 30, 2016

Juanfran wa Atletico Madrid aomba radhi mashabiki

http://www.101greatgoals.com/wp-content/uploads/2016/05/Juanfran-Atletico-Madrid.jpgBAADA ya kukosa penalti katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid, beki wa Atletico Madrid Juanfran Torres amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo.
Beki huyo wa kulia aliyefunga penati ya ushindi katika hatua ya 16 Bora dhidi ya PSV Eindhoven ndiye aliyekuwa mchezaji pekee wa Atletico aliyekosa penalti kwenye Uwanja wa San Siro, Milan Italia wakati wa mikwaju ya penalti na kusaidia kuipa Real Madrid taji la 11 baada ya Cristiano Ronaldo kufunga ya mwisho.
Real Madrid  ilishinda kwa penalti 5-3 baada ya kumaliza dakika 120 timu zote zikifungana bao 1-1, huku Antonie Griezmann akipoteza penalti ambao ingeweza kuisawazishia Atletico katika kipindi cha kwanza.
Juanfran walitia simanzi akiwashinda wachezaji wenzakwa kwa huzuni kubwa iliyowapata baada ya matokeo hayo na beki huyo amewaomba radhi mashabiki wao kwa kile kilichotokea.
Leo Jumatatu Juanfran ameaandika barua maalum kwa mashabiki wa Atletico Madrid ili kuwaomba radhi kwa kilichotokea. Barua hiyo imetupiwa pia katika akaunti ya klabu hiyo ya Instagram.

Waraka huo  unasomeka hivi;


http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/05/Juanfran.jpg
Wakara huo wa Juanfran

 
Hello Atleticos,

Nimeomba klabu kuwafikishia barua juu ya kila kitu ninachojisikia
Kamwe sitasahau moyo wa dhati mlioonesha kwangu wakati nilipokuja kwenu kuomba msamaha. Nikiona machozi yangu yakitiririka mbele ya maelfu ya mashabiki wa Atletico waliofika uwanjani na kunisaidia kuendana na uhalisia wa huzuni kubwa iliyokuwa imejaa kwenye nafsi yangu. Vile vile bila ya kusahau sapoti niliyopata kutoka kwa wachezaji wenzangu, kocha na watu wote wanaounda familia hii ya Atletico.
Pia ningependa kuwashukuru kwa imani kubwa ambayo mara zote mmekuwa mkionesha kwetu na zaidi ya yote ni kutufanya sisi kujiona watu wa tofauti wengine na wenye nafsi ya kipeke kutokana na uwepo wetu hapa Atletico.
Miaka miwili iliyopita, niliwaambia kwamba tungerejea tena fainali na tumefanya hivyo, sasa, nawaambia kwamba, Gabi, nahodha wetu hivi karibuni au baadaye atanyanyua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kusherehekea sote kwa pamoja.
Nawapenda sana na tusonge mbele Wana-Atletico.

Rashford asaini mkataba mpya mrefu Man United

http://ichef.bbci.co.uk/onesport/cps/800/cpsprodpb/ECD9/production/_89833606_marcus_rashford_cameron_borthwick_jackson.jpg
Rashford kushoto na kinda mwenzake Cameron Borthwick-Jackson wakisaini mikataba yao mipya ndani ya Man United
YAMETIMIA. Straika chipukizi wa Manchester United, Marcus Rashford amesainishwa mkataba mpya utakaoenda hadi Juni 2020.
Mkataba huo umeenda sambamba na kuongezwa kwa mshahara wake kwa wiki ambao sasa atalamba Pauni 20, 000, kitu ambacho kinda huyo ameeleza kufurahishwa nacho.
Rashford amejizolea umaarufu mkubwa katika mechi chache za Man United katika Ligi Kuu ya England na michuano ya UEFA Europa League kwa kuifungia mabao na juzi Jumapili aliandikisha rekodi ya kuwa mchezaji kinda kufunga katika kikosi cha Three Lions akicheza mechi yao ya kwanza kabisa.

Zoezi hilo la kusaini mkataba mpya lilienda sambamba pia kwa chipukizi mwingine, Cameron Borthwick-Jackson ambaye naye atajibanza Man United mpaka 2020.

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine, Anne Makinda aula!

