STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 30, 2012

MASHETANI WEKUNDU HOI KWA SPURS, YALALA OLD TRAFFORD




Jan Vertonghen akishangilia bao aliloifungia timu yake ya Tottenham dhidi ya Manchester United jana. Picha:Reuters


TIMU ya soka ya Tottenham Hotspurs chini ya kocha wake Andre Villa Boas jana walivunja mwiko wa kutoifunga Manchester United kwa muda mrefu baada ya kuwalaza Mashetani Wekundu hao kwenye dimba lao la nyumbani la Old Frafford kwa mabao 3-2.
Bao la mapema lililofungwa na Vertonghen liliwachanganya Man United kabla ya kukujikuta wakifungwa jingine nusu saa baadae na Garret Bale na kuwafanya Spurs kwenda mapumziko wakiongoza mabao 2-0.
Katika mechi nyingine, vinara wa ligi hiyo Chelsea wameendelea kung'ara kwa kuilaza Arsenal mabao 2-1, huku Liverpool ikitoa kisango cha 'mbwa mwizi' kwa Norwich City kwa kuilaza mabao 5-2, huku jahazi la Swansea City likiendelea kuzama kwa kulazwa mabao 2-0 na Stoke City mabao yote yakitupiwa kambani na Peter Crouch.
Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu ya England kwa jana ni kama iofuatavyo:


29 September
Man Utd2 - 3Tottenham
LCAdC Nani (50)
S Kagawa (53)

J Vertonghen (1)
G Bale (31)
CD Dempsey (51)
Old TraffordAttendance (75566)
Teams | Report
29 September
Stoke2 - 0Swansea
P Crouch (11)
P Crouch (35)

Britannia StadiumAttendance (27330)
Teams | Report

29 September
Norwich2 - 5Liverpool
S Morison (60)
G Holt (86)

L Suarez (1)
L Suarez (37)
N Sahin (46)
L Suarez (56)
S Gerrard (67)
Carrow RoadAttendance (26831)
Teams | Report
29 September
Sunderland1 - 0Wigan
S Fletcher (50)
Stadium of LightAttendance (37742)
Teams

29 September
Fulham1 - 2Man City
M Petric (pen 9)
SL Aguero (42)
E Dzeko (86)
Craven CottageAttendance (25698)
Teams
29 September
Everton3 - 1Southampton
L Osman (24)
N Jelavic (31)
N Jelavic (37)

G Ramirez (5)
Goodison ParkAttendance (37922)
Teams

29 September
Reading2 - 2Newcastle
JB Kebe (57)
N Hunt (61)

D Ba (57)
D Ba (82)
Madejski StadiumAttendance (24097)
Teams | Report
29 September
Arsenal1 - 2Chelsea
YK Gervinho (41)
FJS Torres (19)
JMG Mata (52)
Emirates StadiumAttendance (60101)
Teams | Report

Yanga, Lyon kujiuliza leo Taifa

MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga leo ikiwa chini ya kocha wake mpya, Ernstus Brandts inatarajiwa kuivaa Africna Lyon katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara pambano litakalofanyika kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Yanga ambayo imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja kocha huyo kutoka Uholanzi, itaikaribisha Lyon ikiwa bado inachekelea ushindi mnono wa mabao 4-1 iliyopata dhidi ya JKT Ruvu.
Pambano hilo ambalo litarushwa hewani na kituo cha Super Sport katika ule muendelezo wa Tanzania Weekend Soccer, linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wa Yanga kutoka kupokea kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Prisons ya Mbeya.
Yanga itahitajika ishinde ili kujiweka pazuri kabla ya kuvaana na watani zao keshokutwa kwenye pambano lao la kwanza ambapo wana Jangwani wana deni kubwa la kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0 katika mechi ya kufungia msimu uliopita.
Mbali na deni hilo la karibuni, pia Yanga ina deni la miaka 37 la kipigo cha mabao 6-0 ilichopewa mwaka 1977 ambacho imekuwa ikihangaika kukirudisha bila ya mafanikio.
Bila shaka pambano hilo litakuwa kipimo kizuri kwa makocha wa timu hizo mbili, Brandts wa Yanga na Muargentina anayeinoa Lyon, iliyoshinda mechi moja tu kama wapinzani wao hao wanaovaana wakiwategemea mshambiliaji wake nyota, Adam Kingwande na wengineo.

