STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

TUNAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID EL HAJJ

http://holisms.in/wp-content/uploads/2014/07/eid-mubarak-images.jpgMICHARAZO MITUPU INAUNGANA NA WAISLAM WOTE ULIMWENGUNI KUWATAKIA KILA LA HERI KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID EL HAJJ INAYOADHIMISHWA LEO DUNIANI KOTE.
SIKUKUU HII INAHITIMISHA IBADA YA HIJJA KWA WAUMINI WA KIISLAM INA MAANA KUBWA KWA WAUMINI KATIKA KUKUMBUKA TUKIO LILILOFANYWA NA MZEE WETU NA NABII IBRAHIM (AS) CHA KUTAKA KUMCHINJA MWANAE ISMAIL (AS). KABLA YA ALLAH SUBHANNA WATAALAH KUMLETEA KONDOO TOKA PEPONI ILI ACHINJWE BADALA YA ISMAIL BAADA YA KURIDHIKA NA IMANI KUBWA ALIYONAYO NABII IBRAHIM YA KUKUBALI KUMCHINJA KIPENZI CHAKE ALIYEMZAA AKIWA NA AKARAIBIA MIAKA 100.
CHA MUHIMU KWA WAUMINI WOTE WAISHEREHEKEE SIKUKUU HII KWA KUMCHA NA KUMUOGOPA ALLAH KWA KUTOSHIRIKI KWENYE MAASI NA MAMBO YA KUMUUDHI MUNGU.
WENYE UWEZO WA KUCHINJA WACHINJE KAMA UTEKELEZAJI WA SUNNAH YA SIKUKUU HII NA WASIO NA UWEZO WAJIKURUBISHE KWA KUFURAHIA SIKUKUU NA NDUGU, JAMAA NA RAFIKI NA MAJIRANI ZAO PAMOJA NA KUTAKIANA KILA LA HERI, KULA NA KUNYWA PAMOJA SAMBAMBA NA KUWAKUMBUKA WASIO NA UWEZO WAKIWAMO YATIMA, WAJANE N.K.
EID MUBARAK!

Kamote, Mashali kuwania mikanda ya UBO Mkwakwani Tanga

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhafURyATzSAlVRjzsICOUhyWMnzIy0e2kbqTM4uJLpKOBMydyX3I4Ytsf9vulZlN3YFZgqiMdDUq29zauCgQtt_gfEiT-q1CydxjQpcTIpEuprJhTiyH-a7G5e_uFYWu26PVSekC8rxpF0/s1600/DSC06608.JPG
Allan Kamote atakayewania ubingwa wa Dunia wa UBO
Thomas Mashali
BONDIA Allan Kamote wa Tanzania anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Jumapili kuzipiga na Osgood Kayuni wa Malawi katika pambano la kuwania ubingwa wa Universal Boxing Organization (UBO).
Mabondia hao watapambana katika pigano la uzani wa Light la raundi 12 kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mpinzani wa Kamote, tayari ameshatua nchini tangu juzi usiku na alitarajiwa kuelekea Tanga jana ili kuwahi zoezi la kupimwa afya na uzito leo Jumamosi.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Anthony Rutta, maandalizi ya pambano hilo na mengine ya utangulizi likiwa la mabondia Thomas Mashali dhidi ya Ali Ramadhani 'Alibaba' yamekamilika.
"Bondia kutoka Malawi ameshatua nchini tayari kwa pambano lake na Kamote na maandalizi kwa ujumla ya michezo hiyo ya Oktoba 5 yanaendelea vyema, hivyo wakazi wa Tanga na maeneo ya jirani wajiandae kupata burudani," alisema Rutta.
Mabondia hao wawili walishakutana mara mbili kabla ya pambano hilo la Jumapili na mara zote Mtanzania Allan Kamote amepoteza mbele ya Kayuni na hivyo pigano la keshokutwa ni nafasi ya Kamote kujifuta aibu nyumbani.

BASATA wampongeza DIAMOND Platnumz

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   PONGEZI KWA MSANII NASSIB ABDUL AKA DIAMOND KWA KUSHINDA TUZO YA MSANII BORA WA MWEZI WA KITUO CHA MTV BASE
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo ya Msanii bora wa mwezi wa kituo cha televisheni cha MTV Base kinachorusha matangazo yake kutoka Afrika Kusini na kuyafikia maeneo mengi duniani.
Aidha, Baraza linampongeza msanii huyu na wenzake Peter Msechu na Vannessa Mdee kwa kuchaguliwa kushindania tuzo mbalimbali katika tuzo za “All Africa Music” (Afrima) ambapo nyimbo zaidi ya 2025 kutoka kwa wasanii mbalimbali barani Afrika zinatarajiwa kushindanishwa na washindi kupatikana.
Kuteuliwa na kushinda kwa Wasanii wa Tanzania katika tuzo mbalimbali za Afrika na duniani ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na nje ya Tanzania.
Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kulitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI