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/12/REUTERS1083589_Articolo.jpg?resize=640%2C400RAIS wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine wa tatu.
Rais Magufuli amemteua  Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo  Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi, Uteuzi huu umeanza leo Mei 30, 2016.
Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Uteuzi wa  Anne Semamba Makinda  umeanza Mei 25, 2016.
Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. 
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es Salaam Institute of Technology - DIT).
Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.
Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.Uteuzi huu umeanza leo Mei 30, 2016.

Ngoma? Haendi kokote, uongozi Yanga wasisitiza

Ngoma (kushoto)
TAARIFA hii huenda ikapunguza presha za mashabiki wa Yanga, baada ya uongozi wao kusema kwa herufi kubwa kuwa 'NGOMA HAENDI KOKOTE KULE'.
Uongozi wa Yanga umetoa kauli hiyo kukanusha taarifa zilizoenea mtaani kuwa, straika wao mkali, Donald Ngoma anataka kuihama klabu hiyo.
Kuna taarifa ambazo zimesambaa kupitia baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zikidai nyota huyo kutoka Zimbabwe aliyefunga mabao 17 katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, alikuwa mbioni kutimkia Afrika Kusini na Misri ambao kuna klabu zinamnyemelea wakati mkataba wake ukiwa umesaliwa na mwaka mmoja kabla ya kuisha.
"Klabu ya bado ina mkataba wa mwaka mmoja na Ngoma baada ya kumalizika kwa msimu huu. Bado hatujapokea ofa kutoka klabu yoyote inayomtaka. Hizo ni taarifa ambazo siyo rasmi na wanachama na mashabiki wanatakiwa kuzipuuza," Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alisema mchana huu.“Ngoma anaipenda Yanga na anafurahia maisha ya Tanzania. Ameshaanza kujifunza Kiswahili na kama mwenzake Kamusoko ambaye tayari anazungumza vizuri Kiswahili, na inaashiria ni kwa kiasi gani anafurahia kuwa hapa”, amesisitiza Muro.
Yanga ilimnyakua Ngoma katikati ya mwaka jana kutoka FC Platinum baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho ambapo Yanga iliing'oa timu yake kwa mabao 5-2.

Samatta aweka rekodi Ulaya aibeba Genk

Samatta-ushindi 
We're going to Europe!STRAIKA Mbwana Samatta amweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuiwezesha timu yake kucheza michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europa League) baada ya kuisaidia Genk ya Ubelgiji kufuzu hatua hiyo kwa kuilaza Charleroi.
Genk iliyopoteza mchezo wa kwanza katikati ya wiki iliyopita kwa mabao 2-0 ugenini iliikandika Sporting Charleroi kwa mabao 5-1.
Samatta aliyeanza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ikiwa mechi yake ya 18 tangu alipojiunga na timu hiyo kutoka TP Mazembe ya DR Congo, aliibeba timu yake hiyo katika mechi hiyo ya Uwanja wa nyumbani wa Cristal Arena.
Mkali huyo na nahodha wa Taifa Stars, alifunga bao moja ambalo lilikuwa ni goli la pili kwenye mchezo huo, huku Mgiriki Nikolaos Karelis akifunga hat-trick akianza na Mkwaju wa penalti dakika ya 17, kisha Samatta akazamisha bao la pili dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kupiga bao la tatu dakika ya 45.
Kipindi cha pili Genk waliongeza mabao mengine mawili kupitia Karelis aliyefunga bao la nne dakika ya 56 kisha kukamilisha hat-trick yake dakika ya 71 kwa kufunga bao la tano.
Genk imefuzu kucheza michuano ya Europa ligi kwa matokeo ya jumla 5-3 na itaanzia hatua ya awali ya mtoano kabla ya kuingia makundi iwapo itaing'oa timu itakayocheza nao hatua hiyo ya awali ya mtoano.

Huyu dogo, Rashford acha kabisa Man United

KINDA wa Manchester United, Marcus Rashford aliyeibuka msimu huu na kuwa Staa amezawadiwa mkataba mpya ulioboreshwa.
Straika huyo, 18 alisaliwa na mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa sasa, lakini sasa atapewa mkataba mpya wa muda mrefu na kuzoa Pauni 20,000 kwa wiki.
Wikiendi Rashford, akiichezea England kwa mara ya kwanza kabisa, alifunga bao katika sekunde 138 tu tangu mpira wakati England inaichapa Australia 2-1 na kuweka rekodi kuwa kijana mdogo kabisa kuifungia England katika mechi yake ya kwanza.
Rashford aliibuka Msimu huu kuchezea Man United alipochezeshwa kwa mara ya kwanza Timu ya kwanza dhidi ya FC Midtjylland kwenye Europa Ligi na kupiga Bao 2 na kisha tena kupiga Bao 2 walipocheza na Arsenal kwenye Ligi Kuu England.

