STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 1, 2016

Wagabon kuihukumu Stars dhidi ya Mafarao Taifa


WAAMUZI wanne kutoka Gabon, wamepewa fursa ya kuwazihukumu timu za Taifa Stars ya Tanzania na Mafarao wa Misri katika mechi ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Afrika, Afcon 2017. Mchezo huo utapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Tanzania inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufikia rekodi ya mwaka 1980 ilipoenda Nigeria.
Mchezo huo kundi G utachezwa kuanzia saa 10.00 jioni na utachezeshwa na mwamuzi wa kati Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.

Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tariq Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia leo Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya juzi ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

No comments:

Post a Comment