Katibu Mwenezi BAWACHA afichua kilichomkimbiza CHADEMA

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/10/396300_216970381724652_100002350745009_483378_1721045790_n.jpg 
Na Kipimo Abdallah
ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Jimbo la Kawe, Batuli Kivuma ambaye amejiunga na chama cha Alliance for Change and Transparent (ACT-Tanzania amesema kilichomuondoa CHADEMA ni ukabila ulioota mizizi kwa muda mrefu.
Kivuma ambaye awali alikuwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi CUF alisema aliamini kuwa chama hicho kinasimamia demokrasia jambo ambalo limeshindikana hasa ukiwa hotekei mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema tangu ajiunge katika chama hicho amekuwa na juhudi za kukijenga chama hasa Kata ya Msasani na jimbo zima la Kawe ila juhudi zake zimekuwa zikikwamishwa kwa misingi ya ukabila.
Katibu Mwenezi huyo wa zamani wa BAWACHA alisema katika kudhihirisha hilo alishiriki kwenye  mchakato wa kugombea nafasi ya Udiwani viti maalum mwaka 2010 ambapo alishinda ila aliondolewa kwa kigezo cha yeye ni Mdigo na wakapewa nafasi hiyo Wachaga.
“Kusema ukweli suala la kuhama vyama sio zuri ila inafikia mahali unashindwa kuvumilia kwani nimekuwa nikionewa mara kwa mara katika chaguzi na ukiangalia vizuri msingi wake ni ukabilia ambao unawabeba Wachaga” , alisema.
Kivuma  alisema alikuwa akikipenda sana chama hicho lakini ubaguzi uliopo amefikia mwisho wa uvumilivu na kwamba anahitaji kuonyesha jitihada zake kwingine.
Alisema suala hilo la ukabila lilikidhiri katika uchaguzi mkuu ambao ulifanyika hivi karibuni hasa katika upande wa BAWACHA ambapo juhudi zilifanywa kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.
Mwenezi huyo wa zamani wa BAWACHA alisema hata upatikanaji wa Mwenyekiti wa BAWACHA wa sasa Halima Mdee ulitawaliwa na ukabila ikiwa ni agizo la Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe.
"Unajua hili neno demokrasia wanalielewa je bwana kwani kwa ufahamu wangu ni kuhakikisha kuwa jamii inaacha pale inapofanya maamuzi yake ila huku ni kinyume", aliongezea Kivuma.
Kivuma alisema atahakikisha kuwa anakibomoa CHADEMA hasa katika Jimbo la Kawe ambapo amefanya kazi za kisiasa kwa muda mrefu.
Kwa upande wake aliyekuwa Mjumbe wa Mtaa Serikali ya Mtaa wa Matofalini Ujiji Kigoma Yassin Mohamed alisema ni vema vyama vikatambua kuwa hakuna uadui baina yao na kuhama chama ni haki ya mtu.
Alitolea mfano hali ya kisiasa ilivyokuwa siku za nyuma kati ya chama na CHADEMA na CUF hali ambayo kwa sasa haipo na vinafanya kazi pamoja.
Mohamed alisema ameamua kujiunga na ACT-Tanzania na kuondoka CHADEMA ili kupata uhuru wa kupigania demokrasia ya kweli.

Tanzia:Ally Choki apata pigo, afiwa na mkewe Mama Shuu

Mama Shuu enzi aa uhai wake
[3.JPG]
Ally Choki aliyefiwa na mkewe. Pole sana kaka kwa msiba ulioupata Mungu akupe Subira katika kipindi hiki kigumu
MKURUGENZI wa bendi wa Extra Bongo na mmoja wa waimbaji nyota nchini wa muziki wa dansi, Ally Choki amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na Mkewe maarufu kama Mama Shuu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanamuziki wa Africana Stars, Twanga Pepeta, Rama Mhoza 'Pentagone', mke wa Choki alifariki usiku wa kuamkia leo na taratibu za mazishi zinaendelea jijini Dar es salaam.
MICHARAZO inatoa pole kwa Choki, ndugu, jamaa na wadau wote wa muziki wa msiba huo ila ikiwakumbusha kuwa Sisi Sote tu waja wa Allah (SW) na Kwake Tutarejea. Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mama Shuu Mahali Pema Pepon. Ameen

Taifa Stars kuingia kambini keshokutwa kuwasubiri Benin Taifa

Kocha Mart Nooij akizungtumza huku Nahodha Nadir Haroub Cannavaro akisikiliza kwa makini
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1728070/highRes/480649/-/maxw/600/-/eoklao/-/stars.jpgKIKOSI cha wachezaji 26 walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam wataingia kambini keshokutwa Jumatatu.

Kocha Mart Nooij aliyetangaza kikosi akiwa mjini Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), alisema kikosi hicho kinachodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Jumatatu.
Wachezaji watakaoingia kambini keshokutwa ambao waliitwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na;
Makipa: Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki:Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo: Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji: Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

HIVI NDIVYO VIKOSI VYA LIGI KUU TANZANIA 2014-2015

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQU3LvczbZmaG2iN7rSrxVpCUV5LQ2K-ynHw6lk7BLgSR3V7uaCFMCXXstuCqtvsi6zGD96zxWQXZKdykLBE8kB5MsMXi0yrZBhF2fPHuKjHqKqVB_fbb_ID9vBtnh4xmA1ivApnVfkYit/s1600/DSC_0015.JPG
Azam Fc

