STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 1, 2016

Jerome Boateng afarijika na kumshukuru Kansela Merkel

https://blog-blogmediainc.netdna-ssl.com/upload/SportsBlogcom/4259301/0335206001446232183_filepicker.jpg
Jerome Boateng
http://i0.web.de/image/406/31373406,pd=3/alexander-gauland-afd.jpg
Alexander Gauland aliyetoa kauli za kibaguzi dhidi ya Jerome Boateng
KIROHO safi. Beki wa kimataifa wa Ujerumani, Jerome Boateng amedai kuwa ubaguzi nchini humo bado upo kwa kiasi kikubwa, ila ameshukuru namna Kansela Angela Merkel kwa jinsi alivyoiponda vikali kauli iliyotolewa na mwanasiasa anayeheshimika nchini humo, Alexander Gauland.
Gauland alikaririwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa asingependa kuwa rafiki au hata jirani na nyota huyo wa Bayern Munich ambaye ana asili Ghana.
Kauli hiyo ilizua mjadala mkubwa huku ikipondwa vikali na watu mbalimbali akiwemo Afisa Mkuu wa Ligi ya Soka ya Ujerumani-DFL aliyedai kuwa kauli hiyo mbaya na isiyovumilika.
Msemaji wa Kansela Merkel amesema 'bosi' wake amesikitishwa sana na kauli hiyo ikizingatiwa kuwa imetoka kwa mwanasiasa huyo anayeheshimika.
Boateng akihojiwa kuhusiana na suala hilo alisema amefarijika mno kuona watu mbalimbali wanavyopingana na kauli hiyo akiwemo kansela Merkel na kuongeza kuwa vita vya kupambana na ubaguzi wa rangi bao haijaisha.

Rashford naye ndani katika kikosi cha mwisho cha England

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/02717/04_01125924_ff23d4_2717346a.jpgLAZIMA iwashike. England imetangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya Fainali za UEFA Euro 2016, huku chipukizi wa Manchester Utd, Marcus Rashford akijumuishwa katika kikosi hicho.
Rashford mwenye umri wa miaka 18, alifunga bao katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa wakati Uingereza waliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Australia katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Ijumaa iliyopita. Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge naye pia amejumuishwa, lakini Andros Townsend wa Newcastle Utd na Danny Drinkwater wa Leicester City wote wameachwa katika kikosi hicho cha mwisho chini ya Kocha Roy Hodgson. 
England inatarajiwa kuchuana na Ureno katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ikishuka dimbani siku moja baada ya uzinduzi wa michuano hiyo inayaofanyika Ufaransa.
England itaanza kibarua chake Juni 11 kwa kuvaana na Urusi. 
Kikosi kamili cha Three Lions ni kama ifuatavyo;
Makipa: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley). 
Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool). 
Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal). Washambuliaji: Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester United).

Maskini Marco Reus aachwa tena Ujerumani

http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/002/728/809/hi-res-450616209-marco-reus-of-germany-in-action-during-the_crop_exact.jpg?w=1500&h=1500&q=85SIJUI ni mikosi au basi tu. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amemuacha mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
Kocha Low alitangaza kikosi chake huku mbali na kumuacha Reus lakini pia amewaacha Karim Bellarabi na Julian Brandt wa Bayer Leverkusen na Sebastian Rudy wa Hoffenheim.
Nyota hao wanne sasa wanatarajiwa kuondoka katika kambi ya timu hiyo huko Uswisi.
Ujerumani itacheza mechi yake ya mwisho ya kujipima nguvu dhidi ya Hungary kabla ya kucheza mechi yao ya ufunguzi wa michuano ya Euro 2016 dhidi ya Ukraine. Reus alishindwa kusalia kwenye kikosi cha Mabingwa hao wa Dunia katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka juzi nchini Brazili, badala ya kuumia, lakini safari hii yupo fiti, lakini kafungiwa vioo.
Kikosi kamili:

Makipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona).

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Emre Can (Liverpool), Jonas Hector (Cologne), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Shkodran Mustafi (Valencia), Antonio Rudiger (Roma).
Viungo: Julian Draxler (Wolfsburg), Mario Gotze (Bayern Munich), Sami Khedira (Juventus), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Schalke), Bastian Schweinsteiger (Manchester United), Julian Weigl (Borussia Dortmund).

Mastraika: Mario Gomez (Besiktas), Thomas Muller (Bayern Munich), Lukas Podolski (Galatasaray), Andre Schurrle (Wolfsburg).