SIMBA YAREJEA KILELENI, YAITUNGUA PRISONS 2-1

 
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu, Simba jana waliendelea kutakata kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuitandika Prisons ya Mbeya mabao 2-0 na kurejea kileleni wakiiondosha Azam Fc iliyowaengua kwa saa kadhaa.
Bao la kwanza la Mrisho Ngassa kwa timu hiyo ndilo lililoipa Simba ushindi iliyomaliza mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa wachezaji tisa uwanjani.
Kwa ushindi huo, Simba imeendelea kuwa timu pekee yenye matokeo ya asilimia 100 baada ya raundi nne, ikiwa na pointi 12, mbili juu ya Azam, katika pambano lililohudhuriwa na watazamaji wachache kuliko kawaida ya mechi za mabingwa watetezi hao.
Coastal Union ni ya tatu ikiwa na pointi nane, tatu juu ya Prisons ambayo imeshuka kwa nafasi moja mpaka kuwa timu ya tano nyuma ya JKT Oljoro kwa uwiano wa mabao, zote zikiwa na pointi tano baada ya michezo minne.
Siku iliisha vibaya kwa Simba baaada ya beki wake Amiri Maftaha kuonyeshwa kadi nyekundu na muamuzi Paul Soleji dakika mbili kabla ya filimbi ya miwsho, baada ya kumchezea rafu mbaya Khalid Fupi.
Siku ilianza vibaya pia kwa Simba baada ya Lugano Mwangama kuipatia Prisons bao la kuongoza katika dakika ya saba tu ya mchezo kwa shuti kali ambalo lilimbabatiza beki Juma Nyoso wa Simba kabla ya kutinga wavuni, kwenye Uwanja wa Taifa.
Iliichukua Simba kipindi kizima cha kwanza kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Felix Sunzu katika dakika ya 45 akiunganisha krosi ya Mwinyi Kazimoto.
Kama alivyomalizia ngwe ya kwanza, Sunzu angeweza kuongeza idadi ya mabao ya Simba dakika tatu tangu kuanza kwa kipindi cha pili lakini shuti lake kutokana na pasi ya Mrisho Ngassa lilipaa juu.
Ndipo Ngassa alipochukua jukumu la kusahihisha kosa hilo mwenyewe dakika saba baadaye kwa shuti lililomshinda David Abdallah kuzuia katika lango la Prisons, akiunganisha krosi ya Said Nassoro.  
Simba iliwatoa Amri Kiemba na nafasi yake kuchukuliwa na Salim Kinje, Ramadhani Chombo aliyempisha Jonas Mkude na Edward Christopher kwa Daniel Akuffor baada ya goli la Ngassa ikiwa ni jitihada za kutawala zaidi mechi hiyo, lakini hapakuwa na goli la ziada.
Kocha wa Simba Milovan Circovic alisema timu yake ilipata ushindi kutokana na kucheza vizuri, na akasikitikia athari za kadi nyekundu ya Maftah ingawa alisema kuna wachezaji wa kuziba pengo lake.
Timu zilikuwa:
SIMBA: Juma Kaseja, Nassoro Masoud, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Juma Nyoso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba (Salim Kinje dk.74), Ramadhani Chombo (Jonas Mkude dk.67), Edward Christopher (Daniel Akuffor dk.76), Felix Sunzu, Mrisho Ngassa.
PRISONS: David Abdallah, Aziz Sibo, Laurian Mpalile, Lugano Mwangama, David Mwantika, Khalid Fupi, Misango Magai, Fred Chudu, Elias Maguri, Peter Michael (Sino Agustino dk.67), John Matei.

 

 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Felix Sunzu (kulia)
 Mashabiki wa Simba wakishangilia
 Mshambuliaji wa Simba, mrisho Ngasa akichuana na nahodha wa Tanzania Prisons, Lugano Mwangama
 Golikipa wa Prisons, David Abdallah akiokoa hatari langoni mwake
Wachezahi wa Prisons ya Mbeya wakiongozwa na kipa wao kuomba dua wakati wa mapumziko





