STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Samuel Eto'o ajiandaa kutua Everton

http://www.foci-live.hu/files/2014/05/samuel-etoo-chelsea1.jpgBAADA ya Liverpool kumpotezea na kuamua kumsajili Mshambuliaji mtukutu kutoka AC Milan, Mario Balotelli, Mcameroon, Samuel Eto'o anajiandaa kutua kwa mahasimu wa Liverpool, Everton imethibitika.
Eto'o aliye huru baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na Chelsea, inaelezwa yupo hatua ya mwisho kutua kwa kikosi cha kocha Roberto Martinez.
Nyota huyo wa zamani wa klabu za Real Madrid, Barcelona, Inter Milan na Chelsea, alikuwan akitajwa kuelekea Anfield baada ya Jose Mourinho kumchunia Stamford Bridge.
Mshindi huyo wa tuzo ya klabu bingwa Ulaya, Eto’o amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa kiangazi hii lakini taarifa za hivi punde zinaonekana wazi kuwa Everton maarufu kama Toffees wameshindwa mbio za kupata huduma yake.
Eto'o 33 amehifadhi rekodi nzuri ya kufunga zaidi ya magoli 300 na Martinez anataka mtu wa kutumainiwa nyuma ya mshambuliaji wake Romelu Lukaku.
Arouna Kone amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi na bado ataendelea kukosekana ilhali Steven Naismith akiwa ndio mshambuliaji namba mbili.
Eto’o atalazimika kupunguza kiasi cha malipo anayotaka cha pauni £130,000 kwa wiki endapo atakabidhiwa mkataba wa miaka miwili ambao inaonekana ni kama Everton imefanya usajili kwa fedha fedha nyingi msimu huu wa uhamisho.

Mshindi wa Mwanamakuka 2013 kuzikwa kesho Dar

http://3.bp.blogspot.com/-6j_OqFxORhQ/UybGKgAKZUI/AAAAAAAAAGo/_DOs7xSLahs/s1600/Mwanamakuka.jpg
Aziza Mbogolume enzi za uhi wake akiwa na washindi wenzake wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Leila Mwambungu Kushoto na Theo aliyekuwa mshindi wa tatu.
MWILI wa aliyekuwa Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume unatarajiwa kuzikwa kesho majira ya mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopenyezwa na chanzo chetu ni kwamba msiba wa marehemu upo Magomeni Mwembechai na kwamba tayari wanandugu na marafiki wa marehemu wamekusanyana na kupanga kumhifadhi mwenzao kesho mchana maeneo ya Magomeni Kagera.
"Marehemu Aziza Mbogolume anatarajiwa kuzikwa kesho saa 9 mchana Magomeni, na hapa tulipo tunajipanga kwa ajili ya shughuli hiyo ili kumsindikiza mwenzetu," chanzo hicho kilisema.

Tanzania kuandaa AFCON 2017?

Rais wa TFF, Jamal Malinzi anayeipigania Tanzania kuandaa Fainali za Afrika 2017
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetuma maombi kwa Shirikisho la Soka Africa (CAF) kwa ajili ya kuwa wenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2017, kufuatia Libya kujitoa.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa, tayari barua ya ombi hilo imetumwa CAF na Rais Jamal Malinzi.