AZAM FC;
Mwadini Ali Mwadini, John Bocco, Aggrey Morris, Abubakar Salum, Mudathir Yahya, Wandwi William Jackson, Said Hussein Morad, Didier Kavumbagu, Braison Raphael, Frank Domayo, Shomari Kapombe,
Leonel Saint Preux, Ismaila Diarra, Abdallah Kheri, Gardiel Michael Mbaga, Kelvin Friday Iddi, Farid Mussa Malik, Joseph Kimwaga, Kipre Tchetche Herman, Brice Dizana Issa, Kipre Bolou Wilfred,
Himid Mao Mkami, Khamis Mcha, David Mwantika, Aishi Manula, Gaudence Mwaikimba, Waziri Salum na Erasto Nyoni.

http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/DSC04881.jpgCOASTAL UNION:
Itubu Imbem, Mshauri Salim, Mansoor Mansoor, Abdallah Mfuko, Bakari Mtama, Hamadi Juma, Hussein Sued, Joseph Mahundi, Hamisi Mbwana, Ayoub Yahaya, Behewa Behewa, Daniel Liyanga,
Shaaban Kado, Bright Ike, Keneth Masumbuko, Mohamed Rajab, Mahmoud Abdul, Rama Salim, Ally Iddi, Yayo Lutimba, Yusuph Chuma, Mohamed Mtindi, Razak Khalfan, Sabri Rashid, Tumba Lui,
Amani Juma, Abdallah Rajabu, Twalib Ali, Selemani Rajabu, Banda Abdi, Abassi Athuman, Abdurahman Sembwana, Ali Mohamed, Athuman Athuman, Ayoub Masood, Fikirini Bakari, Hamisi Rajab, Haruna Salim, Hatibu Hatibu, Juma Mahadhi, Kapama Kapama, Mbwana Mnyaongo, Mohamed Haji, Mohamed Shekuwe, Mtenje Juma, Mwaita Gereza, Zamiru Said, Tumaini Mosha, Omar Mohamed na Peter Terry.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyEobPE20ZtNi1R-UopKnA1am4dMWYZsa7756AEyfSHcvOosRNMAP-efMmHJrvyF7Ow87HahcM35Mc0PHS1WKnJYrQVgpIPDUG7wM0AXLdLATZWM_FgJbvsrDo8w3YZiZ3RL3zmCrX9Dff/s1600/DSC_0125.JPG
JKT RUVU;
Benjamin Haule, Jackson Chove, Alex Abel, Ally Bilaly, Richard Maranya, Furaha Tembo, Napho Zuber, Jaffary Kissoky, Mohamed Faki, Samwel Kamuntu, Issa Kanduru, Jabir Aziz, Emanuel Pius, Gido Simon, Cecil Efrem, Naftali Nashon, Renatus Morris, Iddi Mbaga, Ramadhani Shamte, Amos Edward, George Minja, Damas Makwaya, Nurdin Mohamed, Shabani Mohamed, Madenge Ramadhani, Haruna Adoph, Reliant Lusajo, Juma Godfrey na Najim Magulu.

KAGERA SUGAR;
Adamu Juma Kingwande, Eric Kyaruzi, Daudi Jumanne Kaipe, Salum Kupela Kanoni, Adamu Juma Said Kingwande, Malegesi Samwel Mwangwa Missana, Agathon Antony Mkwando, Benjamin Edward Asukile Mwampa, Paul Lucas Paul Ngalyoma, George Benisius Hilary Kavira, Julius Ambrose Paul, Yusuf Komba Hussein, Abubakar Twaha Msuya Mtiro, Dickson Fredrick Muganda, Atupele Green Jackson Mwaiseba, Hamisi Mwinshehe Kurabu, Andrew John Ntala Simutala, Isaac Job Ibrahim, Shai Mpala Jafari, Victor Husseni Hangaya, Hassan Hamisi Abdallah Sharia, Fred Msafiri Mnubi, Abdulkadir Suleiman Mohamed Ali, Mohamed Abdallah Raashid, Abdallah Yusuph Rwenda, Mohamed Athuman Mohamed Dikongwa, Zed Maulid Zed, Omary Ramadhan Milambo, Ally Abdallah Silas Kagangule, Hamza Rwambow Abdallah, Salehe Hamidu Issa na Rashid Habibu Yusuph Mandawa.

MBEYA CITY:
Yohana Morris, Anthony Matogolo, Deogratus Julius, Alex Seth, Christian Sembuli, Richard Peter, Paul Nonga, Ken Ally, Mwagane Yeya, Hamidu Mohamed, Temi Felix, Steven Mazanda, Eric Mawala, Yusuph Abdallah, Ramadhani Abdi, Deus Kaseke, John Kabanda, Peter Mwalyanzi, Peter Mapunda, David Burhan, Abdallah Seif, Hamad Kibopile, Hassan Mwasapili, Lambon Ashley na Saady Kipanga.

