STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 14, 2014

Manchester United yaanza Ligi yaifumua QPR

Di Maria akishangilia bao lake
1410710470161_lc_galleryImage_14th_September_2014_Barcl
Furaha ya ushindi Manchester wakifurahia baada ya kuypata moja ya mabao yao
Mata akishangilia bao lake
NYOTA wapya wa Manchester United, Ander Herrera na Angel di Maria walithibitisha thamani yao baada ya kuiwezesha timu yao kupata ushindi wa kwanza msimu huu katika mashindano kwa kuilaza QPR kwa mabao 4-0 katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.
Di Maria aliwainua mashabiki wa Old Trafford kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 24 kabla ya Herrera kupachika la pili katika dakika ya 36 akimalizia kazi ya nahodha Wayne Rooney.
Dakika moja kabla ya mapumziko, nahodha huyo Rooney alifunga bao la tatu akimalizia kazi murua ya Herrera na bao la mwisho la vijana wa Luis Van Gaal lilifungwa na Juan Mata katika dakika ya 58 kwa kazi safi ya Di Maria aliyeonyesha ubora wake na kuifanya Mashetani Wekundu kupumua baada ya kuanza vibaya ligi na msimu mzima kwa ujumla.
Radamel Falcao aliingia uwanjani katika kipindi cha pili na kuonyesha makeke yake ikiwa ni mara ya kwanza tangu asajiliwe kutoka Monaco.

Yanga ya Maximo kiwangoo! yaiua Azam x3

Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka Erasto Nyoni wa azam (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto )
Kikosi cha Azam kilichozimwa Taifa leo
Kikosi ch Yanga kilichotwaa Ngao ya Hisani leo kwa kuilzaza Azam
 KLABU ya Yanga iliyo chini ya kocha Marcio Maximo wa Brazil, jioni ya leo imetuma salamu kwa klabu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifumua bila huruma watetezi wa ligi hiyo, Azam mabao 3-0 katika pambano la Ngao ya Hisani lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Yanga ikiwa katika kiwango cha juu na kuwafunika wapinzani wao, walithibitisha kuwa bado ni wababe wa Azam katika mechi ya Ngao ya Hisani baada ya kuifdunga kwa msimu wa pili mfululizo kwani msimu uliopita waliitambia kwa bao 1-0.
Mabao yaliyoizamisha Azam waliotwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita bila ya kupoteza mchezo wowote yalitumbikizwa wavuni na Gelinson Santana 'Jaja' aliyefunga mabao mawili na kuzima ngebe za mashabiki waliokuwa wakimzomea kabla ya Simon Msuva kufunga jingine akitokea benchi kumpokea Nizar Khalfan.
Kipigo hicho cha Azam kimevunja rekodi ya kocha Joseph Omog pamoja na vijana wao ambao walikuwa wakifurahia kushinda au kutoka sare bila kupoteza mchezo wowote tangu mwaka jana katika mashindano nchini Tanzania.

Hofu yatanda Arsenal kuumia kwa Debuchy

Gunners manager Arsene Wenger has admitted that Mathie Debuchy's injury 'doesn't look good'
Arsenal defender Mathieu Debuchy screams in pain after injuring his ankle against Manchester CityKLABU ya Arsenal ipo katika hofu kubwa baada ya beki wake wa kulia Mathieu Debuchy ameumia vibaya na haijajulikana bado  atakaa nje ya kiwanja  kwa muda gani  .
Kocha  Arsene Wenger amesema majeraha ya  Debuchy’s  ‘Hayaonyeshi' kupona upesi na kuna hitajika kufanyika uchunguzi wa kina zaidi waweze kugundua atakaa nje kwa muda gani .
Mchezaji huyo alianguka vibaya na kukanyaga kifundo chake cha mguu wa kushoto katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Arsenal na Manchester City ulioisha kwa sare ya 2-2.
Debuchy, 29 alijiunga na  Arsenal katika majira ya kiangazi akichukua nafasi ya Bacary Sagna,aliyejiunga na  Man City, na alicheza vizuri katika mechi na klabu yake ya zamani katika uwanja Emirates.