Tangu wakati huo, katika Mechi 18 za Man United, Rashford amepiga Bao 8.
Mbali ya Rashford, Kijana mwingine wa Man United ambae nae amebakisha Mwaka mmoja na atapewa Mktaba mpya bora na mrefu ni Cameron Borthwick-Jackson.

JT amuunga mkono Mourinho Man United

NAHODHA wa Chelsea John Terry amemuunga mkono Jose Mourinho kufanikiwa kwenye Klabu yake mpya Manchester United huku akimueleza kuwa Meneja huyo ndie bora kupita yeyote aliewahi kucheza chini yake.
Terry alikaribia kuondoka Chelsea mwishoni mwa Msuimu huu baada ya Mkataba wake kumalizika lakini sasa ameongezewa Mwaka Mmoja na Msimu ujao atakuwa chini ya Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte ambae ni Meneja wa sasa wa Timu ya Taifa ya Italy.

Terry, ambae aliteuliwa na Mourinho kuwa Kepteni wa Chelsea wakati Mourinho alipotua Chelsea kwa mara ya kwanza Mwaka 2004, ameeleza: “Ni habari njema kwa Manchester United. Hii itawafurahisha Mashabiki na Wachezaji wa Man United kwani mara nyingi nimesema Mourinho ndie Meneja Bora niliyewahi kufanya nae kazi!”

Straika wa JKT Ruvu amfunika Ngoma VPL

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AMd2imIABKJxV0HhggwR2EZOfOM&midoffset=2_0_0_1_8003251&partid=2&f=1214&fid=Inbox&ymreqid=64fe4ec4-e6bf-e94e-012e-44001c010000&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Mussa akiwa amebebwa na wachezaji wenzake baada ya kuidungua Simba katika mechi ya kufungia msimu ambapo Simba ilalala mabao 2-1
STRAIKA mkali wa mabao wa JKT Ruvu, Abdulrahman Mussa amembwaga mkali wa Yanga, Donald Ngoma baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Mei.
Mussa amewazidi ujanja Ngoma na Ally Nassor 'Ufudu' wa Mgambo JKT aliokuwa akichuana nao katika kinyang'anyiro hicho.
Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu na uliofungia msimu wa 2015-2016, Mussa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne, mawili katika kila mechi kati ya michezo hiyo mitatu.
Kwa kufanikiwa kunyakua tuzo hiyo ya Mei straika huyo atazawadiwa kitita cha Sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 ni; Hamisi Kiiza-Simba (Septemba), Elias Maguli-Stand United (Oktoba), Thabani Kamusoko- Yanga (Desemba), Shomari Kapombe-Azam (Januari), Mohammed Mkopi- Prisons (Februari), Shiza Kichuya-Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

Mkwasa aishtukia Misri, Stars ikiibana Harambee kwao


NA ALFRED LUCAS, NAIROBI
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania Mei 29, 2016, uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Mkwasa maarufu kama Master anasema kwa msimamo na hali ilivyo kwa sasa, “Najua Misri wanatufuatilia. Na hata Kenya kwa siku zote tatu walikuwako. Najua  Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizi, lakini hawataipata Tanzania.”


Mkwasa anasema mchezo dhidi ya Misri, ana uhakika vijana wake watajitahidi ili kupata matokeo mazuri baada ya Jumapili kufanya vema dhidi ya Harambee Stars waliocheza mechi hiyo mbele ya mashabiki wao wachache ambao pia hawakuchangamka kama wale wa Tanzania ambao licha ya kuwa ugenini walichangamsha mji na uwanja.

Wakati Misri wana pointi saba, Taifa Stars ina pointi moja na hivyo wa kuibania au kupindua matokeo ya Misri isiende AFCON mwakani, basi ni Tanzania hasa kama itawafunga Mapharao Jumamosi kabla ya kwenda Nigeria Septemba, mwaka huu kucheza na Nigeria.

“Kama nilivyosema, Misri wanakujawanahitaji pointi moja. Lakini sisi tunahitaji pointi tatu. Mchezo wa leo unatosha kuona mapungufu (upungufu). Maana ilikuwa mechi ngumu iliuyojaa nyota wote wa Kenya ambao ni professionals, lakini mimi nilikuwa na local based players na matokeo yamekuwa hayo.

