STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Mashetani Wekundu kuweka rekodi mpya England

http://www3.pictures.gi.zimbio.com/Angel+Di+Maria+Hertha+Berlin+v+Benfica+UEFA+At4PKx7NL51l.jpgKLABU ya Manchester United inajiandaa kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza kwa kutaka kumsajili winga mahiri wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Angel Di Maria. 
Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti amebainisha kuwa Di Maria, 26 tayari ameshawaaga wachezaji wenzake kuelekea katika uhamisho wake huo. 
Inakadiriwa kuwa United italazimika kuilipa Madrid kitita cha paundi milioni 75 kama wanahitaji saini ya winga huyo. 
Iwapo United itafanikiwa kutoa kitita hicho watakuwa wamevunja rekodi ya usajili iliyowekwa na Chelsea wakati walipomsajili Fernando Torres kwa paundi milioni 50 kutoka Liverpool mwaka 2011. 
Usajili mkubwa uliowahi kuweka rekodi na kufanywa na United ulikuwa ni wa Rio Ferdinand ambaye alitua Old Trafford kwa paundi milioni 29.1 akitokea Leeds mwaka 2002. 
Muargentina huyo alitua Madrid akitokea Benfica kwa ada ya paundi milioni 36 mwaka 2010 na kufanikiwa kushinda taji la La Liga mwaka 2012 na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
United iliyoanza Ligi Kuu ya England kwa kuchechemea ikivuna pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali inahitaji kuimarisha kikosi ili kuepuka aibua ya msimu uliopita ilipoambulia patupu na kushika nafasi ya saba katika msimamo.

No comments:

Post a Comment