Yanga, Azam leo hapatoshi Taifa katika Ngao ya Jamii

http://3.bp.blogspot.com/-UfUbU9JN1As/Ug8YB5uA5gI/AAAAAAAAA94/1ujFLP8vOXQ/s1600/YANGAVSAZAM.jpgMWISHO wa tambo na mikwara baina ya Azam na Yanga ni leo wakati klabu hizo mbili zitakapopepetana kwenye mechi ya Nf\gao ya Jamii kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Timu hizo zitapambana kwenye uwanja wa Taifa, huku zote zikiwakosa baadhi ya nyota wake kutokana na kuwa majeruhi.
Yanga inatarajiwa kumkosa kiungo wake mahiri, Andrey Coutinho aliyeumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dar es Salaam kwenye uwanja wa sekondari ya Loyola.
Mshambuliaji huyo alipatwa na maumivu hayo wakati alipokuwa akijaribu kupiga mpira na hivyo kushindwa kuendelea na mchezo. Timu hizo zilitoka suluhu.
Azam ambao walilala bao 1-0 katika mechi kama hiyo kwa msimu uliopita, haitakuwa na huduma ya nahodha wake, John Bocco Adebayor aliye majeruhi pia, kwa mujibu wa Meneja wa Azam Said Jemedari.
“Tunao majeruhi wawili, ambao hawatakuwepo kwenye programu ya mchezo wa Ngao ya Jamii, ambao ni beki Waziri Salum na nahodha wetu, John Bocco,”alisema Jemedari.
Timu hizo zinakutana baada ya mwaka jana kushuhudia Azam wakiipindua Yanga na kuwanyang'anya ubingwa wakiwa hawajapoteza mchezo wowote.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.
Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.

Simba yabanwa na Ndanda Fc Mtwara

Simba SC
Ndanda Fc
SIMBA imeendelea kwenda mwendo wa kusuasua katika mechi zake za kujiandaa kwa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya jana kulazimishwa kutoka suluhu na Ndanda FC.
Katika mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, vijana wa Ndanda waliwabana vyema wapinzani wao katika vipindi vyote viwili.
Sare hiyo imekuja siku chache baada ya Simba kuchapwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kama ilivyokuwa katika mechi dhidi ya URA, mshambuliaji Emmanuel Okwi alishindwa kuonyesha makeke yake kutokana na kubanwa vyema na mabeki wa Ndanda. Okwi aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Abdalla Seseme.

Warembo Miss Tanzania 2014 wawasili kambini

Na Father Kidevu 
Wanyange 30 wanao wanbia taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.


Warembo hao waliowasdili kwa muda tofauti kuanzaia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar. 
Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Kanda ya Ziwa ambayo alizawadiwa hivi kjaribuni katika shindano lao.
 Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliendesha kutoka jijini Mwanza.
 Warembo wa Kanda ya Ziwa wakijiandikisha baada ya kuwasili kambini.
 Warembo wakielekea chumba cha mkutano.
 Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.

Shinji Kagawa aanza na mguu mzuri Borussia Dortmund

Japan international Shinji Kagawa (right) celebrates after his goal at the WestfallonstadionKIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Shinji Kagawa amedhihirisha ukali wake baada ya kurejea Borussia Dortmund kwa kishindo kwa kuisaidia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Freiburg katika Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.
Kagawa aliyekaribishwa vyema na mashabiki wa klabu hiyo kwa mabango na bendera ya Japan, alifunga bao moja na kuchangia nyingine lililokuwa la kwanza kwa timu yake lililotumbukizwa wavuni na Adrian Ramos.
Ramos alilipa fadhila kwa kumtengeneza Mjapani huyo aliyepachika bao la pili katika ya 41 na kuifanya wenyeji kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Bao la tatu la Dortmund iliyoimuuza Kagawa kwa Mashetani WEkundu kabla ya kumrudisha hivi karibuni liliwekwa kimiani katika kipindi cha pili na Aubameyang  dakika ya 78 kabla ya wageni kupata bao la kufutia machozi dakika ya 90 kupitia Sorg.