MGAMBO JKT:
Bushiru Mohammed, Salum Said Mlima, Bolly Shaibu Ajaly, Salum Kipaga, Salehe Tendega, Godson Mmasa, Fransis Anyosisye, Said Chambo, Hassan Kibakuli, Mohamed Namkopwe, Mohamed Samatta, Salim Gilla, Novaty Lufunga, Nassoro Athuman Gumbo, Henry Athanas Chacha, Salum Hamis Kipaga, Ramadhan Adam Malima, Sabry Ally Makame, Ally Nassoro Iddy, Chande Hemed Magonja, Pera Ramadhan Mavuo, Uda Sorita Bakarim, Said Salehe Lubawa, Ayoub Salehe Mrisho, Fully Zully Maganga, Malimi Francis Busungu, Damas Phlidorin Milanzi, Boniface Charles Mkumbo, George Paschal Safari, Adam Mohammed Kindemba, Frank Shedrack Humbo, Hilal Faraji Chohadi, Mpokigwa Wilfred Wafumbela, Said Hamisi Abdul, Wistonne Mujuni Kasimbazi, Kuha Hilaly Fabian, Gunda Kumenya  Sozzy, Bakari Mwaita Mweleka, Mansour Omar Makame, Issa Kagia Kigingi, Emnanuel John Elliot, Adam Mussa Athuman, Mohammed Abubakar Zubery, Japhet Mkanga Samson, Aziz Fathawi Eddie, Sadick Khalid Mndeme na Onesmo Thomas Guguluu.

 
MTIBWA SUGAR;
Bahati Bernard Malishali, Athuman Abdallah Kado, Said Afidhu Fadhili, Mohamed Ally Mohamed Kassim, Erick Shukuru Salum Hassan, George Aidan George Mhesa, Said Rashid Ndavanje, Issa Nassoro Kigaga, Mursheed Juma Katundu, Hilal Juma Kapera, Bakari Ally Mtwiku, Ibrahim Auf Seif Mwae, Mussa Mohamed Kirungi, Deograsias Deodatus January Lyandungwe, Mkombozi Hakimu Ayubu, Songa Bethel Jared, Baraka Pearson Antony Kodi, Yassin Hamidu Abeid, Hassan Salim Mbande, Shiza Ramadhan Kichuya, Patrick Athanas Michael Madidi, Ahmad Siasa Msumi, Salim Hassan Abdallah Mbonde, Said Mohamed Said, Jamal Simba Mnyate, Abdallah Salum Juma, Ally Shomari Sharifu, Stanley Leonard Minzi, Khomeiny Abubakry Barwany, Abdallah Said Makangana, Dickson Daudi Mbeikya,
Mzamiru Yassin Selemba, Vicent Barnabas Salamba, Mohamed Ally Ibrahim, Majaliwa Shaban Mbaga,
Mussa Hassan Mgosi, Shaaban Mussa Nditi, Said Ally Mkopi, Andrew Vicent Chikupe, Hassan Khamis Ramadhan, Ally Bakari Lundenga, Ame Ally Amour, Mussa Mohamed Nampaka, Mohamed Salum Mkopi, David Charles Luhende, Ally Makarani Yusuph, Hosam Spear Mbwembwe, Madinda Ramadhan Mfaume na Juma Ally Luzio.

NDANDA FC;
Salehe Malande, Rajabu Isihaka, Cassian Ponera, Ibrahim Mwaipopo, Hemed Khoja, Saidi Mketto, Elius Joseph Ndokezi, Iddi Juma Kulachi, Jeremia Ramadhan Kisubi, Nassor Kapama, Sadam Likote Abdallah, Majid Abdallah, Kassim Omar, Hamisi Maulid, Shukuru Mussa Chachala, Mohamed Juma,
Azizi Sibo, Paul Ngalema, Gideon Benson, Wilbert Mweta, Ernest Mwalupani, Jacob Masawe na Amiri Msumi.

POLISI MORO;
Chacha Marwa, Yahya Mohamed, Yahya Mohamed, Godwine Boniphace, Yahya Mohamed, Abdallah Kingalu, Hiyali Mnyao, Idd Ahamad, George Emmanuel, Rothan Mkanwa, Petro Joseph, Mansury Nassibu, Edgar Charles, Tony Kavishe, Moses Mtitu, Simon Fanuel, Danny Mrwanda, Lulanga Mapunda, Benedicto Magumba, Laban Kambole, Suleiman Kassim, Bantu Admin, Anaf Suleiman, Mohamed Mpopo na Edward Christopher.

PRISONS FC;
Jonathan Lugano Mwangama, Patrick Ntula Mwakibona, Castro Ally Kosam, Mando Lusekelo Mkumbwa, Michael Mpesa Ismail, Beno David Kakolonya, Stanley Simon Hamu, Hasan Omari Kamwela, Frank Mwesigwa Bilaze, Frank William Linus, Rajab Abdallah Hamisi, Lambarti Charles Sabiyanka, Jimmy Shoji Mwaisondola, Ibrahim Isaka Hassan, Salum Mashaka Kimenya, Laurian Shaaban Mpalile, Said Mtupa, Meshack Suleiman, Mfaume Chilumba, Godfrey Magetha, James Mwasote, Hamisi Kasanga, Iginas Simsonga, Aby Athumani,
Francis Humbo, Vedastus Mwihambi, Mpoki Mwansasu, Tito Mwaipaja, Enock Balagashi, Zamoyoni Hamisi, Nasoro Ngaja, Josseph Mapalala, Emmanuel Mwambashi, Lisa Mwaifweya, Emanuel Mnyali, Mfaume Lyonga, Elick Mwakijambile na Jacob Mwaitalako.

