STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 30, 2013

David Mwantika amrithi Kelvin Yondani Taifa Stars, kocha Kim Poulsen amuita kikosini

Beki David Mwantika (kulia) aliyeitwa Taifa Stars kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki wa Azam, David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. 

Mbali na Yondani Stars ina wachezaji majeruhi watatu ambao kocha Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao. 

Wachezaji hao ni Athuman Idd 'Chuji' , Shomari Kapombe na John Bocco 'Adebayor'.

Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. 

Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BIL. 5.5/-

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.

Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.

Gervinho achekelea kuhama Arsenal

http://u.goal.com/310700/310729_heroa.jpg
MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Gervinho (26) amebainisha kwamba alifurahi sana kuondoka Arsenal.
Nyota huyo amesema alikuwa na maisha magumu London Kaskazini na kwamba ilipotokea ofa ya kuondoka aliichangamkia haraka.
Gervinho alishuka kiwango na akashindwa kuonyesha makali yake Arsenal baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa paundi milioni 10.8 akitokea Lille mwaka 2011.
Alikamilisha uhamisho wake wa kutua Roma mapema katika kipindi hiki cha usajili chini ya kocha wake wa zamani wa Ufaransa, Rudi Garcia na amesema atatisha chini ya kocha huyo.
Nyota huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 8 alisema: "Ilikuwa ni faraja kubwa kwangu kuchezea Arsenal, lakini baada ya miaka miwili ya kupanda na kushuka ilikuwa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.
"(Arsene) Wenger, nadhani ni kocha mkubwa. Ni mtu ambaye namheshimu sana na nina furaha kubwa kupata fursa ya kucheza katika timu yake. Nadhani washambuliaji wanahitaji kuaminiwa na kocha wao na kupewa muda mwingi wa kucheza. Nilitamani nami iwe hivyo. Lakini ukurasa huo umepita mambo yamebadilika. Naweka akiliyangu yote Roma.
"Roma ni timu kubwa yenye kocha mkubwa. Sikujiuliza kukubali ofa yao.
"Daima nina mahusiano mazuri na Garcia - amekuwa akinijengea kujiamiani daima, na alikuwa ndiye kocha wa kwanza kunichezesha kwenye wingi.
"Nataka kuonyesha naweza kuisaidia timu. Siko katika hali nzuri kimwili kwa sasa, lakini Garcia ananifahamu vyema, nina kazi ya kufanya ili niwe fiti tena."
(Talksport)

Diamond nouma, amzawadia Mzee Gurumo gari...wengine mpo...!

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Show.
Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

STAA wa nyimbo za 'Kesho', 'Nataka Kulewa', 'Mawazo' na vingine, Naseeb Abdul ameonyesha mfano kwa wadau wa muziki nchini baada ya kumzawadiwa gari mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyetangaza kustaafu, Muhidini Gurumo.
Diamond alimkabidhi Gurumo gari hilo kuonyesha kujali na kuthamini mchango wa mwanamuziki huyo, baada ya hivi karibuni kunukuliwa 'akilia' kwamba kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa mwanamuziki anastaafu akiwa hana hata baiskeli.
Alichokifanya Diamond ni jambo la kupongezwa na kuigwa na wadau wengine wa muziki kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe (Gurumo) kwamba angependa ale jasho na kupewa pongezi zake angali hai badala ya watu kumsubiri afe ndipo watu wajitokeze kumwagia sifa na kujifanya kumuenzi wakati akiwa hao walimtelekeza.
MICHARAZO inakupa pongezi Diamond na tunawaomba wengine wamsadie mkongwe huyo ambaye amestaafu siyo kwa sababu ya kuishiwa kimuziki, bali hali yake ya kiafya akisumbuliwa na maradhi na wenye kutaka kumchangia watume fedha kwa njia ya TiGO Pesa katika simu yake ya mkononi 0655-401383.

