STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

Wakijiandaa kuivaa JKT kesho, Jaja aweke rekodi Yanga 2014-2015

http://4.bp.blogspot.com/-xfO2SabjS0Y/VAc9Y1RA1HI/AAAAAAABO5E/Ch9RNwWds2k/s1600/jaja.jpg
Jaja
LICHA ya kwamba huenda asiwepo kwenye kikosi cha kesho kitakachowavaa JKT Ruvu kutokana na kudaiwa kuwa majeruhi, Mshambuliaji mpya wa Yanga kutoka Brazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ ameweka rekodi katika kikosi cha timu hiyo kwa msimu wa 2014-2015.
Jaja, aliyekuwa gumzo baada ya kufunga mabao mawili yaliyoizamisha Azam kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, likiwamo la pili ambalo limezoelekea kuonekana kwenye 'kideo'. ndiye mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuonyeshwa kadi ya njano na kukosa penalti msimu huu.
Mbrazil huyo anayedaiwa kukingiwa kifua na kocha Marcio Maximo, licha ya kuonekana mzito dimbani, alipewa kadi ya njano katika pambano la kwanza la Yanga dhidi ya Mtibwa kabla ya kuja kukosa penati wakati timu yao ikizama kwa mabao 2-0 uwanja wa Jamhuri Morogoro.

No comments:

Post a Comment