STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 1, 2014

Ebu angalia usajili kabla ya dirisha kufungwa usiku wa leo

http://static.goal.com/439600/439663.jpg
WAKATI dirisha la usajili kwa klabu barani Ulaya likifungwa usiku wa leo, chini ni baadhi ya wachezaji waliohama na kutua katika klabu zao mpya mpaka sasa tukielekea ukingoni.
  • Javier Hernendez 'Chicharito' ametua Real Madrid kwa mkopo akitokea Manchester United
  • Radamel Falcao ajiunga na Manchester United kwa mkopo wa msimu mzima
  • Arsenal inapigana kupata saini ya Matija Nastasic na Ron Vlaar
  • Lewis Holtby awasili Ujerumani Germany kwa mkopo wa kipindi chote cha msimu ambapo anajiunga na Hamburg
  • Tottenham inaongoza mbio za kumnasa Danny Welbeck ambapo Arsenal nao wanamtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United
  • Mlinda mlango aliye na wakati mzuri katika klabu ya Chelsea Petr Cech anatakiwa na QPR
  • Arturo Vidal huenda akasalia Juventus baada ya Manchester United kushindwa mpango wa pauni milioni £30
  • Sandro anatgakiwa na QPR huku Tottenham wakihitaji pauni milioni £16
  • Victor Valdes yuko katika mazunguzmo ya kujiunga na Liverpool akiwa huru
  • Benjamin Stambouli amefanikiwa vipimo vya afya kabla ya kuelekea Tottenham
  • Neil Warnock anataka wachezaji wanne kujiunga na Crystal Palace 
  • Micah Richards beki wa Manchester City anaelekea kutua Fiorentina.
  •  Alvaro Morata ameondoka Real Madrid na kutua Juventus ya Italia kumpisha Chicharito
  • Dirisha la usajili linafungwa saa tano kamili usiku huu wa Jumatatu.

  • Dunga amrejesha Robinho kikosini

    KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amemuita mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Manchester City na AC Milan, Robinho kuziba pengo la majeruhi Hulk wa Zenith kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador. 
    Dunga ambaye alitaja kikosi chake cha kwanza toka achukue mikoba kwa mara ya pili kutoka kwa Luiz Felipe Scolari baada ya Kombe la Dunia, amemchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameichezea nchi hiyo mechi 92. 
    Robinho amerejea nyumbani Brazil kucheza katika klabu ya Santos ambayo ndio alianzia kucheza soka lake baada ya AC Milan kumuuza kwa mkopo wa mwaka mmoja. 
    Dunga aliyewahi kuinoa Brazil katika miochuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kutimuliwa sasa anaelekea katika mchezo dhidi ya Colombia utakaochezwa jijini Miami Ijumaa hii akiwa na wachezaji 10 pekee waliokuwepo katika kikosi cha Scolari. 
    Baada ya kukwaana na Colombia, Brazil itachuana na Ecuador huko East Rutherford jijini New Jersey Septemba 9 mwaka huu.

    Messi aanza na gundu, yathibishwa yu majeruhi

    http://www.barcapakistan.com/wp-content/uploads/2014/01/1388427761_extras_noticia_foton_7_3.jpgNYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi huenda  akawa nje ya dimba kwa kipindi kifupi baada ya kudaiwa kuumia paja jana wakati wa Ligi Kuu ya Hispania.
    Klabu ya Barcelona imetoa taarifa ikidai kuwa nyota wake huyo amepata majeraha ya paja katika mchezo waliopata ushindi mwembamba dhidi ya Villarreal jana. 
    Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai Messi aliumia msuli wa nyuma ya paja katika mguu wake wa kulia lakini sio majeraha makubwa sana. 
    Pia ilithibitisha kuwa mshambuliaji wao mwingine Munir El Haddadi naye aliumia nyama na vipimo vya wote wawili vinatarajiwa kufanyika leo kujua ukubwa wa matatizo ya nyota wake hao. 
    Kuna hatari kubwa Messi akakosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Argentina na Ujerumani unaotarajiwa kuchezwa keshokuwa.

    Beki Manchester City Micah Richards atimkia Fiorentina

    http://www.ljsfoundation.org.uk/wp-content/uploads/2013/12/Micah-Richards_4.jpg
    Micah Richards
    BEKI wa klabu ya Manchester City, Micah Richards anatarajiwa kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia baada ya kumaliza miaka 12 akiwa Etihad. 
    Richards, 26 tayari ameshawasili Italia na anatarajiwa kuwa Mwingereza wa 24 kuichezea klabu hiyo mara atakapokamilisha usajili wake. 
    Beki huyo alikuwa mchezaji muhimu ya kikosi cha City kilichonyakuwa taji la Ligi Kuu mwaka 2012 lakini amejikuta akikosa nafasi ya kucheza chini ya meneja Manuel Pellegrini aliyeibebesha ubingwa msimu uliopita. 
    City pia bado wanasiliza ofa kwa wachezaji wao Matija Nastastic, John Guidetti na Scott Sinclair ambao wanaonekana kutokuwepo katika mipango ya Pellegrini. 
    Richards ambaye ni mzaliwa wa Birmigham alifanikiwa kucheza mechi mbili pekee za Ligi Kuu msimu uliopita na alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.