Real Madrid yafa nyumbani, Neymar aibeba Barcelona La Liga


Atletico Madrid's Arda Turan scores
Kitu hicho! Atletico Madrid wakiwaadhibu wenyeji wao
Cristiano Ronaldo
Hawaamini kama ni kweli wamepigwa
Cristiano Ronaldo scored a penalty in Real Madrid's 2-1 defeat against Atletico Madrid on Saturday
Ronaldo akifunga mkwaju wake wa penalti
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Hispania, Atletico  Madrid wameendeleza ubabe wake kwa Real Madrid baada ya kuinyuka  mabao 2-1 Uwanja wa Bernabeu mjini Madrid, katika mchezo wa ligi hiyo.
Atletico waliwashtukiza wenyeji wao kwa kuandika bao la kuongoza dakika ya 10 tu ya mchezo huo kupitia kwa Tiago.
Wenyeji walicharuka na kusawazisha dakika sita baadaye kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa penalti na kufanya hadi mapumziko mambo yawe 1-1.
Atletico walirejea tena nyavuni mwa wenyeji wao kwa kuandika bao la pili na la ushindi katika dakika ya 76 kupitia kwa Arda Turan aliyemaliza kazi nzuri ya Raul Garcia. 

Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Barcelona walipta ushindi nyumbani dhidi ya Athletico Bilbao kwa kuwalaza mabao 2-0.
Mabao yote ya wenyeji wakiwekwa kimiani katika kipindi cha pili na nyota wa Kibrazil, Neymar.
Ijumaa timu za Almeria na Cordoba zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, wakati katika mechi nyingin e za jana,Malaga na Levante zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu huku Celta Vigo na Real Sociedad zikitoka 2-2.

Coastal, Mtibwa kuzionolea makali Simba, Yanga

http://1.bp.blogspot.com/-_EGj1buXwSc/VA8J8hXVRII/AAAAAAAACog/INkR0p5UtIw/s640/DSCN0138.jpg
Coastal Union
http://3.bp.blogspot.com/-WkWCjJdcbyM/UFXn-kbG6pI/AAAAAAAARZc/AvDif8QhyXg/s640/MTIBWA+SUGAR.jpg
Mtibwa Sugar
MABINGWA wa zamani wa soka nchini Coastal Union ya Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro zinatarajiwa kupimana ubavu leo katika pambano la kirafiki litakalochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Mechi hiyo ni ya mwisho mwisho kwa klabu hizo kabla ya kujichimbia kambini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza rasmi Jumamosi.
Kocha mkuu wa Coastal, Yusuph Chipo ametamba kuwa mchezo huo utakuwa kipimo kizuri kwa timu yake ambayo ilijichimba Pemba, na kugawa dozi nene kwa timu pinzani za Zanzibar ilizocheza nayo ambazo kisoka ni tofauti na timu za Tanzania Bara.
Chipo alisema huo utakuwa ni mchezo kwa kikosi chake kabla ya kuinolea makali Simba watakaofungua nao dimba Jumapili.
Mkenya huyo alisema pia mechi hiyo ni nafasi yake ya kupata kikosi cha kwanza kabla ya kuelekea kwenye Ligi Kuu.
"Baada ya mchezo wa Jumapili na Mtibwa Sugar nitatoa tathmini ya wachezaji, ikiwemo kupata kikosi cha kwanza katika timu,"alisema Chipo.
Kwa upande wa Mtibwa kupitia Msemaji wake, Thobias Kifaru naye alitamba kwamba mechi hiyo ni muhimu kwa benchi lo la ufundi kujiweka tayari kuinza ligi kuikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro siku ya Jumamosi ijyo.
"Tupo kamili kwa ajili ya kuonyesha burudani kwa mashabiki wa Tanga sambamba na kuipa makali timu yetu kabla ya kuvaana na Yanga," alisema Kifaru.