Thursday, August 29, 2013

Frank Ribery ndiye Mchezaji Bora Barani Ulaya awabwaga Messi na Ronaldo

Frank Ribery ambaye kiimani ni Muislam akiomba dua kabla ya kuanza pambano la soka la timu yake ya Bayern Munich

NYOTA wa Kifaransa anayeichezea klabu ya Bayern Munich, Frank Ribery amewagaragaza wakali wa Hispania, Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo kwa kunyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2012-2013.
Mkali huyo aliyeisaidia Bayern Munich kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa ya Ulaya na mengine mawili ya Ligi ya Ujerumani alitangazwa kunyakua tuzo hiyo leo barani humo.
Ribery amenyakua tuzo hiyo akimpokea Iniesta wa Barcelona aliyenyakua msimu uliopita akitanguliwa na Messi aliyetwaa mwaka 2010-2011.
Nafasi ya pili katika kimyang'anyiro hicho ilienda kwa Messim kisha Ronaldo aliyeshina nafasi ya tatu, ingawa hjakuweza kuhudhuria sherehe hizo zilizoenda sambamba na kutangazwa kwa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2013-2014.

Rais Kikwete amteua Kamishna Mkuu Idara ya Uhamiaji

Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
 
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.
Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza
 
Rais pia amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.
 
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.
 
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
 
 
 

Makundi UEFA League yatoka, Barca, Milan, Ajax chungu kimoja

MAKUNDI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yametangazwa leo ambapo mabingwa wa Hispania, Barcelona wametupwa kundi moja na AC Milan na Ajax, wakati Chelsea wameweka kundi moja na 'wasumbufu' Basel.
Makundi kamili ya ligi hiyo ambapo mabingwa wake watetezi ni Wajerumani Bayern Munich, ni kama yafuatayo;
 
Group A
Man. United (ENG)
Shakhtar Donetsk(UKR)
Leverkusen(GER)
Real Sociedad(ESP)
Group B
Real Madrid(ESP)
Juventus(ITA)
Galatasaray(TUR)
København(DEN)
Group C
Benfica(POR)
PSG(FRA)
Olympiacos(GRE)
Anderlecht(BEL)
Group D
Bayern(GER)
CSKA Moskva(RUS)
Man. City(ENG)
Plzeň(CZE)
Group E
Chelsea(ENG)
Schalke(GER)
Basel(SUI)
Steaua(ROU)
Group F
Arsenal(ENG)
Marseille(FRA)
Dortmund(GER)
Napoli(ITA)
Group G
Porto(POR)
Atlético(ESP)
Zenit(RUS)
Austria Wien(AUT)
Group H
Barcelona(ESP)
Milan(ITA)
Ajax(NED)
Celtic(SCO)

'Bondia Ibrahim Maokola hajakamatwa, katelekezwa Italia'

https://fbcdn-sphotos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/944257_379837705469127_1264255997_n.jpg
Bondia Ibrahim Maokola
 KOCHA wa bondia machachari wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Maokola, Chaurembo Palasa amekanusha taarifa kwamba bondia huyo amekatwa nchini Italia kwa tuhuma za dawa za kulevya.
Badala yake Palasa alisema Maokola, aliyechukuliwa na promota maarufu nchini Shomari Kimbau ametelekezwa na promta huyo akiwa hana tiketi ya kurejea nchini.
Palasa alisema bondia wake alichukuliwa kinyemela na Kimbau kwenda kupigana na mipango ikaenda hovyo na Kimbau kumtoroka na kumuacha akiwa hana msaada wowote mpaka sasa na siyo kweli kama katiwa mbaroni kwa tuhuma za dawa za kulevya kama ilivyoelezwa na gazeti moja la kila wiki.
"Bondia Ibrahim Maokola, hajakamatwa Italia kama ilivyoripoti gazeti la ....la wiki iliyopita. Bondia Maokola alichukuliwa na Shomari Kimbau kwenda kupigana ngumi Italia mpaka muda huu bondia huyo ametelekezwa ghetto akiwa hana tiketi ya kurudi Tanzania," Palasa aliiambia MICHARAZO.
Awali ilielezwa kuwa bondia huyo na promota huyo walinaswa Italia kwa tuhuma kwamba walipeleka dawa za kulevya, ingawa hakuna uthibitisho wowote uliowahi kutolewa kuthibitisha taarifa hizo na hivyo meneja huyo wa Maokola ameamua kuweka sawa ili kusafisha hali ya hewa ambayo ilianza kumchafukia bondia wake wakati yupo kwenye matatizo, yeye akijaribu kuwasiliana na familia yake ili kumsaidia arejee nchini..

