STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 20, 2013

Redd's Miss Bagamoyo kusaka vipaji J'5

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiTkXB_wLHpzsqQ905DvOw1PsYZJNU3Ck8iLgJFN1ZnUWcUQqOMWOIhW8at7WeZnDFjQvkb5NMknVzRipc0RkeX1K4Qgw4_o_DKoNowHCFhbIz1EMhJtfFwNdhQty1eZMVrGlXQv3L2xo/s1600/ROSE+MIS+REDDS.jpg
Redd's Miss Bagamoyo wa mwaka jana.

WAREMBO 10 waliojitokeza kushiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Redd's Miss Bagamoyo 2013 wanatarajiwa kuonyeshana kazi kwenye onyesho maalum la kusaka vipaji baina yao litakalofanyika siku ya Jumatano jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, Awetu Salim ambaye ni Mkurugenzi wa Asilia Decorations, aliiambia MICHARAZO kuwa, shindano hlo la kusaka vipaji litafanyika kwenye ukumbi wa Mikocheni Center (MRC) ambapo burudani mbalimbali zitakuwepo kusindikiza mchuano huyo.
Awetu alisema onyesho hilo linafanyika siku mbili kabla ya warembo hao wanaoendelea na mazoezi yao mjini Bagamoyo hawajakutana kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo mkali baina yao siku ya Ijumaa kwenye shindano la Redd's Miss bagamopyo litalakalofanyika kwenye ukumbi wa TaSUBA.
"Katika kuwaweka sawa warembo wetu, Jumatano watachuana kusaka mwenye kipaji onyesho litakalofanyika Mbezi, kabla ya Ijumaa kuonyeshana katika katika shindano la kumsaka kisura wa Bagamoyo kwa 2013," alisema Awetu.
Awetu alisema warembo wote 10 watakaochuana kwenye shindano hilo na lile la vipaji wapo fiti na kila mmoja anajitamba kwamba atawafunika wenzake.
Mratibu huyo aliwataja baadhi ya warembo hao watakaochuana ni Juliet Jeremiah, Rose Anthony, Lilian Joseph, Elizabeth Plet, Sulehya Abdi na Fatuma Hamis.

Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kikanda Wakutana Mbeya kuteta

Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , amesema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani.
Mwenyekiti wa Mkutano  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile amesema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo.
Baadhi ya maafisa wa jeshi hila la Polisi wakiwa makini kusikiliza mwenyekiti wao katika kikao hicho
Baadhi ya makamanda wa polisi wakiwa maetulia kwa umakini kumsikiliza mwenyekiti wa kikao hicho
Picha ya pamoja


MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu  ikiwa na kuweka mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.
Mkutano  huo unafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya usalama na uhalifu wa maeneo katika  Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya  .
Akizungumzia mikakati hiyo, Mwenyekiti wa Mkutano  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo.
Amesema Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu moja hivyo mkutano huu utasaidia kwa wajumbe kubadilishana  na kupeana uzoefu wa kazi,’alisema
Aidha, amefafanua kuwa  jeshi la polisi hivi sasa kupitia baadhi ya askari   limekuwa likikumbwa na matukio ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali za uhalifu.
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali barabarani.
Amesema mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia njia nyingi kufanya uhalifu na kukimbilia mikoa ya jirani  hivyo  mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda pamoja na wakuu wa upelezi utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao uliopo
Mkutano huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza kufanyika Mkoani Iringa na  wapili ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio mapya.
Na Mbeya yetu 

Iringa Mjini ni Shangwe Tupu baada Mhe Msigwa kuachiwa



Add caption

Mhe Msigwa akiwa amebebwa juu na wafuasi wake


SAKATA la vurugu  za machinga na polisi mjini Iringa limechukua  sura  mpya  baada  ya  jeshi la  polisi mkoa wa Iringa  kumfikisha mahakamani mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa pamoja na  watuhumiwa wengine zaidi ya 70

Huku mahakama   hiyo  ikitoa masharti nafuu ya dhamana kwa  watuhumiwa hao na  kuwaonya  kutofanya  kosa kwa  kipindi  chote  cha kesi  hiyo inapoendelea  kusikilizwa .

Watuhumiwa hao  walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya  leo  majira ya saa 8 mchana  huku wakiwa  chini ya ulinzi mkali  wa askari  wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na msafara  wa magari zaidi ya matatu  likiwemo  gari ya maji ya  kuwasha .

Mbali ya mbunge Msigwa  kupanda gari ndogo  ya  wazi ya  polisi pamoja na  watuhumiwa  wawili wanawake  waliokamatwa katika  vurugu  hizo bado  watuhumiwa  wengine 74  walitumia usafiri wa karandinga la polisi .

