STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 30, 2016

Straika wa JKT Ruvu amfunika Ngoma VPL

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AMd2imIABKJxV0HhggwR2EZOfOM&midoffset=2_0_0_1_8003251&partid=2&f=1214&fid=Inbox&ymreqid=64fe4ec4-e6bf-e94e-012e-44001c010000&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Mussa akiwa amebebwa na wachezaji wenzake baada ya kuidungua Simba katika mechi ya kufungia msimu ambapo Simba ilalala mabao 2-1
STRAIKA mkali wa mabao wa JKT Ruvu, Abdulrahman Mussa amembwaga mkali wa Yanga, Donald Ngoma baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Mei.
Mussa amewazidi ujanja Ngoma na Ally Nassor 'Ufudu' wa Mgambo JKT aliokuwa akichuana nao katika kinyang'anyiro hicho.
Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu na uliofungia msimu wa 2015-2016, Mussa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne, mawili katika kila mechi kati ya michezo hiyo mitatu.
Kwa kufanikiwa kunyakua tuzo hiyo ya Mei straika huyo atazawadiwa kitita cha Sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 ni; Hamisi Kiiza-Simba (Septemba), Elias Maguli-Stand United (Oktoba), Thabani Kamusoko- Yanga (Desemba), Shomari Kapombe-Azam (Januari), Mohammed Mkopi- Prisons (Februari), Shiza Kichuya-Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

No comments:

Post a Comment