CHEKA AMCHAPA TENA NYILAWILA SAFARI HII KWA KO

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana

Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa akashindwa kuendelea picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BINGWA wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC, Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana mpinzani katika ngumi hizo nchini baada ya kumchapa kwa KO mpinzani wake mkubwa, Karama Nyilawila na kuongeza taji jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika raundi ya sita ya pam,bano hilo lililokuwa la uzani wa Super Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi zote tano za kwanza Nyilawila akionyesha kumdhibiti Cheka kwa kumchezea 'kibabe' akitumia nguvu nyingi kujihami na baadhi ya watu ukumbini kuamini mwisho wa tambo za Cheka zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo raudni ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallahj Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake.
Mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima kuripuka kwa shangwe akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga Nyilawila.
Kabla ya pambano hilo lililoanza majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na mapambano saba ya utangulizi pamoja na burudani ya muziki toka bendi ya Mashujaa ambao hata hivyo sio wapenzi wengi walioweza kuishuhudia kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika pambano la kwanza la utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi Dickson Mwakipesile, Juma Kihiyo alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola katika pambano lililovutia kwa namna mabondia hao walivyoonyeshana kazi.
Pia mdogo wa Cheka, Cosmas Cheka alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Fadhil Awadh katika pamnbano jingine lililosisimua wengi kwa ufundi uliokuwa ukionyesha na mabondia hao, naye Shaaban Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Khalfan Jumanne.
Michezo minginme iliwakutanisha Stan Kessy na Seba Temba, pambano lililoisha kwa mabondia hao kutoka sare na Hassani Kidebe alitolewa nishai na Deo Samwel kwa kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ambaye aliutangazia umma kwamba kama Mlezi wa Ngumi za Kulipwa amefanikiwa kuwafuta wafadhili katika mchezo huo na kumtambulisha raia mmoja wa kigeni kwamba ni miongoni mwao.

Saturday, September 29, 2012

ZUNGU JIPYA YANGA LAAHIDI KUUA MNYAMA JUMATANO TAIFA

KOCHA MPYA YANGA AJIFUNGA MWAKA YANGA


Kocha mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Upande wa Yanga, uliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga ambaye alishuhudiwa na viongozi wengine wa klabu hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro, Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako na Majjid Suleiman, mmoja wa watu muhimu kwenye klabu hiyo.
Brandts kulia na Sanga kushoto

Anamwaga wino

Brandts kulia na Sanga kushoto

Brandts na Sanga

Brandts na Sanga

Brandts na Sanga

Brandts na Sanga

Mkutano

Mwalusako akimshuhudia Sanga

Dina Ismail na Vicky Kimaro kazini

Brandts akifafanua jambo, kulia ni Majjid

Katabaro na Mwalusako

Makuburi Ally, pembezi ni wazee wa Yanga wakipiga chabo
CHANZO:BIN ZUBEIRY

Huyu ndiye Hemed Morocco kocha mpya wa Coastal Union

HUYU NDIYE KOCHA MKUU MPYA WA COASTAL UNION, ANAITWA HEMED SULEIMAN 'MOROCCO' NYOTA WA ZAMANI WA KIMATAIFA WA TANZANIA UPANDE WA VISIWANI

TFF YATOA ITC NNE, VODACOM, KLABU ZAMALIZANA  LIGI KUU 



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanne waliokuwa wakichezea timu mbalimbali nchini.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana jijini kuwa, wachezaji hao ni Tony Ndolo aliyejiunga na KCC ya Uganda kutoka Toto Africans, Felix Amech Stanley aliyekwenda Bahla ya Oman kutoka Coastal Union, Ernest Boakye kutoka Yanga aliyejiunga na Tripoli Athletics Club ya Lebanon na Derrick Walulya aliyerejea URA ya Uganda kutoka Simba.
Katika hatua nyingine, Wambura amesema wanamichezo 15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Aliwataja waliochukua fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy, Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Makafu. Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba nafasi ya Katibu Msaidizi.
Alisema waombaji watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na Zena Chande. Nafasi ya Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose Msamila.
Alisema Sophia Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin Badar Soud wao wanaomba nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho kwenye uchaguzi huo ambao utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Ombeni Zavalla.
Wakati huo huo: Klabu za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom zimekutana jana mjini Dar es Salaam.
Wambura amesema mazungumzo yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity) kilichopo kwenye mkataba wa udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa zimeomba kwa mdhamini kuangalia uwezekano wa kukiondoa.
Alisema pande hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya kuitafutia kila klabu mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika ligi hiyo na kwamba klabu zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa African Lyon ambayo ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo.
Kuhusu mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA), Wambura alisema unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea.
Alisema kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka huu.
Alisema fomu hizo zinapatikana ofisi za TAFCA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 alasiri. Ada ya fomu kwa waombaji wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi ni sh. 200,000.
Alisema nafasi zilizobaki za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ada ya fomu ni sh. 100,000. Uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu.