RUVU SHOOTING:
Raphael Bathromeo Keyala, Abdul Juma Seif, Abdallah Rashid Abdallah, Juma Said Mdindi, Abdallah Seif Rashid, Salvatory Venance Ntebe, Abdul Ally Mpambika, Ernest Jackson Ernest, Bidii Hussein Abdallah, Justin Chagu Chagula, Yusuph Innocent Nguya, Kassim Zuberi Dabi,
Juma Mohammed Mpakala, Abdulrahaman Mussa Abdulrahaman, Ally Hamis Kaijage, Abbass Waine Natalis, Rashid Salehe Tarimo, Kassim Salum Mdoe, Deogratius John Kwanzo, Salum Mwalami Lubawa, Baraka Shaaban Mtuwi, Isihaka Hussein Sembuli, Mohamed Said Abdallah, Salim Kibwana Kilagi, Majid Musisi Nassibu, Adam Omary Seseme, Abdallah Juma Hassan, Kambo Zuberi Zinyori, Sudy Ayoub Chemchem, Saad Ally Ndoleni, Hamisi Selemani Kasanga, Ambele Daudi Hamis, Mathayo Herzon Willson, Juma Hamisi Nade, Stephano Asangalwisye Mwasyika, Lambele Jerome Ruben, Frank Faraja Msese, Ally Khan Mkanga, Juma Seif Dion, Raphael Bathromeo Keyala, Michael Aidan Pius, Ayoub Salehe Kitala, George Ossey Maiko,
Said Imani Madega, Hassan Omary Gumbo na Haki Hassan Lubea.

 
SIMBA SC:
Shaffi Hassan Rajab, Saidi Hamisi Juma, Shaabani Kisiga, Uhuru Suleiman Mwambungu, William Lucian Elias, Awadh Juma Issa, Emmanuel Okwi, Abdallah Seseme, Abdi Banda, Amissi Tambwe, Amri Kiemba, Elias Maguri, Haroun Chanongo, Hussein Shariff, Hassan Isihaka Hussein, Twaha Ibrahimu, Ibrahim Migomba, Issa Rashid Issa, Ivo Mapunda, Jonas Mkude, Joram Mgeveke, Joseph Owino, Peter Manyika Peter, Miraji Adam Suleiman, Mohamed Husseini Mohamed, Said Nassor Masoud,
Pierre Kwizera, Ramadhani Singano, Raphael Kiongera, Abdul Misiru, Denis Richard Deonis, Elia Jaffary Nyondo, Iddy Bahati Khamis, Issa Abdallah, Juventus Joseph, Malik Kapolo, Mbaraka Abeid, Miza Abdallah, Omary Hamisi Hassan, Omary Matola, Patrick Mhagama, Saidi Issa Mohamed, Salum Abbas Salim, Seleman Ibrahim Omar, Yunus Dadi Kambi, Abdulaziz Makame na Yunus Benard Moshi.

STAND UNITED:
Mussa Said, Pastory Athanas, John Mwenda, Peter Mutabuzi, Robert Magadula, Iddy Mobby, Hamad Juma, Kheri Mohamed, Salum Kamana, Mohamed Soud, Swalehe Abdallah, Mohamed Makaka, Jisend Maganda, Richard Elisha, Alex Masanja, Ally BakarI, Baraka Ramadhani, John Michael, Hussen Yassin, Abasirim Chidiebere, Daud Mwita, Geneya Thimos, Kulwa Jackson, Lucas Charles, Mawazo Jumanne, Paschal John, Daniel Barnabas, John Ganga, Hussein Rajab, Hussein Ally, Kitoba Emmanuel, Omary Mtaki, Nelson Kimath, Juma Ramadhani, Revocatus Richard, Tola Anthony, Yassin Mustapha, Karim Sadick, Hashimu Ramadhani, Kassim Kisengo, Reyna Mgungira, Ismail Mchame, Paschal Mrope, Khalid Suleiman na Saturday Baraka.

http://api.ning.com/files/JSct6ft9ycR27Xjb-D8vTJOgspZD10uV9u2oBuswwtecqIFoY9qgHQswx-6142uEW*FFyhfB9XOVBwnm7Ja5YepDgKixFJZc/IMG_2791.JPGYANGA SC:
Emmanuel Arnold Okwi, Andrey Marcel Ferreira Coutinho, Geilson Santana Santos, Ally Mustafa Mtinge, Salum Abdul Telela, Oscar Joshua Fanuel, Rajab Zahir Mohamed, Kelvin Patrick Yondani, Mbuyu Junior Twite, Haruna Niyonzima, Jerson John Tegete, Said Rashid Bahanuzi, Juma Kaseja Juma, Omega Sunday Seme, Pato George Ngonyani, Nizar Khalfan Khalfan, Mrisho Khalfan Ngassa, Hamisi Thabit Mohamed, Hamisi Kiiza, Hussein Omar Javu, Nadir Haroub Ali, Hassan Salehe Dilunga, Simon Happygod Msuva, Deogratias Boneveture Munishi, Juma Abdul Jaffar, Said Juma Ali, Edward Charles Manyama, Almasi Juma Majaliwa, Amos Abel Charles, Ayoub Mohamed Ayoub, Bennito John Michael, Frank Gerald Maulaga, Frank Shineta Kijoti, Gadafi Hamis Kapondo, Hamisi Issa Kipande, Hassan Ngilo Nyonho, Hussein Mwakipa Hussein, Issa Hamis Ngao, Juma Kayanda John, Junior Ricky Paulo, Mandela Mgunda Mussa, Ramadhani Awam Kabwili, Said Ally Ndutu, Salum Suleiman Abdallah, Sospeter Maiga Kasoli, Mwinyi Bakari Juma, Shaaban Idd Shaaban, Joseph Mapembe Simbaulanga na Almasi Juma Majaliwa.