Yanga, Coastal Union wavuna Sh . Mil. 152

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj404PkGb7SiEVuMydJgAD5SUi1Dn7qkqZ-XJCGqQF3h-FdUmM4SqgP3xdez_ThTpx8JPnrFmD3GbEKygqyxzrpvY7SJWe6UDXkWzwSGti0PPt1pVV8_19cFA9PBY88prvEcTXFt_7qkmc/s640/IMG_3331.JPG
Na Boniface Wambura
PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Coastal Union lililochezwa jana (Agosti 28 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 152,296,000.

Watazamaji 26,137 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 23,231,593.22.

Mgawo mwingine ni asilimia 15 ya uwanja sh. 18,786,827.52, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 11,272,096.51, Kamati ya Ligi sh. 11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,383,593.09.

Golden Bush kukipiga Pugu, yamnyatia George Masatu

http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AH1bimIAABNxUh7nBQAAAM7weWo&midoffset=2_0_0_1_1255535&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
BAADA ya kushindwa kutambiana na Mwanza United Veterani kwa kutoka sare ya mabao 4-4, wakali wa soka jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani Jumamosi inatarajiwa kuwafuata Pugu Veterani kwao kwa ajili ya pambano la kirafiki litakalofanyika Pugu Kajiungeni, nje kidogo ya jiji la Dar.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' ni kwamba pambano hilo litachezwa majira ya asubuhi na kuna uwezekano kikosi chao kikamtumia kwa mara ya kwanza nyota wa zamani wa Pamba, Simba na Taifa Stars, George Masatu.

Ticotico alisema Golden Bush imevutiwa na Masatu baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika mechi ya kirafiki baina yao na kwamba walikuwa katika 'mazungumzo' ya kumsajili rasmi katika kikosi chao ili aweze kuanza kuitumikia Golden Bush dhidi ya Pugu Veterani.

Msemaji huyo ambaye pia ni mmoja wa washambuliaji tegemeo wa timu hiyo, alisema mazungumzo ya kumnyakua Masatu ili kumahamisha kutoka Mwanza United yanafanywa na mwanasheria wa timu ya Golden Bush Godfrey Chambua  a.k.a Zacharia Hans Poppe.

"Bwana Poppe aliyeshikana mkono na Athumani Machuppa pichani ndiye aliyewezesha usajili wa akina Athuman Machuppa na Sadik Muhimbo ambao wote wametolewa kwa mkopo timu za Sweden na DRC," alisema Ticotico.

Kabla ya pambano hilo kulikuwa na mipango Golden Bush iumane na TASWA, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Ticotico, wanahabari hao wamechomoa kiaina na wao kulazimika kusafiri hadi Pugu Kajiungeni ili kugawa dozi kwa wapinzani wao kama inavyofanywa kwa viklosi vingine jijini Dar es Salaam.

Copa Cola Cola Kanda kuanza Septemba 2

Na Boniface Wambura
MICHUANO ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 inayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani inaanza kutimua vumbi Septemba 2 mwaka huu katika vituo sita tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa leo (Agosti 29 mwaka huu), kituo cha Mwanza mechi zake zitachezwa katika viwanja vya Alliance ambapo timu zitakazofungua dimba ni Kagera vs Kigoma, Mara vs Tabora, Simiyu vs Geita na Mwanza vs Shinyanga.

Kituo cha Mbeya ambapo mechi zitachezwa viwanja vya Iyunga ni Katavi vs Njombe, na Ruvuma vs Mbeya. Kituo cha Pwani ni Ilala vs Kaskazini Unguja, na Lindi vs Pwani.

