STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 2, 2015

El Merreikh yamfukuzisha kazi kocha wa Azam

http://jamboleo.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/OMOG.jpg
MABINGWA wa soka nchini, Azam imemtimua kocha wake, Joseph Omog na msaidizi wake Ibrahim Shikanda na baadhi ya watendaji baada ya klabu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor 'Father' ameweka bayana maamuzi hayo akisema imetokana na makubaliano waliyowekeana na Mcameroon huyo wakati wakiingia naye mkataba.
Father alisema kuwa, wakati wanaingia mkataba na Omog walikubaliana kuivusha mahali ilipo Azam ikiwamo kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa, lakini kwa miaka miwili kocha huyo ameshindwa.
"Kwa hali hiyo tumeamua kuachana kwa wema na yeye mwenyewe analifahamu hilo, na hajatoka pekee yake bali na msaidizi namba mbili Ibrahim Shikanda na baadhi ya watendaji wa benchi la ufundi,"alisema.
Aliongeza kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha msaidizi  kutoka Uganda, George Nsimbe ambaye atakaimua nafasi hiyo mpaka watakapopata kocha mkuu katika mchakato utakaoendeshwa na klabu yao.

GUINEA YAZIGOMEA CAF, FIFA AFCON 2023

https://athlet.org/jdd/public/documents/athlet/football/competitions/200x300/can2023.png

http://www.ghanasoccernet.com/wp-content/uploads/2015/03/AFCONtrophy.jpeg 
WENYEJI wa Fainali za Afrika za 2023, Guinea imeweka bayana kwamba hatakubali kuhamisha michuano hiyo toka mwanzoni mwa mwaka na kufanyika katikati ya mwaka  kama FUIFA inavyotaka.
Wenyeji hao wamesema kuwahawakubaliani na fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2023 kuchezwa mwezi Juni ili kuziwezesha fainali za Kombe la Dunia kufanyika Qatar, alisema waziri wao wa michezo.
Domani Dore alipingana na taarifa ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) Jerome Valcke, ambaye wiki iliyopita alisema kuwa, fainali za Mataifa ya Afrika 2023 zinatakuwa kusogezwa mbele kwa miezi sita hadi Juni kutoka katika muda wake wa kawaida wa mwezi Januari.
Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zimepangwa kufanyika Novemba na Desemba, kufuatia mapendekezo ya kamati ya maandalizi.
Valcke alisema kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwezi mmoja baadae ni jambo lisilowezekana, na aliongeza kuwa anakubaliana na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuhamisha fainali hizo zinazoshirikisha jumla ya timu 16 baadae mwaka huo.
Hatahivyo, Guinea, imesema kuwa itapinga tarehe hizo mpya.
"hatuwezi kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika mwezi Juni, ni kipindi cha mvua, “’alisema Dore alipozungunza na televisheni ya Guinea.
"Caf walitakiwa kusikiliza ushauri wa Guinea kuwa kama sisi ni taifa tunatakiwa kuamua tarehe gani zifanyike. Tunaelewa matatizo yanayolizunguka Kombe la dunia na kugongana na fainali za Mataifa ya Afrika.
"Lakini Caf walitakiwa kusikilisha maoni yetu. Mwezi juni , haiwezekani, " aliongeza Dore.
Shirikisho hilo la Soka la Afrika limesisitiza kuhusu fainali Mataifa ya Afrika 2023 nchini Guinea, likisema kuwa "Uamuzi kuhusu Afcon 2023 utatolewa na Kamati ya Utendaji ya CAF, na sio mtu mwingine, wakati utakapofika."

MALI YAWEKA REKODI AFRIKA YATWAA UBINGWA U17

http://www.foot224.net/wp-content/uploads/2015/03/mali.jpghttp://www.fiba.com/images.fiba.com/Graphic/e7176210/86bb/4e9b/af1c/5e20b580e6d4.jpg?v=20140930135344693MALI imetawazwa kuwa mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuifunga Afrika Kusini kwa bao 2-0 katika fainali iliyofanyika jijini hapa.
Mabao ya kipindi cha pili yaliyowekwa kimiania na Siaka Bagayoko na Aly Malle yaliiwezesha Mali kutwaa taji hilo.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Mali timu yake ya vijana inayojulikana kama Eaglets kushinda taji la mashindano ya vijana.
Awali, nchi hiyo ilikaribia kushinda taji mwaka 1997, wakati ilipomaliza ya pili nyuma ya washindi Botswana.
Timu zote Mali na Afrika Kusini zilienda katika fainali hiyo ya Jumapili zikiwa tayari zimewahi kukutana katika hatua ya makundi ya mashindano hayo, wakati Afrika Kusini ikiwa nyuma kwa bao 2-0 na kulazimisha sare ya 2-2.
Hatahivyo, Mali haikuruhusu hilo utokea tena, na kuhakikisha inaweka ulinzi mkali baada ya kupata bao la kuongoza na kuhakikisha inaibuka na ushindi.
Bao lao la kwanza lilipatikana baada ya dakika 67 wakati Bagayoko alipofunga kwa kichwa mpira wa kona.
The Eaglets waliongeza bao la pili zikiwa zimebaki dakika 12 kufuatia juhudi binafsi ya Aly Malle. 
Bao hilo alilifunga kutoka umbali wa kama mita 20 kutoka nje ya boksi na kuibua furaha kwa mashabiki wao.
Afrika Kusini walifikiri wangeweza kupata bao la kufutia machozi wakati Khanyisa Eric Mayo alipokaribia kufunga, lakini alijikuta akiwa ameotea.