Klabu zatishia kuigomea Ligi Kuu, kumng'oa Malinzi madarakani

http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/NDUMBAROZ7067-11.jpg
Damas Ndumbaro (kulia)
http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2013/11/malinzi1.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
SIKU moja  baada ya Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal  Malinzi kutangaza kuvibana vilabu vya ligi kuu kuchangia mapato yao kwa asilimia tano ili kuchangia miradi mbalimbali iliyo anzishwa na shirikisho la soka nchini, vilabu vya ligi kuu kupitia kwa mwanasheria wao Dr Damas Ndumbaru vimetishia kugomea kuendelea na ligi kuu.
Rais wa TFF, Malinzi kusisitiza lazima klabu zikatwe asilimia 5 kwenye fedha zao za udhamini wa Vodacom na Azam TV, zenyewe zimejibu mapigo.

Hata hivyo kupitia mwanasheria wao, klabu 14 za Ligi Kuu Bara, zimesisitiza mambo haya ya msingi, kuwa hazitavaa jezi zenye nembo ya wadhamini hao, kupinga kukatwa fedha zao.
Pili, zitaitisha mkutano wa dharura wa kamati ya utendaji kupiga kura ya kutokuwa na imani na Malinzi ambayo itamuondoa madarakani.
Mwanasheria maarufu nchini Dk Damas Daniel Ndumbaro amesema kwa mujibu wa katiba ya TFF, klabu hizo 14 ambazo ni mwanachama zinaruhusiwa kufanya hivyo.
“Hilo linaruhusiwa kwa mujibu wa ibara ya 25 (ibara ndogo ya TFF) kama wanachama tuitishe mkutano mkuu maalum.
“Katika mkutano huo tutapiga kura za kutokuwa na imani na Malinzi, kinachotakiwa ni kufikia theluthi mbili tu, yaani kura mia moja,” alisema Ndumbaro.
TFF ina wanachama 150, hivyo kama utaitishwa na kufikisha theluthi hizo mbili za kura ya kutokuwa na imani, Malinzi atakuwa ameng’oka madarakani.
Uamuzi wa klabu hizo kupinga umetokana na kwamba TFF kupitia sekretarieti yake iliyodai ni kwa mujibu wa kamati ya utendaji, imepitisha uamuzi wa kutaka ipewe asilimia 5 ya fedha za udhamini za klabu.
Jambo hilo halijafanyika sehemu yoyote duniani, pia kumekuwa hakuna ufafanuzi mzuri wa kutosha zaidi ya Malinzi kusisitiza kuwa ni lazima fedha hizo zikatwe.
Kiutaratibu inaonyesha klabu ndiyo zinazotangaza wadhamini hao, ndiyo zenye haki ya fedha hizo.
Lakini katika mapato ya milangoni, fedha zimekuwa zikikatwa fedha ambazo zinakwenda kwenye mfuko wa maendeleo ya soka nchini ambao sasa TFF unataka ukate na fedha za wadhamini.

Mbeya City na Mtibwa Sugar, zimetishia kuifikisha TFF mahakamani kama itaendelea kulazimisha uamuzi huo.

Wakijiandaa kuivaa JKT kesho, Jaja aweke rekodi Yanga 2014-2015

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQD9zGjMKlGjDtiG0PcThHe6lEsE6teLq8d3OG3Ky4pkrFbBbT1T_olSTRW1jKQeLphL6-M1nxf8JwXmzVCU-CtsCuyXs1xNK-J2YdgGOy97cURhrsDqyNOQOB8LwyRBA_Tw7VutMVe9T-/s1600/jaja.jpg
Jaja
LICHA ya kwamba huenda asiwepo kwenye kikosi cha kesho kitakachowavaa JKT Ruvu kutokana na kudaiwa kuwa majeruhi, Mshambuliaji mpya wa Yanga kutoka Brazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ ameweka rekodi katika kikosi cha timu hiyo kwa msimu wa 2014-2015.
Jaja, aliyekuwa gumzo baada ya kufunga mabao mawili yaliyoizamisha Azam kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, likiwamo la pili ambalo limezoelekea kuonekana kwenye 'kideo'. ndiye mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuonyeshwa kadi ya njano na kukosa penalti msimu huu.
Mbrazil huyo anayedaiwa kukingiwa kifua na kocha Marcio Maximo, licha ya kuonekana mzito dimbani, alipewa kadi ya njano katika pambano la kwanza la Yanga dhidi ya Mtibwa kabla ya kuja kukosa penati wakati timu yao ikizama kwa mabao 2-0 uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Vumbi Ligi Kuu England kutimka leo, Chelsea v Arsenal ni Sheeda kesho

