STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

Klabu zatishia kuigomea Ligi Kuu, kumng'oa Malinzi madarakani

http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/NDUMBAROZ7067-11.jpg
Damas Ndumbaro (kulia)
http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2013/11/malinzi1.jpg
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
SIKU moja  baada ya Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal  Malinzi kutangaza kuvibana vilabu vya ligi kuu kuchangia mapato yao kwa asilimia tano ili kuchangia miradi mbalimbali iliyo anzishwa na shirikisho la soka nchini, vilabu vya ligi kuu kupitia kwa mwanasheria wao Dr Damas Ndumbaru vimetishia kugomea kuendelea na ligi kuu.
Rais wa TFF, Malinzi kusisitiza lazima klabu zikatwe asilimia 5 kwenye fedha zao za udhamini wa Vodacom na Azam TV, zenyewe zimejibu mapigo.

Hata hivyo kupitia mwanasheria wao, klabu 14 za Ligi Kuu Bara, zimesisitiza mambo haya ya msingi, kuwa hazitavaa jezi zenye nembo ya wadhamini hao, kupinga kukatwa fedha zao.
Pili, zitaitisha mkutano wa dharura wa kamati ya utendaji kupiga kura ya kutokuwa na imani na Malinzi ambayo itamuondoa madarakani.
Mwanasheria maarufu nchini Dk Damas Daniel Ndumbaro amesema kwa mujibu wa katiba ya TFF, klabu hizo 14 ambazo ni mwanachama zinaruhusiwa kufanya hivyo.
“Hilo linaruhusiwa kwa mujibu wa ibara ya 25 (ibara ndogo ya TFF) kama wanachama tuitishe mkutano mkuu maalum.
“Katika mkutano huo tutapiga kura za kutokuwa na imani na Malinzi, kinachotakiwa ni kufikia theluthi mbili tu, yaani kura mia moja,” alisema Ndumbaro.
TFF ina wanachama 150, hivyo kama utaitishwa na kufikisha theluthi hizo mbili za kura ya kutokuwa na imani, Malinzi atakuwa ameng’oka madarakani.
Uamuzi wa klabu hizo kupinga umetokana na kwamba TFF kupitia sekretarieti yake iliyodai ni kwa mujibu wa kamati ya utendaji, imepitisha uamuzi wa kutaka ipewe asilimia 5 ya fedha za udhamini za klabu.
Jambo hilo halijafanyika sehemu yoyote duniani, pia kumekuwa hakuna ufafanuzi mzuri wa kutosha zaidi ya Malinzi kusisitiza kuwa ni lazima fedha hizo zikatwe.
Kiutaratibu inaonyesha klabu ndiyo zinazotangaza wadhamini hao, ndiyo zenye haki ya fedha hizo.
Lakini katika mapato ya milangoni, fedha zimekuwa zikikatwa fedha ambazo zinakwenda kwenye mfuko wa maendeleo ya soka nchini ambao sasa TFF unataka ukate na fedha za wadhamini.

Mbeya City na Mtibwa Sugar, zimetishia kuifikisha TFF mahakamani kama itaendelea kulazimisha uamuzi huo.

No comments:

Post a Comment