Ayaa kakatwa! Sendros aachwa Uswisi

https://metrouk2.files.wordpress.com/2013/04/162435959-e1365621949755.jpgKAKATWA. Beki wa zamani wa Arsenal, Philippe Senderos ambaye amekuwa akihaha kurejea katika kiwango chake katika misimu ya karibuni, ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uswisi kwa ajili ya michuano ya Euro 2016. 
Senderos ambaye ametumia muda mwingi msimu uliopita akiwa na timu yake ya nyumbani ya Grasshopper Zurich, alishindwa kuonyesha uwezo makeke ili kumshawishi kocha wake wakati Uswisi ilipotandikwa mabao 2-1 na Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu. 
Kocha Vladimir Petkovic ameamua kumuacha beki huyo mwenye umri wa miaka 31 licha ya hofu iliyopo kwenye ukuta wa timu hiyo baada ya Timm Klose na Johan Djourou kuwa nje kwa majeraha.
Beki wa Udenese Silvan Widmer na kiungo wa Basel Luca Zuffi aliyeonyesha uwezo mkubwa msimu huu pia wamekatwa katika kikosi hicho. 
Uswisi inatarajiwa kucheza na Moldova katika mechi yake ya mwisho ya kujipima nguvu keshokutwa Ijumaa kabla ya kuvaana na Albania, Romania na wenyeji Ufaransa katika kundi A. 
Kikosi Kamili 
Makipa: Yann Sommer (Borussia Monchengladbach), Roman Burki (Borussia Dortmund), Marwin Hitz (Augsburg) 

Mabeki: Stephan Lichtsteiner (Juventus), Nico Elvedi (Borussia Monchengladbach), Michael Lang (Basel), Johan Djourou (Hamburg), Steve von Bergen (Young Boys), Fabian Schar (Hoffenheim), Francois Moubandje (Toulouse), Ricardo Rodriguez (Wolfsburg)  
Viungo: Valon Behrami (Watford), Blerim Dzemaili (Genoa), Gelson Fernandes (Rennes), Fabian Frei (Mainz), Granit Xhaka (Arsenal), Xherdan Shaqiri (Stoke City), Renato Steffen (Basel), Denis Zakaria (Young Boys) 
Washambuliaji: Breel Embolo (Basel), Haris Seferovic (Eintracht Frankfurt), Admir Mehmedi (Bayer Leverkusen), Eren Derdiyok (Kasimpasa), Shani Tarashaj (Everton)

Yanga yaipoka TFF uchaguzi mkuu wao kufanyika Juni 11

http://2.bp.blogspot.com/-2jspLbxdTC4/VqjXv-Gxl_I/AAAAAAAACAg/oYANqZloaFI/s1600/yanga.JPGWAKATI Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Yanga ikiongeza muda wa uchukuaji na urudishwaji fomu za uchaguzi huo, uongozi wa mabingwa hao wa soka umeamua kuonyesha ubabe.
Uongozi huo umetangaza kutoutambua uchaguzi huo wa Juni 25 na badala yake kuutangaza wao ambao utafanyika Juni 11 na zoezi la uchukuaji fomu za uchaguzi huo utakaoshirikisha wanachama wote wakiwamo wa zamani na wale wenye kadi za Benki ya Posta.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit, alitangaza maamuzi hayo leo kwa madai kuwa, TFF haiwezi kuusimamia uchaguzi wao kwa vile hawawajui wanachama halali wa klabu hiyo.
Baraka alisema kuwa, wanaweza kuwekewa mamluki na kuivuruga Yanga ambayo kwa siku za karibuni imekuwa na mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi kiasi cha kutinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni rekodi kwa klabu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Tanzania kwa ujumla.
Uongozi huo umesema zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litaanza kesho Juni 2-3 kabla ya kufanyiwa usaili na baadaye kuendelea na taratibu nyingine ikiwamo pingamizi na kisha kuwasilisha majina ya wagombea watakaopitishwa kabla ya kampeni kuanza Juni 8-10 na uchaguzi kufanyika Juni 11 kisha matokeo yake kutangazwa Juni 12.
Hata hivyo hayo yanaendana kinyume na Kamati ya Uchaguzi wa TFF inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.

Mpaka jana wanachama tisa (9) walikuwa wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.

Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.

Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz


Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa 

nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 

100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa 

kamati ya utendaji.  

Wagabon kuihukumu Stars dhidi ya Mafarao Taifa


WAAMUZI wanne kutoka Gabon, wamepewa fursa ya kuwazihukumu timu za Taifa Stars ya Tanzania na Mafarao wa Misri katika mechi ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Afrika, Afcon 2017. Mchezo huo utapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Tanzania inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufikia rekodi ya mwaka 1980 ilipoenda Nigeria.
Mchezo huo kundi G utachezwa kuanzia saa 10.00 jioni na utachezeshwa na mwamuzi wa kati Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.

Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tariq Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia leo Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya juzi ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Mbeya City haijalala mwanangu

http://mbeyacityfc.com/wp-content/uploads/2016/05/city-in-malawi-copy.jpgWAKATI klabu nyingine zikienda likizo kwa ajili ya mapumziko ya Ligi Kuu Bara, Mbeya City haijalala kwani inatarajiwa kufanya ziara ya kisoka Malawi.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, kikosi hicho cha Mbeya City kinatarajia kufanya ziara hiyo ambapo itacheza mechi tatu za kirafiki za kimataifa ili kuwapa uzoefu nyota wao kabla ligi haijaanza baadaye mwaka huu.
Kwenye ratiba hiyo, City itaanza kushuka kwenye Uwanja wa Kamuzu, jijini Blantyre Juni 18  kwa kucheza na vigogo wa soka Malawi, Big Bullets.