http://img.eplmatches.com/2014/06/premier-league.jpghttps://infobase360.files.wordpress.com/2014/08/barclay2014-2015-teams.pngVUMBI la Ligi Kuu ya England inatarajiwa kuendelea kutimka tena leo kwa michezo sita tofauti, ambapo mabingwa watetezi Manchester City watakuwa ugenini kuvaana na Aston Villa, huku Liverpool ambayo imekuwa ikigawa takrima katika ligi hiyo watajiuliza nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion pale Anfiled.
Mechi  nyingine kwa mujibu wa ratiba hiyo kwa leo ni kwamba Hull City watakuwa nyumbani kuikaribisha Crystal Palace na Leicester City wataialika Burnley wakat Swansea City wataikaribisha Newcastle United.
Pambano jingine kwa siku ya leo ni kati ya Sunderland itakayokuwa nyumbani kuivaa Stoke City.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mipambano ya kukata na shoka wakati Arsenal itasafiri hadi Stanford Bridge kuvaana na wenyeji wao Chelsea ambao kwa miaka ya karibuni wakiwa chini ya Jose Mourinho wamekuwa wakiionea Ze Gunnerz.
Vijana wa Luis Van Gaal, Manchester United watakuwa uwanja wa Old Trafford kuikaribisha Everton katika pambano jingine 'tamu' kwa kesho huku Tottenham Hotspur watakuwa nyumbani kuwaalika Southampton.
Kadhalika kesho litashuhudiwa pambano kati ya West Ham United itakayoumana na QPR
Hii ndiyo ratiba kamili ya wikiendi hii;

Leo Jumamosi:
17:00 Hull vs Crystal Palace
17:00 Leicester vs Burnley
17:00 Liverpool vs West Brom
17:00 Sunderland vs Stoke
17:00 Swansea vs Newcastle
19:30 Aston Villa vs Man City

Kesho Jumapili:
14:00 Man United vs Everton
16:05 Chelsea vs Arsenal
16:05 Tottenham vs Southampton
18:15 West Ham vs QPR

Simba majaribuni tena leo Taifa, Yanga kujiuliza kwa JKT Ruvu kesho

Simba wanaoingia tena majaribuni kusaka ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu
Azam wapo ugenini Mjini Mbeya kuvaana na Prisons wataendeleza ubabe au...!
Mbeya City wanatoka kwa mara ya kwanza kuvaana na Ruvu Shooting-Mbatini
Mtibwa wenyewe watashuka dimbani kesho kuvaana na Mgambo JKT

Ndanda Kuchele watakuwa Mkwakwani kujiuliza kwa Coastal Union
Baada ya kushindwa kuhimili vishindo vya Yanga, Prosns kuvuna nini kwa Azam leo?
Yanga wataendeleza ubabe wao kwa JKT Ruvu au watazamishwa Taifa kesho

BAADA ya kushindwa kupata ushindi katika mechi mbili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Taifa, Simba leo itashuka tena kwenye dimba hilo kujaribu bahatai yake kwa timu iliyopanda daraja ya Stand United wakati watani zao wakijiandaa kuivaa JKT Ruvu kesho katika uwanja huo huo wa Taifa.
Simba iliambulia sare mbili kwa Coastal Union na Polisi Moro na kuibua taharuki kwa mashabiki wao ambao hawaamini kama timu yao ndiyo inayochechemea katika ligi hiyo baada ya kufanya mabdiliko ya benchi ya ufundi na kikosi chao toka kile cha msimu uliopita kiliochowanyima raha na kuambulia nafasi ya nne.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri ameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake ili kupata ushindi baada ya kuchoshwa na sare mfululizo, huku wakitangulia kufunga mabao na kurejeshwa na wapinzani wao.
Ushindi pekee ndiyo utakaoisaidia Simba kuwatuliza mashabiki wao ambao tayari wameanza kumsaka mchawi wakiamini mgawanyiko wa makundi ya wanachama ni sababu ya 'kuhujumuiana'.
Wakati Simba ikipania kupata ushindi wake wa kwanza wapinzani wao walionja ushindi katika mechi yao iliyopita dhidi ya Mgambo JKT imeapa kuendelea kuwatonesha Msimbazi kwa kuwagiwa dozi ili waendelee kula tamu ya ligi hiyo wanayoicheza kwa mara ya kwanza msimu huu.
Kikosi hicho kupitia kocha msaidizi, Athuman Bilal 'Bilo' kimetamba kuwa kinatambua Simba kama timu kubwa na kongwe, lakini soka halitegemei vigezo hivyo zaidi ya timu kujituma na kupata uishindi uwanjani kitu ambacho wamekipania kufanya hivyo jioni ya leo.
Mbali na pambano hilo leo kuna mechi nyingine nne katika viwanja tofauti ambao mabingwa watetezi na vinara wa msimamo huo kwa sasa, Azam watakuwa ugenini kuwakabili wenyeji wao Prisons ya Mbeya inayouguza kichapo cha amabao 2-1 ilichopewa na Yanga wiki iliyopita.
Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na ukweli hiyo ni mechi ya kwanza ya nyumbani kwa Prisons na ya kwanza ya ugenini pia kwa Azam walioshinda mechi mbili za awali nyumbani uwanja wa Chamazi dhdidi ya Polisi Moro na Ruvu Shooting.
Ruvu wanaoburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo watakuwa uwanja wa nyumbani kuwaalika Mbeya City wakiwa na machungu ya kupoteza mechi zao mbili za awali huku wakiwa hawana bao hata moja kuonyesha kwamba pengo la Elias Maguri, bado halijapata mbadala wake.
Kocha Tom Oloba amesema kuwa anaamini timu yake leo itashinda nyumbani baada ya kurekebisha tatizo lililokuwa likiikabili Ruvu hasa eneo la kiungo na ushambuliaji waliokuwa wakipoteza mipira kizembe.
Pambano jingine ni lile litakalochezwa mjini Morogoro wakati Polisi watakapowakaribisha kwenye uwanja wa Jamhuri, Kagera Sugar ambao mechi yao ya tatu sasa wapo ugenini, huku Ndanda Fc walioanza kwa mbwembwe ligi hiyo kwa kuicharaza Stand mabao 4-1 itakuwa wageni wa Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Siku ya kesho Yanga watavaana na maafande wa JKT Ruvu wanaonolewa na nyota wao wa zamani na aliyekuwa kocha msaidizi wa vijana wa Jangwani, Fred Felix Minziro.
Katika mechi ya mwisho kukutana kwa tyimu hizo msimu uliopita, Minziro na vijana wake waliaibika kwa kukandikwa mabao 5-1, jambo ambalo hata hivyo halitegemewi litokee leo hasa baada ya JKT Ruvu kusuka upya kikosi chake na kikiwa na usongo wa kutaka kupata ushindi wa kwanza katika ligi hiyo.
Maafande hao walianza kwa suluhu mjini Mbeya kabla ya kutolewa nishai wiki iliyopita na Kagera Sugar hali inayowafanya Yanga wajiandae kukabiliana na upinzani mkubwa toka kwa vijana hao wa Minziro.
Pambano jingine litakalochezwa kesho litakuwa ni kati ya Mtibwa Sugar watakaoialika Mgambo JKT wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi zao mbili za awali na kuongoza msimamo sambamba na Azam.
Mtibwa inayonolewa na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime ilianza kwa kuinyuka Yanga mabao 2-0 kabla ya kuwazima Ndanda kwa mabao 3-1, huku wenzao walianza kwa kuilaza Kagera Sugar bao 1-0 na kulala kwa idadi kama hiyo mbele ya Stand United kitu kinachofanya pambano hilo kushindwa kutabirika mapema.
Je ni timu zipi zitakazocheka au kulia kwa leo na kesho? Bila shaka ni suala la kusubiri baada ya dakika 90 kumalizika katika viwanja vitakavyotumiwa kwa mipambano hiyo ya kusisimua ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Francis Cheka kuzipiga Namibia kuwani ubingwa wa WBU