Barnabas asisitiza soka ya vijana

Vincent Barnabas (kulia) katika pambano la Taifa Stars na Msumbiji

WINGA wa timu ya Mtibwa Sugar ya ligi kuu ya Bara, Vincent Barnabas, amesema ili nchi irejeshe makali yake katika soka la kimataifa ni lazima shirikisho la mchezo huo, TFF, na wadau kuwekeza nguvu zao katika maendeleo ya vijana.
Barnabas, alisema mataifa yanayotamba kwenye soka duniani yaliwekeza fedha katika soka la vijana baada ya kuwa na mipango endelevu katika mchezo huo kuanzia ngazi za chini.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum na MJICHARAZO, Barnabas aliyewahi kuwika na timu za Kagera Sugar na Yanga, alisema timu za Tanzania kuanzia za taifa hadi klabu zinafanya vibaya katika michuano ya kimataifa kwa kupuuza soka la vijana.
"Mbali na kupuuza soka la vijana, pia maandalizi duni na kutokuwepo kwa mipango endelevu ya kuinua kandanda katika ngazi zote imekuwa ikiikwaza Tanzania kutamba kimataifa," alisema.
"Lazima tubadilike iwapo tunataka kufika walipo wenzetu."
Alisema nchi imejaliwa vijana wenye vipaji vya soka lakini vinaishia njiani kwa kutoendelezwa, hivyo ni lazima kuwepo na uwekezaji wa kutosha katika soka la vijana ili kuifanya nchi ing'are kama mataifa mengine.
Akizungumzia ligi kuu ya Bara iliyoingia katika mzunguko wa nne sasa alisema, "ni ngumu na haitabiriki.
"Ila kwa aina ya wachezaji tuliopo Mtibwa nadhani msimu huu utakuwa wetu licha ya upinzani toka kwa timu nyingine shiriki."
Mtibwa Sugar iliyomaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya nne, keshokutwa itacheza na Ruvu Shooting ikiwa na kumbukumbu ya kunyukwa bao 1-0 na Azam siku chache baada ya kuisasambua Yanga 3-0 mjini Morogoro.

KARAMA, CHEKA KUONYESHANA KAZI LEO PTA

Bondia  Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Karama Nyilawila  litakalofanyika leo Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.

 Karama Nyilawila akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka litakalofanyika leo Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.


MABONDIA Francis Cheka 'SMG' na Karama Nyilawila 'Captain' leo wanatarajiwa kumaliza ubishi nani mbabe baina yao wakati watakapopanda ulingoni jijini Dar es Salaam kupigana katika pambano linalosaiwa kuwa la kuwania ubingwa wa Mabara wa shirikisho la UBO.
Pambano hilo la uzito wa super middle la raundi 12 lililoandaliwa na kampuni ya Afrika Kabisa chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini, PST, litafanyika kwenye ukumbi wa PTA.
Cheka aliyemshinda kwa pointi Nyilawila katika pambano lao lililopita lililofanyika Februari 28 mwaka huu, ametamba amejiandaa vya kutosha kushinda mchezo huo wa leo ili kulinda heshima yake kwa mashabiki kwa kumpiga mpinzan wake.
Nyilawila amesisitiza rekodi yake ya kutoshindwa mapambano ya ubingwa inamfanya aamini atashinda leo.
"Sijawahi kupigwa kwenye pambano lolote la kuwania ubingwa, hivyo nina imani hata kesho nitaendeleza ubabe kwa kumpiga Cheka na kulipiza kisasi cha kupigwa nae mapema mwaka huu akiwa kwao Morogoro," alisema jana Nyilawila.
Mratibu wa pambano hilo, Robert Ekerege, alisema litasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi na burudani ya bendi ya Mashujaa.
Ekerege aliwataja mabondia watakaopigana katika utangulizi kuwa ni Seba Temba dhidi ya Stan Kessy, Juma Kihiyo atakayepigana na Ibrahim Mahokola, Anthony Mathias atakayechapana na Shaaban Kilumbelumbe na Cosmas Cheka dhidi ya Fadhil Awadh.
Mapambano mengine ya utangulizi ni Husseni Kidebe atakayepigana na Deo Samuel huku Amos Mwamakula akionyeshana kazi na Sadiki Momba.
Michezo yoye hiyo imedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola Kwanza itakayouza soda zake za chupa za plastiki, na Dume Condoms.

