STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 9, 2013

Diamond, Wema Sepetu, kitu na box

BAADA YA kuzikanusha taarifa kwamba amerudiana na zilipendwa wake, Wema Sepetu imefahamika wazi kwamba Diamond Platnumz sasa ni kitu na box na mlimbwende huyo.
aada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Awali kulikuwa na taarifa wawili hao wamerudiana walipokuwa Malaysia Diamond alipoenda kutumbuiza na Wema kwa shughuli zake binafsi, lakini msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya alikanusha.
Hata hivyo picha zilizonaswa zimewaonyesha wawili hao walikuwa wakiuhadaa umma kwani hakuna ubishi ni ng'ari ng'ari mwanzo mwisho.


Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny

Nini nitakachofuata...TUSUBIRI!

BaabKubwa

Mbeya City yazidi kupepea, Azam, Mtibwa Sugar wazinduka


Mbeya City

WAKATI Azam ikizinduka na kuondoka na 'mdudu' wa sare baada ya kuitungua Mgambo JKT mabao 2-0, wageni wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mbeya City ya jijini Mbeya imeendelea kutakata baada ya kuisasambua Rhino Rangers nyumbani kwao mjini Tabora kwa kuilaza mabao 3-1.

Ushindi wa timu hizo mbili zimezifanya ziisogelee Simba kwa kufikisha pointi 14, moja pungufu na zile ilizonazo vinara hao ambao leo hawakushuka dimbani.
Azam ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na shukrani zikienda kwa kinda Faridi Mussa Maliki na Kipre Tchetche na kuipeleka Azam hadi nafasi ya pili mbele ya Mbeya City wakizidi kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine, Ruvu Shooting imetoshana nguvu dhidi ya maafande wenzao wa Oljoro JKT baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, mabao ya timu hizo yakifungwa na Elias Maguri wa Ruvu na Fikiri Mohammed wa Oljoro waliyofunga kila mmoja mawili.
Nao mabingwa wa zamani wa Tanzania, Mtibwa Sugar imezinduka nyumbani kwao Manungu Morogoro baada ya kuwatungua JKT Ruvu mabao 2-1 na kujivuta hadi nafasi ya tisa.
Mabao mawili ya Juma Luizio yalitosha kuibeba Mtibwa ambao mwishoni mwa wiki walinyanyaswa na Yanga kwa kulazwa mabao 2-0, na mkongwe Salum Machaku akiifungia JKT bao pekee la kufutia machozi.

Mfanyabiashara mwingine amwagiwa Tindikali, safari hii Arusha

 
MFANYABIASHARA mkazi wa Sakina jijini Arusha, Japhet Minja anadaiwa kumwagiwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni tindikali na watu wasiofahamika na kuachwa na majeraha usoni na mikononi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha zinasema kuwa Minja alikumbwa na tukio hilo eneo la Shamsi Kata ya Elarai baada ya kumwagiwa kimiminika hicho na kuachwa na maumivu makali.
Akizungumza katika hospital ya Seriani alikola wa, Minja ambae ni mfanyabiashara adai alisimamishwa na watu waliomtaka kuongozana nao kwa ajili ya masuala ya kibiashara na ghafla wakiwa njiani ghafla alizuiwa na watu hao waliofunga njia na kumdhuru.
Daktari wa zamu aliyempokea mgonjwa huyo Godbless Masawe amesema walimpokea
mgonjwa huyo jana asubuhi akiwa na fahamu lakini baadae hali ilibadilika na
kulazimika kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi na kwa sasa Minja anaendela vyema kwa sasa.

Yaillah Toba, Ajali nyingine tena yahusisha magari matatu

  GA
 Lori la Mizigo likiwa limeacha njia leo, baada ya kugongana na basi katika eneo la Kabuku mkoani Tanga na kuyahusisha magari matatu katika ajali hiyo. (Picha na Francis Dande) 
 Askari wa usalama barabara wakiwa katika eneo la tukio.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali iliyoyakutanisha malori mawili pamoja na basi la abiria lenye namba za usajili T 158 BXG, iliyotokea leo katika eneo la Kabuku, mkoani Tanga

Uchaguzi Bodi ya Ligi wapigwa dochi, Rufaa za wagoimbea TFF kupitiwa kesho


Na Boniface Wambura
UCHAGUZI wa viongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) sasa utafanyika Oktoba 25 mwaka huu badala ya Oktoba 18 mwaka huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesogeza mbele uchaguzi huo kutokana na maombi ya Kamati ya Ligi kwa vile baadhi ya wajumbe wa Baraza la Bodi hiyo kuwa vilevile wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.

TFF itafanya Mkutano Mkuu wake Oktoba 26 mwaka huu ambao utakuwa na ajenda za kawaida kama zilivyoainishwa katika Katiba yake wakati ajenda ya uchaguzi itakuwa Oktoba 27 mwaka huu.

Wagombea uongozi TPL Board ni Hamad Yahya Juma anayewania nafasi ya Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Abeid. Wanaowania nafasi za ujumbe katika Kamati ya Uongozi ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib Mwindadi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni inatarajia wakati wowote kutangaza tarehe ya kuanza kampeni kwa wagombea katika uchaguzi huo. Baraza la Bodi linaundwa na wajumbe 38 ambao ni wenyeviti 14 wa klabu za Ligi Kuu na wenyeviti 24 wa klabu za Daraja la Kwanza.
Wakati huo huo Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda itakutana keshokutwa (Oktoba 10 mwaka huu) kusikiliza rufani zilizowasilishwa mbele yake.

Waombaji uongozi watatu wamekata rufani katika Kamati ya Jaji Luanda wakipinga kutopitishwa kugombea katika uchaguzi wa TFF, uamuzi uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ajili ya uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Warufani ni Samwel Nyalla aliyeondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda namba 2 ya mikoa ya Mara na Mwanza kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi TFF kwa kutoonesha malengo yake.

Ayoub Nyaulingo yeye anapinga kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda namba 6 (Katavi na Rukwa) kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

Naye Ayoub Nyenzi amekata rufani kupinga kuondolewa kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha Kanda namba 7 (Iringa na Mbeya) kwa kushindwa kuthibitisha uraia wake.

Ndanda, Green Warriors hapatoshi leo FDL

Na Boniface Wambura
GREEN Warriors ya Dar es Salaam na Ndanda ya Mtwara zinaumana kesho (Oktoba 9 mwaka huu) katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mshindi atakamata uongozi wa kundi A.

Mechi hiyo ya raundi ya tano itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo timu itakayoshinda itafikisha pointi kumi na kuipiku African Lyon inayoongoza sasa kundi hilo ikiwa na pointi tisa.

Kwa upande wa kundi B kutakuwa na mechi tatu ambapo Polisi Morogoro inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi tisa itakuwa ugenini dhidi ya Majimaji inayokamata mkia ikiwa na pointi moja. Mechi itachezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kurugenzi itakuwa kwenye uwanja wake wa Wambi ulioko Mafinga mkoani Iringa kuikabili Burkina Faso ya Morogoro wakati Uwanja wa CCM Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Kimondo na Mkamba Rangers.