Nyatawe 'awafunda' wenzake, ataka wajiheshimu

MUIGIZAJI mahiri wa filamu nchini aliyewahi kutamba na makundi ya Shirikisho Msanii Afrika, Happy Mkamwa 'Nyatawe' amewataka wasanii wenzake wa kike kupenda kujiheshimu na kujithamini ili nao waheshimiwa na kuthaminiwa na jamii.
Aidha aliwataka wasanii nchini kwa ujumla kuwa wabunifu na kuumiza vichwa ili kutoa kazi ambazo zitabamba anga la kimataifa.
Akizungumza na MICHARAZO, Nyatawe alisema wasanii wa kike wanapaswa kujitambua wao ni  nani ndani ya jamii na hivyo kuwa mfano bora kuanzia mavazi yao, matendo na hata kwa kauli zao ili kujijengea heshima mbele ya jamii inayowazunguka.
Alisema kuendelea kufanya mambo ya ovyo yanawashushia heshima na kufanya wadharaulike.
"Wasanii wa kike wa leo ndiyo wazazi na walezi wa kesho wa familia hivyo ni wajibu wetu kuwa makini kwa kila tunalofanya au kulitamka, ili kujenga heshima na hadhi zetu," alisema.
Pia aliwakumbusha wasanii kupenda kuwa wabunifu katika kazi zao pamoja na kujituma kwa bidii ili mwishowe waje kutamba kimataifa badala ya kuridhika na mafanikio ya nyumbani.

Sikinde sasa kuzindua Jinamizi lao Oktoba

http://3.bp.blogspot.com/-J-v3cQW_bXU/TfmmcHJ7o7I/AAAAAAAABG0/P-GhVXbtP5s/s1600/sikinde.JPGBENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' inatarajia kuzindua albamu  yake mpya ya 'Jinamizi la Talaka' mwishoni mwa Oktoba baada ya kushindwa kufanya hivyo  mwezi uliopita.
Aidha bendi hiyo inatarajiwa kufanya ziara ya kimuziki katika mikoa ya Morogoro na Dodoma  wiki ijayo kwa ajili ya kuzitambulisha nyimbo zao mpya za albamu hiyo kwa mashabiki wa mikoa  hiyo.
Msemaji Msaidizi wa Sikinde, Emmanuel Ndege aliiambia MICHARAZO kuwa baada ya kukwama  kufanya uzinduzi wao Agosti kama ilivyokuwa imetangazwa, Sikinde sasa inatarajiwa kuzindua  albamu yao mpya katika maadhimisho ya miaka 38 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Ndege alisema kwa sasa wanaendelea kufanya mchakato wa wadhamini kabla ya kutangaza rasmi  tarehe ya jambo hilo, japo alisisitiza itakuwa mwishoni mwa Oktoba.
"Uzinduzi wa albamu yetu mpya utafanyika Oktoba sambamba na maadhimisho ya miaka 38  tangu kuanzishwa kwa Sikinde," alisema Ndege.
Pia aligusia juu ya ziara ya kimuziki wanaotarajia kuifanya wiki ijayo katika mikoa ya Morogoro na  Dodoma ili kutambulisha nyimbo zao mpya kwa mashabiki wa bendi hiyo wa mikoa husika.
"Tupo katika maandalizi ya kwenda kuzitambulisha nyimbo za albamu yetu mpya katika mikoa ya  Dodoma na Morogoro, tukiwa huko pia tutakumbushia nyimbo za zamani za bendi hiyo zilizoipa  Ubingwa wa Muziki wa Dansi Tanzania," alisema Ndege