BINGWA wa zamani wa Dunia wa WBF, Francis Cheka anatarajiwa kupanda ulingoni  mwishoni mwa Novemba nchini Namibia kupigana na mwenyeji wake Harry Simon katika kuwania ubingwa wa WBU.
Pambano hilo la uzito wa Light Heavy litakalokuwa la raundi 12 litachezwa Novemba 29 kwenye Uwanja wa Kuisebmond mjini Walvis Bay, nchini humo.
Cheka atakuwa na kibarua kizito kwa bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 29 na kushinda yote, 21 yakiwa ya KO, huku akiwa hajapoteza wala kutoka sare mchezo wowote.
Mkanda huo wanaouwania ulikuwa wazi na hivyo kutoa nafasi kwa Cheka kurejesha heshima yake iwapo atafanikiwa kumpiga Simon na kutwaa taji hilo katika ardhi ya ugenini.
Kwa muda mrefu, Cheka amekuwa hafanyi vizuri nje ya Tanzania na hiyo ni nafasi yake ya kuuthibitishia umma kwamba yeye ni mkali kokote kwa kumshinda mpinzani wake.
Mara ya mwisho Cheka kupanda ulingoni ilikuwa Aprili mwaka huu alipopigna na bondia kutoka Iran, Sajjad Mehrabi na kutoka naye sare.
Cheka alitwaa mkanda wa Dunia wa WBF kwa kumchakaza Mmarekani Phil Williams Agosti mwaka jana kabla ya kupoteza ubingwa huo alipoenda kuchezea kichapo cha 'mbwa mwizi' nchini Russia kwa kupigwa KO ya raundi ya tatu na Fedor Chudinov.

Arsenal bado Majanga, Ramsey aumia tena kuwakosa Chelsea kesho

http://i.huffpost.com/gen/1718401/thumbs/o-AARON-RAMSEY-facebook.jpgKIUNGO Aaron Ramsey atalikosa pambano la kukata na shoka la kesho kati ya timu yake ya Arsenal dhidi ya Chelsea sambam,ba na mechi nyingine baada ya kuthibitika kuwa ni majeruhi.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa atamkosa Ramsey kwa wiki nne au zaidi. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alipata majeruhi ya msuli wa nyuma ya paja wakati wa mchezo wa Ligi Kuu uliokwisha kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs Jumamosi iliyopita.
Kuumia huko kunamfanya akose mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano na michezo kadhaa ya Ligi Kuu ukiwamo wa kesho dhidi ya Chelsea. 
Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa Ramsey anaweza kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne lakini Wenger amesema nadhani kiungo huyo anaweza kurejea uwanjani mwanzoni mwa mwezi ujao. 
Wenger amesema kwa mujibu wa madaktari Ramsey anaweza kuwa nje kwa muda wa wiki tatu mpaka nne hivyo yeye ameamua kuhesabu nne kabisa. 
Ramsey, 23 akiwa nje ya wiki hizo ina maana atakosa michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Chelsea, Hull City na Sunderland na pambano la ugenini la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Anderlecht.