“Tilianza kufunga bao, lakini wakarudisha. Bora mchezo umeishia hivi maana najua Wakenya hawana uvumilivu, tungewafunga hapa sijui kama tungetoka salama,” amesema Mkwasa ambaye baadhi ya waandishi, hususani wale wa Kenya walianguka kicheko kuashiria kuwa kuna matatizo katika utawala wa soka.

Mkwasa anasema ana taarifa namna ambavyo Misri wanaifuatilia Taifa Star hususani ukusanyaji wa video kwa ajili ya kuona aina ya soka la Tanzania, huku akisema: “Hawatafanikiwa kwa sababu soccer is the game of different approach (Soka ni mchezo wenye mifumo tofauti). Hivyo tulivyocheza na Kenya sivyo nitakavyocheza na Misri, nitakuwa na approach yake.”

Anasema ushindi wa Jumamosi ijayo ni wa kuvuna pointi tatu ili kupata kasi ya kushinda mchezo dhidi ya Nigeria na kufungua ukurasa mpya wa Taifa Stars kutengeneza mazingira mazuri ya kuwashinda Nigeria katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi utakaofanyika Septemba, mwaka huu.

“Tunaomba Wakenya mtuombee. Nasi tunawaombea ili kama wote inatokea mwaka huu tunakosa mafasi, basi iwe kheri kwa kipindi kijacho. Sisi tumekuja kucheza kwenu katika mji wenu wenye baridi basi nanyi karibuni siku moja dar es Salaam, Tanzania katika mji wetu wetu wenye joto, huenda mkaambulia sare vile vile,” anasema.

Mkwasa alipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (FKF), kwa kuandaa mchezo huo angalau kwa asilimia 70 kwa kushirikiana na Tanzania iliyojazia gharama za juu sambamba vijana wake kwa kucheza kwa kujituma licha ya kuwakosa nyota wake wa kulipwa na hivyo kupata picha na mbinu sahihi za kuivaa Misri Jumamosi ijayo.

“Bado tunaendele kujenga timu yetu, wengi ni vijana kama mlivyoona na wengine ni mara ya kwanza wanacheza. Nimewapa nafasi na mmeona uwezo wao, bila shaka tutafanya vema maana wengine ni under 21 wako kwenye kikosi. Huko mbele tutakuwa na timu nzuri,” anasema Mkwasa akimtolea mfano Shiza Ramadhani ambaye alipewa nafasi kwa mara ya kanza katika kikosi cha kwanza akichukua winga ya kulia.


VICTOR WANYAMA
“Kwa hiyo tayari tumeona kitu gani cha kuongeza,” anasema Mkwasa hoja yake iliyoungwa mkono na Nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama ambaye kwa dakika chache, alizungumza na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania na kuhoji: “Unasema leo hamkuwa na professional pale uwanjani?” alipohakikishiwa ukweli huo, akasema:

“Basi mna kikosi kizuri. Wengi ni vijana, wanaweza kama mkicheza kwa kutubana kama mlivyobana hapa, Misri mnaifunga na hata hao Nigeria, si ajabu nikasikia mnakwenda AFCON mwakani. Ninaitakia kila la khetri timu hii, nawatakiwa kila la kheri Watanzania katika harakati zao. Sisi mwaka huu tumepotea kabisa, hatuna matumaini tena, tunajipanga ndiyo maana nimekuja kutetea taifa langu, hata kama tumekosa nafasi,” alisema Wanyama anayekipiga Southampton ya England.

Katika mchezo huo, Taifa Stars iliwakosa nyota wake Mbwana Samatta anayechezea Genk ya Ubelgiji kwa kuwa alikuwa na mchezo muhimu wa kupa nafasi timu yake ama icheze Ligi ya Uropa au ibaki nje katika michezo ya kimataifa ngazi ya klabu Ulaya. Shirikisho la Soka Tanzania na Kocha Mkwasa walimruhusu kama ilivyo kwa Thomas Ulimwengu anayekipiga TP Mazembe waliokuwa na mchezo mkali dhidi ya AS Vita ambao wana utani na ushindani mkali wa soka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


MWINYI KAZI MOTO
Naye Nahodha wa Taifa Stars katika mchezo huo, Mwinyi Kazimoto amesema kwamba mchezo dhidi ya Kenya, umeonesha picha ya kinachotakiwa kufanyika katika michezo ijayo inayoikabili timu hiyo baada ya kusifu maandalizi, mapokezi mazuri na sapoti nzuri kutoka kwa mashabiki wa Kitanzania, hasa wale waliosafiri umbali mrefu kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuishangilia Stars. Nahodha wa Taifa Stars ni Mbwana Samatta anayesaidiwa na John Bocco ambao katika mchezo huo, hawakucheza. Bocco ni Majeruhi.

