STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 10, 2015

Straika wa Simba atwaa tuzo Kenya

Michael Olunga
MFUNGAJI Bora wa Kombe la Kagame, na Striaka anayemezewa mate na Simba, Michael Olunga ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) katika sherehe za tuzo hizo zilizofanyika usiku wa jana Jumatano nchini humo.
Simba imekuwa ikimfukuzia Olunga tangu alipofanya vizuri na Gor Mahia katika michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Tanzania Julai mwaka huu na Azam kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Olunga amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 19 na kuisadia Gor Mahia kutwaa ubingwa wa KPL.
Kiungo, Khalid Aucho wa Gor Mahia pia aliyekuwa akiwaniwa na Yanga alishika nafasi ya pili katika tuzo ya Kiungo Bora wa msimu.
Kipa Boniface Oluoch ambaye naye alikuwa akinyemelewa na Simba mwanzoni mwa msimu huu alifanikiwa pia kung'ara katika tuzo hizo kwa kuwatwaa tuzo ya Kipa Bora.
Olunga hata hivyo ametajwa kuwa mbioni kutua klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) ya Mamelodi Sundown ambayo awali ilikuwa ikimvizia Donald Ngoma wa Yanga ila ikampotezea.

No comments:

Post a Comment