STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Mashindano ya Taifa ya Ngumi kufanyika Dar es Salaam

http://4.bp.blogspot.com/-CndqAvf3z6I/T0FlU2UxvEI/AAAAAAAAI5A/xXrOFiC5cTs/s1600/MAKORE+MASHAGA.JPG
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga

http://2.bp.blogspot.com/-cwPwCevqWqo/UvbZWBmCQjI/AAAAAAAANIo/xcqifOpgfos/s1600/IMG_1118.JPG
Mabondia kama hawa wataonyeshana kazi jijini Dar
MASHINDANO ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa yanatarajiwa kufanyika kuanzia  Oktoba 8-14 jijini Dar es Salaam.
Michuano hiyo itatumiwa kwa ajili ya kusaka wachezaji wa kuunda timu ya taifa kwa michezo mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania itashiriki.
Baadhi ya mashindano ambayo Tanzania inatarajiwa kushiriki ni pamoja na Michezo ya Kanda ya tatu ya Afrika, Michezo ya Afrika na Ubingwa wa Dunia itakayochezwa mwakani na ile ya Olimpiki ya mwaka 2016.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema kuwa michuano hiyo itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na vyombo vya Ulinzi na Usalama itafikia kilele siku ya Nyerere Day.
Siku hiyo huwa ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwl Julius Nyerere aliyefarikia Oktoba 14, 1999.
Mashaga alisema mashindano hayo yatahusisha mabondia vijana (youth), wakubwa (senior) na wanawake (women) kwa ratiba itatolewa siku chache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.
Alisema timu shiriki zinatakiwa ziwe zimeshatuma majina ya vikosi vyao kabla ya Septemba 29 na timu zote zinatakiwa ziwe zimeshawasili jijini Dar es Salaam kabla ya Oktoba 7.
Mashaga alisema uzinduzi wa michuano hiyo itfanyika Oktoba 10 na mgeni rasmi watakayemtangaza baadaye.

No comments:

Post a Comment