 Mbele  ya mahakama  hiyo  wakili  wa serikali  Adolph Maganda alisema  kuwa  watuhumiwa hao kwa pamoja  wanatuhumiwa  kwa kosa kwa makosa matatu  likiwemo la kufanya kushiriki  mkutano na kufanya   vurugu ,uchechezi na kuharibu mali kinyume na sheria 

Huku mbunge  akisomewa mashitaka mawili likiwemo  kushawishi   na kufanya mkutano bila  kibali  .

Watuhumiwa  wote  wamekana  mashitaka  dhidi yao  huku  wakili  wa  serikali akidai  kuwa hana pingamizi na dhamana kwa  watuhumiwa hao wote  hata  hivyo wote   wamekana  mashitaka  yote yaliyotolewa  dhidi  yao .

Hata  hivyo makimu anayesikiliza kesi  hiyo alisema kuwa dhamana kwa  washitakiwa  wote  ipo  wazi  kwa kila mmoja kuwa mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na kusaini hati ya dhamana  ya Tsh milioni moja .

 Hadi majira ya  saa 10 jioni mahakama  hiyo  ilikuwa ikiendelea na mchakato  wa  kupitia barua  za dhamana kwa  wadhamini  huku  mbunge akiwa  wa kwanza kudhaminiwa ,mbali ya  mbunge  watuhumiwa kati ya 74  waliokuwa  bado kupata  wadhamnini  ni  watuhumiwa  sita pekee.

 Katibu  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima alisema  kuwa  mchakato  wa  kuwadhamini  watuhumiwa  wote  waliosalia unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa  watuhumiwa  wote kudhaminiwa .

Hadi  majira  haya  ya saa 10 .40  mbunge  msigwa na  wengine  wameachiwa  huku  watuhumiwa 26 kati ya 74  wamekosa  dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa  tena tarehe 3 /6/2012
Wakati  huo  huo  wananachi  waliofika  mahakamani hapo  kushuhudia mbunge  wao akifikishwa mahakamani  wamempongeza mkuu  wa  kikosi cha kutuliza ghasia mkoa  wa Iringa (FFU) Said Abdulah Mnunka  kwa kusimamia amani na utulivu katika  eneo hilo la mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza  kupambana na machinga  pasipo kumwaga damu kwa  siku ya  jana wakati  wa vurugu  hizo

WAKAZI MBEYA WAGOMBEA MAFUTA BAADA YA LORI KUPINDUKA

 WAKAZI WA MLIMA NYOKA MKOANI MBEYA WAKIWA NA PILIKA KUELEKEA KUCHOTA MAFUTA BAADA YA GARI HILO KUPINDUKA.
 SHUHUDIA WAKAZI WA MLIMA NYOKA WAKIWA WANAGOMBANIA MAFUTA
 GARI LA KAMPUNI YA LAKE OIL BAADA YA KUPINDUKA
 KILA MKAZI YUPO BIZE NA MAFUTA
 PICHA NA MBEYA YETU

Maskini Madame Rita, ajali yamuacha hoi!


KILICHOMPATA Madame Rita kinasikitisha! Ndivyo unavyoweza kusema ukibahatika kumuona the big boss wa Benchmark Production inayoratibu Shindano la Bongo Star Search, Rita Poulsen ‘Madam’ anayetembelea magongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuwa kimya muda mrefu ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru kwa kutoka salama.

 Kabla ya ajali

Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo aliipata katikati ya Jiji la Dar  na kusababisha kuvunjika kwa kifundo ‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya hospitali kumuwekea ‘hogo’.
“Namshukuru Mungu kwanza kwa kunitoa salama katika ile ajali japokuwa sijapona vizuri,” alisema Madam Rita.

Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza kuwa alipopata ajali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Mifupa ya Moi lakini hali ilipokuwa kuwa mbaya alihamia katika hospitali moja ya Kichina ambapo kwa sasa amepata nafuu.