Malinzi amenukuliwa mapema leo akisema kuwa wana uwezo na wako tayari kuwa wenyeji wa fainali hizo- hivyo wataomba. “Tutaomba kuwa wenyeji wa AFCON ya 2017 kuziba pengo la Libya, tuko tayari na tuna uwezo, tunatarajia sapoti kubwa ya Serikali na wadau wengine wa Tanzania katika hili,”amesema Malinzi. Libya imeamua kujitoa kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo- hivyo kuhofia mazingira ya kiusalama. Awali, Libya ilipewa uenyeji wa fainali za mwaka 2013, lakini ikajitoa kwa sababu kama hizo na Afrika Kusini ikapewa nafasi hiyo- huku makubaliano yakifikiwa wao wataandaa AFCON ya mwaka 2017.
Jumamosi ikatangazwa tena, Libya imejitoa baada ya viongozi wa nchi hiyo kukutana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou.
CAF ikasema jitihada za kumsaka mbadala wa Libya zinaanza mara moja- maana yake kujitokeza kwa Tanzania ni ahueni kwao.
Kwa sasa, Tanzania inaweza kabisa kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa kuwa ina viwanja visivyopugua vitatu vyenye sifa, ingawa vingine vitahitaji marekebisho madogo.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hakuna shaka una sifa zote, wakati CCM Kirumba mjini Mwanza na Sheikh Amri Abeid Arusha vitahitaji marakebisho kidogo.   
Iwapo Tanzania itafanikiwa kupata uenyeji wa fainali za mwaka 2017, itakuwa imefuzu moja kwa moja kucheza michuano hiyo bila kupitia kwenye hatua ya mchujo.
Na hiyo itakuwa mara ya pili kihistoria kushiriki AFCON baada ya 1980 mjini Lagos, Nigeria wakati huo bado michuano hiyo ikiitwa Kombe la Mataifa ya huru ya Afrika.
Tanzania ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji Nigeria, Ivory Coast na Misri na ikashika mkia. Ilifungwa 3-0 na Ngeria, 2-1 na Misri na kutoka sare ya 1-1 na Ivory Coast.  
Yapo matumaini makubwa Tanzania ikafanikiwa kupewa yenyeji wa michuano hiyo mwaka 2017, kutokana na uhusiano mzuri baina ya Hayatou na rais wa sasa wa TFF, Malinzi. Kwa ujumla, FIFA na CAF zina imani kubwa na utawala wa Malinzi.

Rais Kikwete amtunuku Luis Figo Tuzo Ikulu


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya kinyago mchezaji veterani wa timu Real Madrid Luis Figo wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia wachezaji wa timu hiyo na timu ya maveterani ya Taifa Stars ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku baada ya mechi ya kirafiki ambapo Real Madrid illifungaTaifa Stars 3-1 katika uwanja wa Taifa. Picha na Freddy Maro

Boniface Wambura azidi kuula TFF

Mkurugenzi Mpya wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura
AFISA Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameula baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa, Wambura amepandishwa cheo na hivyo ataachana na kiti chake cha sasa cha usemaji wa shirikisho hilo.
Wambura amekuwa kipenzi cha wanahabari kutokana na ushirikiano wake kwa vyomo vya habari na alikuwa katika uongozi uliopita wa rais Leodger Tenga.
Mkurugenzi huyo mpya wa Mashindano wa TFF anatajwa kama Afisa Habari Bora aliyewahi kutokea ndani ya TFF tangu shirikisho hilo lilipobadilisha mfumo wake wa uongozi kwa kuajiri baadhi ya watendaji wake.

Stars kukipiga na Morocco kirafiki tarehe ya FIFA

http://tff.or.tz/wp-content/uploads/2014/05/taifa-stars-2014.jpgTIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars kitasafiri mpaka Morocco kwenda kucheza na wenyeji wake katika mechi ya kirafiki ndani ya tarehe za Fifa.
Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Septemba 5 nchini Morocco. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine amesema wamepokea mwaliko na tayari Kocha Mart Nooij ameishatangaza kikosi chake.
"Ni tarehe ambayo iko ndani ya tarehe za Fifa, hivyo maandalizi yanaanza na kocha ameishaita kikosi," alisema Mwesigwa ambaye pia ni katibu mkuu wa zamani wa Yanga.
Katika mechi yake ya mwisho, Stars ilichapwa kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini nchini Msumbuji na kutolewa katika mbio za kuwania kucheza michuano ya Mataifa Afrika.

Mashetani Wekundu kuweka rekodi mpya England

http://www3.pictures.gi.zimbio.com/Angel+Di+Maria+Hertha+Berlin+v+Benfica+UEFA+At4PKx7NL51l.jpgKLABU ya Manchester United inajiandaa kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza kwa kutaka kumsajili winga mahiri wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Angel Di Maria. 
Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti amebainisha kuwa Di Maria, 26 tayari ameshawaaga wachezaji wenzake kuelekea katika uhamisho wake huo. 
Inakadiriwa kuwa United italazimika kuilipa Madrid kitita cha paundi milioni 75 kama wanahitaji saini ya winga huyo. 
Iwapo United itafanikiwa kutoa kitita hicho watakuwa wamevunja rekodi ya usajili iliyowekwa na Chelsea wakati walipomsajili Fernando Torres kwa paundi milioni 50 kutoka Liverpool mwaka 2011. 
Usajili mkubwa uliowahi kuweka rekodi na kufanywa na United ulikuwa ni wa Rio Ferdinand ambaye alitua Old Trafford kwa paundi milioni 29.1 akitokea Leeds mwaka 2002. 
Muargentina huyo alitua Madrid akitokea Benfica kwa ada ya paundi milioni 36 mwaka 2010 na kufanikiwa kushinda taji la La Liga mwaka 2012 na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
United iliyoanza Ligi Kuu ya England kwa kuchechemea ikivuna pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali inahitaji kuimarisha kikosi ili kuepuka aibua ya msimu uliopita ilipoambulia patupu na kushika nafasi ya saba katika msimamo.

Msiba! Mshindi wa Mwanamakuka 2013 afariki ghafla Dar

http://1.bp.blogspot.com/-pWV9rBQ6zSU/UTsAJzwBYSI/AAAAAAAEMbs/wIoMPtgWHwc/s1600/03.jpg
Aziza Mbogolume (wa pili kulia) enzi za uhai wake wakati akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda tuzo ya Mwanamakuka 2013 kutoka kwa Mke wa Makamu wa Rais, Aisha Bilal.
http://4.bp.blogspot.com/-6hZqPBN8luU/UW3H0k0LiQI/AAAAAAACIkY/j9xLijjnl2k/s640/DSC_3104.JPG
Baadhi ya viongozi waratibu wa shindano la Tuzo za Mwanakuka wakistaajabia kazi za mikono ya Aziza Mbogolume (wa pili toka kushoto) enzi za uhai wao katika maonyesho ya mwaka huu yaliyofanyika Escape 1 Mikocheni
HABARI zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa, aliyekuwa mshindi wa Shindano la Wajasiriamali Tanzania maarufu kama Tuzo za Mwanamakuka zilizoasisiwa mwaka 2012 Aziza Mbogolume amefariki dunia ghafla mchana huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO imepenyezewa na wasomaji wake na kuthibitishwa na Mshindi wa mwaka huu, aliyekuwa wa pili wakati marehemu Aziza akiibuka kidedea, Leila Mwambungu ni kwamba marehemu alikumbwa na mauti mchana wa saa 9 kutokana na tatizo la shinikizo la Moyo.
Inaelezwa kuwa kabla ya kukumbwa na mauti, Aziza aliyenyakua tuzo hiyo na kuzoa kitita cha Sh. Mil 6 toka kwa waandaji wa shindano hilo Marafiki Wanawake wa Tanzania UWF na kudhaminiwa na benki ya Wanawake Tanzania (TWB) kwa kipaji chake cha kuchora picha mbalimbali za mapambo alikuwa akisumbuliwa na tatizo hilo.
"Ni kweli hata mwenzetu amefariki. Nilipigiwa simu na Mwenyekiti wa UWF, Mariam Shamo na kunijulisha na nimempigia mtoto wa marehemu naye amenithibitishia. Kwa kweli inasikitisha kwa sababu ni wiki iliyopita nimetoka kjuwasiliana naye na kuahidi kuja kuniona," alisema Leila kwa sauti na huzuni.
Leila alisema, yeye ametoka kujifungua na hivyo alimjulisha mshiriki mwenzake wa tuzo hizo na shoga wake juu ya kujifungua kwake salama na kumjulisha angeenda kumjulia hali na ghafla leo mchana napigiwa simu juu ya msiba wa Aziza.
Mipango ya mazishi ya marehemu Mwanamakuka huyo wa 2013 zinaendelea na MICHARAZO itawajulisha mara itakapopatra taarifa kamili.
Marehemu Aziza aliyezaliwa miaka zaidi ya 40 mjini Tabora na ameacha mtoto mmoja wa kike aliyekuwa akiishi naye Magomeni Mwembechai na kufanya shughuli zake za uchoraji na uuzaji wa bidhaa za mapambo eneo la Mwenge Vinyago. Mwenyezi Mungu Aiweke Roho ya marehemu Mahali Pepa Peponi. Innalillah Waina Illah Rajiun.
MICHARAZO inatoa pole kwa ndugu, familia na jamaa wa marehemu Aziza Mbogulume na kuwatakiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Kinyambe aamua kuanzisha kampuni Mbeya

http://2.bp.blogspot.com/-nD77bTwFV0U/UtAO8K2MlmI/AAAAAAAAHNg/re3SC9j9Mas/s1600/1521701_579327915475733_414873147_n.jpg
Kinyambe kushoto, alipokuwa Vituko Show akiwa na mpiga picha Yosso Komando
MCHEKESHAJI maarufu nchini James Mohammed 'Kinyambe' ameanzisha kampuni yake ya kutengeneza filamu iitwayo Kinyambe Video Production ambayo ipo njiani kuachia kazi ya kwanza iitwayo 'Fumbafu Thana', huku akimaliza nyingine jijini Mbeya.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka kambini Mbeya, Kinyambe alisema kampuni hiyo ambayo inadili na kutengeneza filamu na video za muziki, itakuwa ikisaidia wasanii chipukizi wa mkoani humo na kwingineko ambao watakuwa wakihitaji kuendeleza vipaji vyao.
Kinyambe aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya kuigiza kama zezeta na kuyabadilisha macho yake kama kinyonga, alisema filamu ya 'Fumbafu Thana' ilitengenezwa mapema, lakini ilikwama kutokana ambapo sasa itaachiwa mapema mwezi ujao.
Alisema wakati filamu hiyo ikiwa njiani kutoka, pia ameshaanza kutengeneza filamu nyingine aliyoigiza na wasanii chipukizi wa jijini Mbeya akiwamo Deus Luis aliyewahi kuuza sura na marehemu Steven Kanumba katika filamu ya 'Poison Leather'.

Juma Luizio 'Ndanda' achekelea maisha mapya Zesco

http://images.uncova.com.s3.amazonaws.com/fad774132f9c41bc2ebfb8ec3a7a75a625cd45e6.jpg
Juma Luizio akiwa kwenye mazoezi ya timu ya Zesco nchini Zambia
MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya ZESCO ya Zambia, Juma Luizio 'Ndanda', amesema hakuna kitu kinachomstaajabisha ugenini kama viwanja vya mazoezi vya timu.
Ndanda anayeichezea pia timu ya taifa aliyetua Zesco akitokea Mtibwa Sugar alisema klabu za Zambia zinajitahidi mno kuwa na viwanja vya mazoezi tofauti na ilivyo nyumbani Tanzania.
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya mtandao mapema leo asubuhi, mchezaji huyo alisema mazingira mazuri aliyokutana nayo Zambia yamemfanya kujisikia faraja.
"Dah mazingira ya huku fresh sana kaka wametuzidi sana kwa sababu kwamba ni waelewa wanaojua nini maana ya mpira, pili wanawalipa vizuri wachezaji pia kuhusu viwanja dah! Aisee kila timu wamejitahidi kuwa na uwanja wa mazoezi na mechi tena vizuri tofauti na huko," alisema.
Luizio aliyemaliza msimu uliopita akiwa mmoja wa wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema kwa kipindi kifupi tangu atue Zesco aliyoingia mkataba wa miaka mitatu ameyazoea mazingira ya soka la nchini hiyo.
"Nashukuru sana nimeshazoea maisha ya huku na naahidi kuitangaza vyema nchi yangu nikiwa na ndoto za kupata nafasi ya kucheza soka Ulaya," alisema.

