STRIKA
USILIKOSE
Friday, August 30, 2013
Gervinho achekelea kuhama Arsenal
MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Gervinho (26) amebainisha kwamba alifurahi sana kuondoka Arsenal.
Nyota huyo amesema alikuwa na maisha magumu London Kaskazini na kwamba ilipotokea ofa ya kuondoka aliichangamkia haraka.
Gervinho alishuka kiwango na akashindwa kuonyesha makali yake Arsenal baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa paundi milioni 10.8 akitokea Lille mwaka 2011.
Alikamilisha uhamisho wake wa kutua Roma mapema katika kipindi hiki cha usajili chini ya kocha wake wa zamani wa Ufaransa, Rudi Garcia na amesema atatisha chini ya kocha huyo.
Nyota huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 8 alisema: "Ilikuwa ni faraja kubwa kwangu kuchezea Arsenal, lakini baada ya miaka miwili ya kupanda na kushuka ilikuwa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.
"(Arsene) Wenger, nadhani ni kocha mkubwa. Ni mtu ambaye namheshimu sana na nina furaha kubwa kupata fursa ya kucheza katika timu yake. Nadhani washambuliaji wanahitaji kuaminiwa na kocha wao na kupewa muda mwingi wa kucheza. Nilitamani nami iwe hivyo. Lakini ukurasa huo umepita mambo yamebadilika. Naweka akiliyangu yote Roma.
"Roma ni timu kubwa yenye kocha mkubwa. Sikujiuliza kukubali ofa yao.
"Daima nina mahusiano mazuri na Garcia - amekuwa akinijengea kujiamiani daima, na alikuwa ndiye kocha wa kwanza kunichezesha kwenye wingi.
"Nataka kuonyesha naweza kuisaidia timu. Siko katika hali nzuri kimwili kwa sasa, lakini Garcia ananifahamu vyema, nina kazi ya kufanya ili niwe fiti tena."
(Talksport)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment