STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 29, 2014

Hatimaye Tevez arejeshwa kikosi cha Argentina

http://e0.365dm.com/14/01/768x432/Carlos-Tevez_3060385.jpg?20140102104022
Carlos Tevez
MSHAMBULIAJI nyota wa Juventus, Carlos Tevez ameitwa kwenye timu ya taifa ya Argentina kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu baada ya kuchaguliwa katika kikosi kitakachocheza mechi zijazo za kirafiki.
Nyota huyo wa zamani wa West Ham United, Manchester United na Manchester ity amekuwa nje ya kikosi hicho cha taifa tangu 2011 alipocheza mechi ya kichapo cha robo fainali ya michuano ya Copa America dhidi ya Uruguay.
Hata hivyo, kocha mpya Gerardo Martino, ambaye alichukua mikoba kutoka kwa Alejandro Sabella kufuatia kipigo cha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Ujerumani, alisema mapema mwezi huu kuwa milango iko wazi kwa Tevez kurejea kikosini kama atathibitisha ubora wake katika ngazi ya klabu.
Na sasa kocha huyo wa zamani wa Barcelona amemuita kikosini nyota huyo (30) kwa ajili ya mechi za kuwakabili Ureno na Croatia, kufuatia kufunga magoli nane katika mechi 10 akiwa na Juventus msimu huu.
Miongoni mwa wakali walioitwa yupo nahodha Lione Messi, mshambuliaji Sergio Aguero, Angel di Maria, Javier Mascherano,  Marcos Rojo, Pablo Zabaleta, Martin Demichelis, huku pia Erik Lamela wa Tottenham naye akiitwa siku chache tu tangu alipofunga goli "la miujiza" la mkasi wa kupiga mpira kwa kupitisha mguu wa kushoto nyuma ya mguu wa kulia.

Polisi wwatambua waliomuua kipa wa Afrika wa Kusini

http://www.itnewsafrica.com/wp-content/uploads/2014/10/Senzo.jpgPOLISI nchini Africa Kusini wameonesha nyuso zinazo dhaniwa kuwa ni wauaji wa golikipa na kapteni wa timu ya taifa Africa Kusini Bafana Bafana, Senzo Meyiwa.
Meyiwa alipigwa risasi na kufa siku ya jumapili wakati alipokuwa akikabiliana na wavamizi waloingia nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo ambaye ni mwanamuziki na pia ni muigizaji,maziko ya Meyiwa yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Kifo cha mwanasoka huyo kimeonesha picha halisi ya kiwango cha uhalifu na matumizi mabaya ya silaha nchini Africa Kusini.
Africa kusini inatajwa kuwa moja ya nchi zenye matukio makubwa ya uhali,na kiwango cha uhalifu kinazidi kuongezeka siku hadi siku.
Mwanzoni mwa mwezi huu mwanariadha Oscar Pistorious alihukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake.
BBC