Meya Kinondoni kuzindua ngumi za 10 Bora J'mosi

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/mwenda-july19-2013.jpg
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuyazindua mashindano ya ngumi za ridhaa za mkoa wa Dar es Salaam yatakayoanza Agosti 30.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA) yanafahamika kama Kumi Bora na yataendeshwa kwa muda wa miezi miwili kabla ya kufikia tamati Novemba 30.
Afisa Habari wa DABA, Mwamvita Jacob aliiambia MICHARAZO kuwa michuano hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Manyara uliopo Tandele CCM na siku ya ufunguzi Meya wa Mwenda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.
Mwamvita alisema michuano hiyo itashirikisha klabu zote za ngumi za ridhaa za mkoa wa Dar es salaam.
"DABA inatarajia kuendesha mashindano ya ngumi ya Kumi Bora ambayo yatazinduliwa rasmi siku ya Jumamosi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda majira ya saa 10 na yatafikia tamati Novemba 30," alisema. Mwamvita alisema michuano hiyo itatumika pia kusaidia mikoa ya kimichezo ya Ilala, Temeke na Kinondoni kupata timu za kuziwakilisha kwenye mashindano ya taifa ya ngumi itakayofanyika Oktoba mwaka huu.

Mashindano ya Taifa ya Ngumi kufanyika Dar es Salaam

http://4.bp.blogspot.com/-CndqAvf3z6I/T0FlU2UxvEI/AAAAAAAAI5A/xXrOFiC5cTs/s1600/MAKORE+MASHAGA.JPG
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga

http://2.bp.blogspot.com/-cwPwCevqWqo/UvbZWBmCQjI/AAAAAAAANIo/xcqifOpgfos/s1600/IMG_1118.JPG
Mabondia kama hawa wataonyeshana kazi jijini Dar
MASHINDANO ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa yanatarajiwa kufanyika kuanzia  Oktoba 8-14 jijini Dar es Salaam.
Michuano hiyo itatumiwa kwa ajili ya kusaka wachezaji wa kuunda timu ya taifa kwa michezo mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania itashiriki.
Baadhi ya mashindano ambayo Tanzania inatarajiwa kushiriki ni pamoja na Michezo ya Kanda ya tatu ya Afrika, Michezo ya Afrika na Ubingwa wa Dunia itakayochezwa mwakani na ile ya Olimpiki ya mwaka 2016.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema kuwa michuano hiyo itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na vyombo vya Ulinzi na Usalama itafikia kilele siku ya Nyerere Day.
Siku hiyo huwa ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwl Julius Nyerere aliyefarikia Oktoba 14, 1999.
Mashaga alisema mashindano hayo yatahusisha mabondia vijana (youth), wakubwa (senior) na wanawake (women) kwa ratiba itatolewa siku chache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Alisema timu shiriki zinatakiwa ziwe zimeshatuma majina ya vikosi vyao kabla ya Septemba 29 na timu zote zinatakiwa ziwe zimeshawasili jijini Dar es Salaam kabla ya Oktoba 7.
Mashaga alisema uzinduzi wa michuano hiyo itfanyika Oktoba 10 na mgeni rasmi watakayemtangaza baadaye.