    TFF ya Malinzi yaanza kumeguka, Mtawala abwaga Manyanga

    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSQ7BeiDzxhk14-HL8gurpeyPz64Qn0tI8Gj2omoupD6K16O-zr_DKEXD68dKyPKFjspbnWu26oGUXv8rIqDr00euTQs8yEy_KCHcTtm_kVoj9G2e1gWXNpDmN1exK-AsWbAT_2YLhTlgN/s1600/DSC_0392.JPG
    Evodius Mtawala (kulia) akiwa na viongozi wenzake wa TFF kabla ya kubwanga manyang'a
    TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, aliyekuwaMkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, ameachia ngazi katika nafasi hiyo.
    Inaelezwa kuwa
    Mtawala Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Simba,  alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo na ndiyo chanzo cha kung'atuka TFF.
    Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za taaluma yake ya uanasheria.
    “Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
    “Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
    Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa miezi nane tu tangu alipoteuliwa Desemba 24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais mpya, Jamal Malinzi. 

    Rasmi Chicharito mali ya Real Madrid

    Akiwa na jezi yake mpya ya Real Madrid na Rais wa klabu hiyo Perez
    Wakati akichukuliwa vipimo vya afya na kubainika yupo fiti
    Akiangunga saini ya kuichezea klabu hiyo bingwa ya Ulaya
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Mexico, Javier Harnendez Chicharito amefaulu vipimo vya kujiunga na klabu ya Real Madrid na amekabidhiwa jezi namba 14 kwa ajili ya kuichezea wababe hao wa Ulaya kwa mkopo akitokea klabu yake ya Manchester United.
    Chichirito ambaye hakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu tangu alipotua akitokea kwao Mexico, amejiunga na Madrid akimpisha Ramadel Falcao aliyetokea Monaco aliyetua Old Trafford kwa mkopo vilevile.
    Mshambuliaji huyo alitua Ol Trafford mnamo mwaka 2010 na amenyakuliwa na Madrid ili kuchukua nafasi ya Alvaro Morata ambaye aliuzwa Juventus.

    Rais Kikwete atuma Salamu za rambirambi Mbeya

    http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/08/ajali-mbeya-298x295.jpg

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
    DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

    Telephone: 255-22-2114512, 2116898
    Website : www.ikulu.go.tz              

    Fax: 255-22-2113425



    PRESIDENT’S OFFICE,
          STATE HOUSE,
                  1 BARACK OBAMA ROAD,  
    11400 DAR ES SALAAM.
    Tanzania.
     

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu 10 vilivyotokea Mbalizi, Mkoani Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237 BFB kugongana na lori aina ya Tata Na. T 158 CSV.   Katika ajali hiyo, watu saba wengine walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
    “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba kujeruhiwa katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali nyingine kutokea Mkoani Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81 kujeruhiwa”, amesema Rais katika salamu zake.
    Rais Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa karibu kwa mienendo ya wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa na hata kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.

    “Naomba upokee  salamu zangu za rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao”Ameongeza.

    Rais Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na jamaa wa watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba wote wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

    “Ninawaombea kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ili waweze  kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika salamu zake. 


    Imetolewa na;
    Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
    Ikulu – Dar es Salaam.
    31 Agosti,2014

    Manchester United yamnasa Falcao kilaini

    http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01643/falcao_1643245a.jpg
    Add caption
     
    KLABU ya Manchester United imezipiga bao klabu za Arsenal na Manchester City zilizokuwa zikidaiwa kumnyemelea  mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao baada ya nyota huyo kutua kwao kwa mkopo akitokea Monaco ya Ufaransa. 
    Falcao, 28 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka muda mrefu kiangazi hiki kutoka Monaco ambao walimsajili kwa paundi milioni 50 mwaka jana. 
    Toka ametua Monaco Falcao amefanikiwa kufunga mabao 11 katika mechi 20 huku akikaa nje nusu msimu kutokana na majeruhi ya goti yaliyomsababisha pia kuikosa michuano ya Kombe la Dunia. 
    Mahasimu wa United katika Ligi Kuu Manchester City walishindwa kumuwania nyota huyo kwa sababu hawakuweza kumhakikishia namba katika kikosi chao. 
    Falcao pia alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na Arsenal, mabingwa wa Italia Juventus na mabingwa wa Ulaya Real Madrid.