AZAM YAIENGUA SIMBA KILELENI, YAILAMBA JKT 3-0


TIMU ya soka ya Azam Fc,  usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine, baada ya kuilaza timu ngumu ya JKT Ruvu 3-0 katika mechi iliyocheza jijini Dar es Salaam.
Azam imeiengua Simba ambayo ndiyo iliyokuwa ikiongoza na leo inatarajiwa nao kushuka dimbani jioni kuumana na Prisons ya Mbeya, baada ya kufikisha jumla ya pointi 10 moja zaidi ya ilizonazo Simba.
Ushindi huo wa pili mfululizo kwa Azam ulipatikana katika mechi kali iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa na na kurushwa 'live' na kituo cha Super Sport kwa mabao yaliyofungwa na nyota wa timu hiyo, John Bocco 'Adebayor' na mapacha toka Ivory Coast, Kipre Tchetche na Kipre Balou.
Kipigo hicho cha jana ni cha tatu mfululizo kwa JKT Ruvu inayonolewa na kocha Charles Kilinda baada ya awali kunyukwa mabao 4-1 na Yanga kabla ya kulazwa mabao 2-1 na Simba katika mechi yao iliyopita.
Katika muendelezo wa Tanzania Soccer Weekend leo jioni mabingwa watetezi Simba watakuwa wakijaribu kurejea kileleni kwa kuikaribisha Prisons ya Mbeya kabla ya kesho watani zao Yanga kuumana na African Lyon na Jumatatu kuwa zamu ya Mtibwa Sugar kupaishwa na Super Sport kwa kuumana na Ruvu Shooting.
Mechi ya mwisho katika mlolongo huo, ni pambano la watani wa jadi Simba na Yanga zinazotarajiwa kuvaana katika mechi yao ya kwanza kwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa siku ya Jumatano.
Mechi hiyo ya watani inayosubiriwa kwa hamu kubwa inatarajiwa kurushwa hewani kuanzia majira ya saa 1;30 usiku siku hiyo ya Oktoba 3.


KOCHA MPYA YANGA AWASILI, KUTAMBULISHWA LEO

 

Brandts wa pili kutoka kulia, akiwa na viongozi wa Yanga. Kulia ni Seif Magari. Kushoto kwake ni Bin Kleb na Majjid


Anapakia mizigo kwenye gari la Bin Kleb

Anazungumza na Waandishi wa Habari

Akiwa na viongozi wa Yanga

Kulia kwake Bin Klerb, kushoto Mwalusako

Anatoka Uwanja wa Ndege



KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, anatarajiwa kutambulishwa leo saa 3:00 asubuhi katika Mkutano maalum na Waandishi wa Habari utakaofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, katika Mkutano huo, pamoja na kuelezwa mkataba ambao klabu imeingia na kocha huyo, lakini pia Waandishi watapata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kocha huyo.
Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, aliwasili jana majira ya saa 3:45 usiku katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na ndege ya KLM na kupokewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako na viongozi wengine, Abdallah Ahmad Bin Kleb, Seif Ahmad ‘Magari’ na Majjid Suleiman.
Yanga, imetimiza malengo yake ya kuwa kocha mpya, kabla ya kucheza na wapinzani wao wa jadi, Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kumfukuza Mbelgiji, Tom Saintfiet, kutokana na kuwasili kwa Brandts, ambaye ataanza kazi mara moja leo.
Kikosi cha Yanga kipo kambini, hoteli ya Uplands, Changanyikeni, Dar es Salaam na kabla ya kucheza na Simba Jumatano, kesho kitacheza na African Lyon, Uwanja wa Taifa pia.
Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi miwili iliyopita na sasa amepata maisha mapya Yanga.
Akiwa APR, Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mbelgiji Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine ya Nusu Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye fainali.
Brandts atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite anayeanza msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima anayeingia katika msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR.
CHANZO:BIN ZUBEIRY