STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 10, 2013

K-Guitar wa Bana Marquiz Usikate Tamaa


K- Guitar
MUIMBAJI wa bendi ya muziki wa dansi, Kelvin Nyoni 'K Guitar', amefyatua wimbo mpya binafsi  uitwao 'Usikate Tamaa' katika miondoko ya Bongofleva akiwa mbioni kutoa albamu yake nje ya  bendi hiyo inayoongozwa na mkongwe, Tshimanga Kalala Assosa 'Mtoto Mzuri'.
Akizungumza na MICHARAZO, muimbaji huyo wa zamani wa bendi ya Victoria, alisema wimbo huo  ambao anajiandaa kuanza kuusambaza katika vituo vya redio ni kati ya nyimbo tatu zilizokamilika  kwa ajili ya albamu yake ijayo.
K-Guitar alisema hata hivyo kwa sasa anasaka meneja wa kumsaidia kusimamia kazi zake, akiamini  bila usimamizi wa mtu makini lengo lake la kutoa albamu halitaweza kufanikiwa kama atakavyo.
"Nimerekodi wimbo mmoja uitwao 'Usikate Tamaa' huku nyingine mbili za 'Subira' na 'Zawadi'  zikiwa zinasubiri kurekodiwa, ila nitafanya hivyo nikifanikiwa kupata meneja wa kusimamia kazi  zangu," alisema muiimbaji huyo ambaye pia ni mahiri kwa kupiga gitaa la rythim.
Muimbaji huyo alisema kwa vile yeye ni mwanamuziki wa Bana Marquiz akipata meneja wa  kumsimamia kazi zake binafsi kama msanii wa kujitegemea itamsaidia kutumikia 'mabwana wawili'  bila tatizo.
Kabla ya kuibukia kwa Assosa, muimbaji huyo aliwahi kuachia wimbo katika muziki wa kizazi kipya  uitwao 'Mapenzi Siyo Pesa' ambao ameurudia akiwa na Bana Marquiz aliyonayo tangu mwaka  2010.

No comments:

Post a Comment