STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 14, 2014

Coastal, Mtibwa kuzionolea makali Simba, Yanga

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEih8GIhwPpFvx9y37-dG5TLICcp_KCiphSP1VYgwX79MDr9R3tnTWyceiGkEuX9A89bxtFoklDDQtYSmrAox361CSsxPLNO0QiOzOiXFjYBym8OfCB3s-9GgU3KnI0_8FXHv919Cb0oO1Xk/s640/DSCN0138.jpg
Coastal Union
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbodZ0IJ3DDDukQkZOD3uBBhFnRyS_36bTNfa2lByCz4hi3do7n2ffnbHwJPZ7M927cjrGC4zHIdMWa_k0r-eR3D8YaAO8lvvkkH17E8Xf7I_WhVKdmiJ87gem7uKakkwoXHDsRcIjqCQC/s640/MTIBWA+SUGAR.jpg
Mtibwa Sugar
MABINGWA wa zamani wa soka nchini Coastal Union ya Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro zinatarajiwa kupimana ubavu leo katika pambano la kirafiki litakalochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Mechi hiyo ni ya mwisho mwisho kwa klabu hizo kabla ya kujichimbia kambini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza rasmi Jumamosi.
Kocha mkuu wa Coastal, Yusuph Chipo ametamba kuwa mchezo huo utakuwa kipimo kizuri kwa timu yake ambayo ilijichimba Pemba, na kugawa dozi nene kwa timu pinzani za Zanzibar ilizocheza nayo ambazo kisoka ni tofauti na timu za Tanzania Bara.
Chipo alisema huo utakuwa ni mchezo kwa kikosi chake kabla ya kuinolea makali Simba watakaofungua nao dimba Jumapili.
Mkenya huyo alisema pia mechi hiyo ni nafasi yake ya kupata kikosi cha kwanza kabla ya kuelekea kwenye Ligi Kuu.
"Baada ya mchezo wa Jumapili na Mtibwa Sugar nitatoa tathmini ya wachezaji, ikiwemo kupata kikosi cha kwanza katika timu,"alisema Chipo.
Kwa upande wa Mtibwa kupitia Msemaji wake, Thobias Kifaru naye alitamba kwamba mechi hiyo ni muhimu kwa benchi lo la ufundi kujiweka tayari kuinza ligi kuikaribisha Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro siku ya Jumamosi ijyo.
"Tupo kamili kwa ajili ya kuonyesha burudani kwa mashabiki wa Tanga sambamba na kuipa makali timu yetu kabla ya kuvaana na Yanga," alisema Kifaru.

No comments:

Post a Comment