Jose Mourinho ataka mataji zaidi Stanford Bridge


Mourinhio akilia kwa furaha
Mourinho akikia kwa furaha baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa taji la kwanza msimu huu la Capital One
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amedhamiria kutafuta mataji zaidi baada ya kunyakuwa taji la Kombe la Ligi  (Capital One) jana ikiwa ni la kwanza kwa kocha huyo toka achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo kwa mara ya pili.
Mabao yaliyofungwa na John Terry na lingine la kujifunga la Kyle Walker yalitosha kuipa ushindi wa mabao 2-0 Chelsea dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Wembley. Taji hilo linakuwa la 21 kwa Mourinho toka aanze kufundisha soka.
Akihojiwa Mourinho amesema anajiona kama mtoto aliyeshinda kwa mara ya kwanza kwani mara zote imekuwa ngumu kwake kuishi bila mataji.
Mourinho ambaye kwa mara ya kwanza amewahi kuinoa Chelsea mwaka 2004 hadi 2007 kabla ya kurejea tena mwaka 2013, hilo linakuwa taji lake la saba akiwa timu hiyo na pia kuisaidia Chelsea kulipa kisasi kwa Spurs ambao waliwatungua mabao 2-1 katika fainali za michuano hiyo zilifanyika mwaka 2008.
Kwa furaha kocha huyo alijikuta akimwaga chozi kabla ya baadaye kujumuika na wachezaji wake kushangilia mafanikio hayo yaliyokuja wakati Chelsea ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England na pia ikiwa kwenye hatuia nzuri ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

TAIFA STARS KUPASHA MISULI MOTO COSAFA CUP

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha runinga cha Supersport 4.

Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi  nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.
 
Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za  Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.

Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros, Lesotho, Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji, Namibia, Reunion, Sychelles, Swaziland, Zambia na Zimbabwe
.

BASATA LAMLILIA CAPT JOHN KOMBA

Mwili wa Kapteni Komba ukiwasilia Karimjee mapema leo kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Lutuhi, Nyasa, wilayani Mbinga.
Kapteni John Komba enzi za uhai wake katika picha tofauti akiwajibika katika sanaa yake ya uimbaji wa kwaya
Na Rahim Junior
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limetuma salamu za rambirambi kumlilia Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba aliyefarikia wikiendi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa yake BASATA imekielezea kifo cha Komba kama pigo kubwa katika tasnia ya sanaa.
Taarifa ya BASATA inasomeka hivi;
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Captain John Damian Komba kilichotokea jioni ya Jumamosi ya tarehe 28/02/2015.
Captain John Damian Komba ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.
Mchango wake katika muziki wa dansi, kwaya na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza wasanii mbalimbali nchini hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha alama kuu katika muziki wa bendi, kwaya na taarabu na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa dansi na kwaya mahali ulipo leo.
Aidha, pamoja na kujiunga na siasa na hatimaye kuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Mheshimiwa Komba hakukoma kuendelea kuipigania sekta ya Sanaa kwani alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambayo kwa mujibu wa kanuni za Bunge ndiyo inayoisimamia na kuishauri Serikali katika masuala yote yahusuyo sekta ya Sanaa na Utamaduni.
Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu John Komba hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania.
Hakika pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.
Baraza linatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda, wabunge na wadau wote wa Sanaa hususan wasanii kwa msiba huu. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu, hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.
Bwana ametoa na  Bwana ametwaa, Amen
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

HII NDIYO NGOMA MPYA YA ALI KIBA-CHEKECHA CHEKETUA

http://api.ning.com/files/3A8rUyA9jKO74o0hv92PLkY4cX5Pc5NkU5Zpw0YYfLFhqQS2Bf6-S-SDS87ET40281CaSxj2VQO9q9KxkyAfyCDor8nBaOVv/IMG_0128.jpg
Baada ya Mwana, Ali Kiba amekuja kivingine na Chekecha Cheketua ebu isikilize hapo chini;

KICHUPA KIPYA CHA ZOLA D FT LATINHO.- I DON'T CARE.

http://3.bp.blogspot.com/-XpkM1hU5p-w/UQiyEQPyyzI/AAAAAAAAEUM/IbEOVC5n9U4/s1600/Zola+D2.JPG
Zola D King aliyeachia video ya wimbo wake wa I Don't Care