STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, October 30, 2014

LIGI DARAJA LA PILI KUANZA NOV 22.

MICHUANO ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini Dar es Salaam jana (Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange ilipitia maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake (roadmap).
Kwa mujibu wa mwongozo huo, usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu. Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kupitisha usajili.
Pia Kamati ya Mashindano imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu ya Mpanda United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Uwanja wa Town Small Boys haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa kutenganisha wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu kutokana na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi kipindi cha Masika.
Kwa upande wa uwanja wa Mpanda United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi vinavyotakiwa ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio wa kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.
Kutokana na uamuzi huo, Mpanda United sasa itatumia Uwanja wa Mandela uliopo Sumbawanga wakati Town Small Boys itachezea mechi zake kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

29 waitwa Stars Maboresho II

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/Staz.jpg
Baadhi ya wachezaji wa Maboresho awamu ya kwanza katika kikosi cha Stars kilichopigwa 3-0 na Burundi
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.
Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.
Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.
Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.
TFF ina imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.
Wachezaji walioteuliwa ni Aishi Manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).
Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Abdi Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).
Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).

TFF yatoa dili kwa wabunifu jezi za Stars



http://tff.or.tz/wp-content/uploads/2014/05/Boniface-Wambura.jpg
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. 
Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa. Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja). Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.

MSIBA! MZEE MANENTO WA BONGO MOVIE AFARIKI!


TASNIA ya sanaa imeendelea kukumbwa na majonzi baada ya msanii mwingine wa Bongo Movie, David Manento 'Mzee Manento' kufariki.
Mzee Manento aliyekuwa swahiba mkubwa wa marehEMU Steven Kanumba alifariki usiku wa jana baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari pamoja na Presha akiwa na miaka 73.
Rais wa Shirikisho la Wasanii Tanzania, TAFF, Simon Mwakifwamba amethibitisha kufariki kwa Mzee Manento na kusema kuwa msiba wake upo nyumbani kwake Kigogo/Mburahati jijini Dar es Salaam
Mzee Manento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakini na marehemu Kanumba. 
Baadhi ya filamu zilizomjengea jina kubwa ni pamoja na Fake Pastor, Dar to Lagos na Hero of the Church.
Marehemu Manento anayetokea mkoa wa Kilimanjaro ameacha watoto 9 na inaelezwa tangu alipofiwa na mkewe miaka michache iliyopita alikuwa mpweke kiasi cha kushindwa hata kula vizuri.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Amina.

Robo Fainali ya Capital One hii hapa

VINARA wa Ligi Kuu ya England, Chelsea imepangiwa kukutana na Derby County katika Robo Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One League) huku vijogoo vya London, Tottenham Hotspur wakipangiwa wabaya wao Newcastle United.
Newcastle waliifumua Spurs mabao 2-1 nyumbani mwishoni mwa wiki katika Ligi kabla ya usiku wa jana kuitemesha taji Manchester City kwa kuilaza mabao 2-0 katika Capital One.
Kwa mujibu wa ratiba ya hatua huyo,  Liverpool impangwa kucheza na FC Bournemouth na robo fainali ya mwisho itazikutanisha timu za Sheffield United.
Mechi hizo zitachezwa Desemba 16 na ratiba kamili iko hivi;
Tottenham vs Newcastle
Derby vs Chelsea
Bournemouth vs Liverpool
Sheffield vs Southampton