STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

Tanzia:Ally Choki apata pigo, afiwa na mkewe Mama Shuu

Mama Shuu enzi aa uhai wake
[3.JPG]
Ally Choki aliyefiwa na mkewe. Pole sana kaka kwa msiba ulioupata Mungu akupe Subira katika kipindi hiki kigumu
MKURUGENZI wa bendi wa Extra Bongo na mmoja wa waimbaji nyota nchini wa muziki wa dansi, Ally Choki amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na Mkewe maarufu kama Mama Shuu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanamuziki wa Africana Stars, Twanga Pepeta, Rama Mhoza 'Pentagone', mke wa Choki alifariki usiku wa kuamkia leo na taratibu za mazishi zinaendelea jijini Dar es salaam.
MICHARAZO inatoa pole kwa Choki, ndugu, jamaa na wadau wote wa muziki wa msiba huo ila ikiwakumbusha kuwa Sisi Sote tu waja wa Allah (SW) na Kwake Tutarejea. Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mama Shuu Mahali Pema Pepon. Ameen

No comments:

Post a Comment