STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 30, 2012

Yanga, Lyon kujiuliza leo Taifa

MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga leo ikiwa chini ya kocha wake mpya, Ernstus Brandts inatarajiwa kuivaa Africna Lyon katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara pambano litakalofanyika kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Yanga ambayo imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja kocha huyo kutoka Uholanzi, itaikaribisha Lyon ikiwa bado inachekelea ushindi mnono wa mabao 4-1 iliyopata dhidi ya JKT Ruvu.
Pambano hilo ambalo litarushwa hewani na kituo cha Super Sport katika ule muendelezo wa Tanzania Weekend Soccer, linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wa Yanga kutoka kupokea kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Prisons ya Mbeya.
Yanga itahitajika ishinde ili kujiweka pazuri kabla ya kuvaana na watani zao keshokutwa kwenye pambano lao la kwanza ambapo wana Jangwani wana deni kubwa la kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0 katika mechi ya kufungia msimu uliopita.
Mbali na deni hilo la karibuni, pia Yanga ina deni la miaka 37 la kipigo cha mabao 6-0 ilichopewa mwaka 1977 ambacho imekuwa ikihangaika kukirudisha bila ya mafanikio.
Bila shaka pambano hilo litakuwa kipimo kizuri kwa makocha wa timu hizo mbili, Brandts wa Yanga na Muargentina anayeinoa Lyon, iliyoshinda mechi moja tu kama wapinzani wao hao wanaovaana wakiwategemea mshambiliaji wake nyota, Adam Kingwande na wengineo.

No comments:

Post a Comment