Ufunguzi katika kituo cha Arusha ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid ni Manyara vs Kilimanjaro, na Arusha vs Singida.

Uwanja wa Jamhuri ambapo utatumika kwa mechi za kituo cha Morogoro, Tanga itacheza na Dodoma wakati Morogoro itaumana na Temeke. Mjini Zanibar kwenye Uwanja wa Chuo cha Amaan ni kati ya Kaskazini Pemba na Mjini Magharibi, na Kusini Pemba dhidi ya Kusini Unguja.

USAILI WAGOMBEA TFF, TPL BOARD KUANZA KESHO


Na Boniface Wambura
USAILI kwa wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi wa Ligi Kuu (TPL Board) unaanza kesho (Agosti 30 mwaka huu).

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Agosti 30 mwaka huu ni usaili kwa waombaji uongozi wote katika Bodi ya Ligi Kuu pamoja na waombaji uongozi wa TFF kwa kanda namba 11 (Morogoro na Pwani), kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) na kanda namba 13 (Dar es Salaam).

Agosti 31 mwaka huu ni kanda namba sita (Rukwa na Katavi), kanda namba saba (Mbeya na Iringa), kanda namba nane (Njombe na Ruvuma), kanda namba tisa (Lindi na Mtwara) na kanda namba kumi (Dodoma na Singida).

Usaili kwa kanda namba moja (Geita na Kagera), kanda namba mbili (Mara na Mwanza), kanda namba tatu (Simiyu na Shinyanga), kanda namba nne (Arusha na Manyara) kanda namba tano (Kigoma na Tabora), na nafasi za Rais na Makamu wa Rais wa TFF utafanyika Septemba Mosi mwaka huu.

Waombaji wote wamepangiwa muda wao wa usaili. Kwa mujibu wa ratiba usaili ufanyika kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi saa 2 usiku. Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia muda waliopangiwa.

Duniani kuna Mambo! Wanaume China wanakodisha wanawake kunyonya maziwa yao kama vichanga



GAZETI la Morning Post la China Kusini limeripoti kwamba watu wazima nchini humo wanawalipa wanawake fedha ili wawanyonyeshe maziwa yao ya kifuani !.
Wanawake wanaojitolea kutoa maziwa yao hulipwa kiasi cha dola 2,700 za Marekani  (kama sh. Milioni 4) kwa mwezi ambapo watu wazima hao huweza kuyanyonya maz
iwa hayo moja kwa moja kutoka vifuani mwa kinamama hao kama watoto wadogo !.

Watu wengi wanaona jambo hilo ni la ajabu kwa mwanamme au mwanamke mzima kunyonya matiti ya mwanamke mwenzake.  Hata hivyo, nyuma ya kituko hicho kuna habari kwamba watu wanaofanya hivyo ni wale wenye magonjwa sugu na ambao wanashindwa kupata chakula kizuri chenye rutuba ya asili, badala ya vyakula vingi nchini humo ambavyo vimechakachuliwa.

Hivyo katika mazingira ya uchakachuaji huo ambayo yameenea nchini humo, watu wanakimbilia kwenye maziwa ya kinamama ambayo wanaona ndicho chakula halisi na cha asilia na chenye viini vingi vyenye kuimarisha afya ya binadamu.

Pamoja na hivyo, maoni ya watu ni kwamba iwapo watu wengine wanawakodisha kina mama hao kwa ajili tu ya kufanya kitu hicho kama burudani, basi kitendo hicho si cha kiungwana, lakini kama kweli wanafanya hivyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao, hatua hiyo ni jambo jema.

Mwanajeshi wa Tanzania afa Goma- DR Congo


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
Simu ya Upepo  : “N G O M E”                                             Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo  : DSM  22150463                                         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                                       DAR ES SALAAM,   29  Agosti, 2013.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe         : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                   : www.tpdf.mil.tz
                  
TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI-DRC,GOMA

1.       Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO.

2.       Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha Majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3.       MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.