As Vita, TP Mazembe hakuna mbabe Esperance yaua

http://voiceofcongo.net/wp-content/uploads/2014/05/as-vita-tp.jpg
WAKATI Esperance ya Tunisia ikimaliza mechi zake za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa heshima kwa kuilaza Al Ahly Benghaz ya Libya kwa bao 1-0, wapinzani wa soka wa DR Congo AS Vita na TP Mazembe zenyewe zimeshindwa kutambiana baada ya kutopka suluhu mjini Kinshasa.
Pambano la Mazembe na Vita lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kutokana na upinzani wa timu hizo mbili za Kongo ambazo zote zimeshafuzu hatua ya Nusu Fainali kutoka kundi A lilishuhudia dakika 90 zikiisha milango ikiwa migumu.
Katika mechi hiyo watanzania wanaoichezea TP Mazembe Mbwana Samatta na Ulimwengu Thomas aliyeingizwa kipindi cha pili wakijitahidi kuipigania timu hiyo wakishirikiana na wenzao lakini bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo Mazembe wamemaliza kileleni kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa licha ya kuwa na pointi 11 sawa na wapinzani wao hao.
Katika mechi nyingine ya kundi B Esperance ya Tunisia ilikamilisha ratiba yake kwa kuilaza ndugu zao wa Libya Al Ahly Benghaz na kuishia kukamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7.
Katika mechi nyingine za kukamilisha ratiba kwa Kombe la Shirikisho, Sewe Sport ya Ivory Coast iliinyuka Nkana Red Devils kwa mabao 3-0, huku Al Ahly ya Misri ilibanwa nyumbani na Etoile du Sahel na kutoka suluhu licha ya kwamba imeshafuzu Nusu Fainali ikiungana na Sewe.
Mechi nyingine AC Leopards ya Congo iliifumua ASEC Memosa kwa mabao 4-1 na Real Bamako ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Coton Sport ambayo iliungana na Leopards kufusu hatua ya nusu fainali kutoka kundi B.

Mcameroon afa uwanjani kwa kupigwa na kitu kichwani

http://www.maracanafoot.com/wp-content/uploads/2013/09/Ebosse1.jpgMCHEZAJI kutoka nchini Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kurushiwa kitu na mashabiki katika mchezo wa ligi nchini Algeria.
Ebosse, 24, alithibitishwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hospitali katika eneo la Tizi Ouzou, mashariki mwa mji mkuu, Algiers.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya JS Kabylie, ambaye alikuwa amefunga goli moja katika mchezo huo waliopoteza kwa 2-1, dhidi ya USM Alger aligongwa na kitu hicho baada ya mpira kumalizika, wakati wachezaji wakiwa wanatoka uwanjani.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi imetaka uchunguzi kufanyika mara moja.
Haijathibitishwa ni kitu gani hasa alichogongwa nacho, lakini gazeti moja la Algeria limesema mashabiki walikuwa wamekasirishwa na kufungwa na walikuwa wakirusha mawe.
Taarifa iliyotolewa na klabu yake imesema :”alikufa kutokana na jeraha la kichwani” baada ya kurushiwa kitu mwisho wa mchezo.
Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, Issa Hayatou ametoa taarifa inayolaani tukio hilo.

Waziri Mwigulu Nchemba asitisha safari kuokoa majeruhi wa ajali


Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo. 

Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.


Na.Festo Sanga.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Lori Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
 
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Lori hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
 
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,
 
Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
 
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongeza sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.

Chriss Brown anusurika kufa kwa risasi Marekani

Chris Brown aliyenusurika kuchapwa risasi
http://www.vibe.com/sites/vibe.com/files/styles/article-bounds-718/public/photo_gallery_images/suge-knight-crazy-quotes.jpg
Suge Knight aliyejeruhiwa kwa risasi mbili
MUIMBAJI nyota wa Marekani Chris Brown amenusurika kuuawa katika shambulio la risasi ndani ya klabu ya usiku jijini Los Angeles ambapo prodyuza Suge Knight amejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika klabu ya usiku iitwayo 1OAK iliyopo magharibi mwa Hollywood wakati wa shoo iliyokuwa ikiongozwa na Cris Brown kabla ya zoezi la utoaji Tuzo za VMA ambapo watu watatu wamejeruhiwa mmoja akiwa mahututi.
Suge Knight alipigwa risasi mara mbili tumboni na mkononi na kukimbizwa hospitali ambapo anaendelea na matibabu.
Mastaa wengine waliokuwepo kwenye klabu hiyo wakati tukio hilo likitokea ni pamoja na Justin Bieber, rappa The Game, Pia Mia, Tyson Beckford, Robert Ri'chard  na wengineo.
Indaiwa mlengwa mkuu katika shambulio hilo alikuwa Chris Brown, lakini Mungu akamuepushia msala huo unaokumbusha matukio ya nyota wa hiphop 2 Pac Shakur na BIG Notorious waliouwawa katika mikasa tofauti ya ulipizaji kisasi baina ya kambi za East Coast and West Coast