 MCHEZO WA HARAMBEE STARS, TAIFA STARS
Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza mashabiki walishuhudia mabao 1-1 kwa kila upande na ndiyo yaliyokuwa matokeo ya mwisho katika dakika 90, lakini kipindi cha pili wadau wa soka walishuhudia mabadiliko ya kila timu kujaribu nyota wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA), linaloruhusu kubadili wachezaji hadi wachezaji sita. Lakini hakukuwa na mabadiliko ya matokeo.

Kuhusu mabao ni Elias Maguli ndiye aliyetangulia kuifungia Taifa Stars bao katika dakika ya 30 kwa kichwa baada ya kupokea krosi murua kutoka kwa Juma Abdul kutoka Mashariki ya Uwanja wa Moi Kasarani kabla ya dakika saba baadaye kumfanyia madhambi Winga Ayub Masika ndani ya eneo la hatari hivyo Mwamuzi, Brian Nsubuga kutoka Uganda, kuamuru penalti iliyokwamishwa wavuni na Victor Wanyama.

Katika mchezo huo ambao wakati wote ulikuwa ni wa kushambuliana kwa timu zote mbili, Taifa Stars iliwapumzisha kipa Deogratius Munishi na nafasi yake ikachukuliwa na Aishi Manula na kwa wakati mmoja kuwatoa Jonas Mkude na Shiza Ramadhani na nafasi zao kuchukuliwa na Farid Mussa na Mohammed Ibrahim baadaye Kocha Mkwasa alimwingiza Jeremiah Juma kuchukua nafasi ya Maguli.


Kenya wao waliwatoa Humphrey Ochieng kwa kuingia Cliford Miheso; akatolewa tena Jesse Were kwa Wyclif Ochomo; Ayub Masika akapumzishwa na John Makwata akapewa nafasi kama alivyopumzishwa Anthony Agay na nafasi yake kuchukuliwa na Mayeko Mohammed. Pamoja na mabadiliko hayo, matokeo yalibaki vilevile 1-1 hadi dakika ya 90 katika mchezo ambao Wanyama alipewa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Kazimoto.

VIKOSI VYA TIMU ZOTE
Vikosi vya kwanza katika mchezo, Kenya: 1. Boniface Oluoch, 9. Joakins Otieno Atudo, 5. Abud Omar Khamis, 12. Eugene Ambuchi Asike, 8. David Owino Odhiambo, 14. Anthony Akumu Agay, 15. Victor Mugubi Wanyama, 23. Ayub Timbe Masika, 19. Humphrey Mieno Ochieng’ 16. Eric Johanna Omondi, 29. Jesse Jackson Were
Wachezaji wa akiba: 3. David Okello Abongo, 10. Eric Ouma Otieno, 6. Mayeko Musa Mohammed, 24. Victor Ali Abondo, 27, Wycliff Okello Ochomo, 20. John Mark Makwata, 21. Clifford Miheso Ayisi

Tanzania XI: 1. Deo Munishi, 6. Juma Abdul Jafari, 2. Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, 13. Aggrey Morris, 15. Erasto Edward Nyoni, 17. Jonas Gellard Mkude, 7. Himid Mao Mkami, 16. Shiza Ramadhan Yahya, 12. Mwinyi Kazimoto Mwitula, 10. Elias Mrugao Maguli, 4. Deus David Kaseke

Wachezaji wa akiba walikuwa: 18. Aishi Salum Manula, 5. David John Mwantika, 9. Farid Mussa Shah, 11. Jeremiah Juma Ally, 8. Abrahim Hajibu Migomba, 3. Mwinyi Haji Mngwali, 14. Mohammed Ally Ibrahim

 WAAMUZI


Brian Nsubuga (Mwamuzi wa kati), Hussein Bugembe (Msaidizi wa Kwanza), Ronald Katenya (Msaidizi wa Pili), Amir Abdi Hassan (Kamishna wa mchezo) and  Davies Omweno (Mwamuzi wa Akiba, Mezani.)