Polisi wanaswa wakisafirisha bhangi kwenye gari la bosi wao

Picha haihusiani na stori hapo chini
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwakamata askari 16 wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya magendo, askari wengine wawili wa jeshi hilo wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa na shehena kubwa ya bangi wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.
Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.
Akithibitisha kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema askari hao walikuwa wakipeleka bangi hiyo Wilaya ya Rombo kwa mfanyabiashra mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake.
Kamanda Boaz aliwataja askari waliokamatwa na wanashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi katika mji mdogo wa Himo kuwa ni F.1734 Koplo Edward (dereva) wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Arusha na G.2434 Konstebo George wa kituo cha polisi Ngarenanyuki Wilaya ya Arumeru.
Alibainisha kuwa kukamatwa kwa askari hao kunatokana na operesheni ya kukabiliana na dawa za kulevya inayofanywa na polisi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Alisema operesheni hiyo imefanyika kikamilifu katika Mkoa wa Arusha uliokuwa ukitumika kupitishia bidhaa hiyo, na sasa wahusika wameamua kuutumia Mkoa wa Kilimanjaro.
“Baada ya kuwahoji askari wale, walidai kuwa walikodishwa na mfanyabiashara huyo kuipeleka bangi hiyo wilayani Rombo tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini Kenya ambako inaaminika kuna soko kubwa,” alisema.
Kamanda Boaz alisema hivi sasa polisi wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha wanafanya uchunguzi kubaini mtandao wa askari hao unaojihusisha na vitendo haramu.
Aliongeza kuwa hatua inayofuata kwa askari hao ni kufunguliwa mashtaka ya kijeshi na iwapo watakutwa na hatia watafukuzwa kazi kisha watafikishwa katika mahakama za kiraia.
Kamanda Boaz alibainisha kuwa kwa kawaida askari wanapotoka mkoa mmoja kwenda mwingine hupatiwa kibali maalumu cha kusafiria (Movement Order).
Alisema kibali hicho husaini kila mkoa ambao askari husika hupita, lakini waliokamatwa na bangi hawakuwa nacho.
Kamanda Boaz alibanisha kuwa kwa hali ilivyo askari hao waliondoka na gari la mkuu wa FFU bila kumpa taarifa wala kupata kibali chake.
Tanzania Daima limedokezwa kuwa askari hao wamekuwa wakisafirisha bangi hiyo mara kwa mara kupitia mji huo wa Himo bila kukamatwa kutokana na gari lao kuwa na namba za kijeshi, hivyo kuwa vigumu kwa askari wenzao kuwatilia shaka.
Taarifa zaidi zimedai kuwa kukamatwa kwa askari hao kulitokana na gari lao kupata hitilafu katika eneo hilo la Kilemapofu, na ndipo askari wa doria walipofika kwa lengo la kutoa msaada kwa wenzao, lakini ghafla walisikia harufu ya bangi.
Mtoa taarifa aliyezungumza kwa sharti la kutotaka jina lake litajwe, alisema baada ya askari hao kusikia harufu ya bangi waliwaarifu viongozi wao waliowaamrisha walifanyie upekuzi gari hilo sambamba na kuwaweka chini ya ulinzi askari wote waliokuwamo.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa katika upekuzi huo walibaini uwepo wa magunia 18 ya bangi yaliyolengwa kupelekwa nchini Kenya.
Kilibainisha kuwa baada askari hao kukamatwa, mmoja wao alisikika akiongea na mtu aliyemuita bosi kumuarifu kukamatwa kwao.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa bosi aliyearifiwa tukio hilo alihoji imekuwaje wakakamatwa kizembe namna hiyo.
Kilidokeza kuwa bosi huyo alimhoji aliyempigia simu kuwa wamebaki na shilingi ngapi ili wawape rushwa polisi waliowakamata.
“Bosi aliambiwa kuna laki tano, naye akawaambia wawape fedha hizo zote, lakini kwa bahati mbaya hawakufanikiwa,” kilisema chanzo chetu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, hakukiri wala kukanusha kuwapo kwa taarifa za kukamatwa kwa askari wake.
Tanzania Daima lilitaka kujua Jeshi la Polisi mkoani Arusha limechukua hatua gani dhidi ya askari hao ambapo kamanda Sabas alisema hayupo katika nafasi nzuri ya kulizungumzia jambo hilo kwa kuwa yupo hospitalini.

Credit:Tanzania Daima

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MSIGWA KWA DHAMANA


WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge  wa  Jimbo  hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa  wanafanyiwa  utaratibu  wa  dhamana  baada ya mahakama  kukubali  kupewa  dhamana. 
 Awali watuhumiwa  walisomewa mashitaka matatu  huku mbunge  akisomewa shitaka la  kushawishi  watuhumiwa hao kufanya  vurugu.
  
Watuhumiwa  wote  wamekana mashitaka  dhidi yao na kwa  sasa utaratibu  wa dhamana  unafanyika mbele  ya mahakama ya  hakimu mkazi  wa wilaya ya  Iringa, Mheshimiwa  Godfrey Isaya.




Mashitaka waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo ni kushawishi kufanya vurugu, huku  wengine  wote  makosa yao yakiwa ni kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni  kufanya  vurugu.