STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

Vumbi Ligi Kuu England kutimka leo, Chelsea v Arsenal ni Sheeda kesho

http://img.eplmatches.com/2014/06/premier-league.jpghttps://infobase360.files.wordpress.com/2014/08/barclay2014-2015-teams.pngVUMBI la Ligi Kuu ya England inatarajiwa kuendelea kutimka tena leo kwa michezo sita tofauti, ambapo mabingwa watetezi Manchester City watakuwa ugenini kuvaana na Aston Villa, huku Liverpool ambayo imekuwa ikigawa takrima katika ligi hiyo watajiuliza nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion pale Anfiled.
Mechi  nyingine kwa mujibu wa ratiba hiyo kwa leo ni kwamba Hull City watakuwa nyumbani kuikaribisha Crystal Palace na Leicester City wataialika Burnley wakat Swansea City wataikaribisha Newcastle United.
Pambano jingine kwa siku ya leo ni kati ya Sunderland itakayokuwa nyumbani kuivaa Stoke City.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mipambano ya kukata na shoka wakati Arsenal itasafiri hadi Stanford Bridge kuvaana na wenyeji wao Chelsea ambao kwa miaka ya karibuni wakiwa chini ya Jose Mourinho wamekuwa wakiionea Ze Gunnerz.
Vijana wa Luis Van Gaal, Manchester United watakuwa uwanja wa Old Trafford kuikaribisha Everton katika pambano jingine 'tamu' kwa kesho huku Tottenham Hotspur watakuwa nyumbani kuwaalika Southampton.
Kadhalika kesho litashuhudiwa pambano kati ya West Ham United itakayoumana na QPR
Hii ndiyo ratiba kamili ya wikiendi hii;

Leo Jumamosi:
17:00 Hull vs Crystal Palace
17:00 Leicester vs Burnley
17:00 Liverpool vs West Brom
17:00 Sunderland vs Stoke
17:00 Swansea vs Newcastle
19:30 Aston Villa vs Man City

Kesho Jumapili:
14:00 Man United vs Everton
16:05 Chelsea vs Arsenal
16:05 Tottenham vs Southampton
18:15 West Ham vs QPR

No comments:

Post a Comment