STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 15, 2014

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa hii hapa


KLABU ya Manchester City imepangwa kucheza na Barcelona katika hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ratiba iliyopangwa leo jijini Nyon, Ufaransa. 
Timu hizo zilikutana pia katika hatua hiyo msimu uliopita ambapo Barcelona waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 
Timu zingine ambazo zilikutana msimu uliopita katika hatua hiyo ni pamoja na Paris Saint-Germain ambao watakwaana tena na Chelsea msimu huu. 
Wengine ni mabingwa watetezi Real Madrid ambao watakwaana na Schalke wakati mshindi wa pili msimu uliopita Atletico Madrid wao wataivaa Bayer Leverkusen. 
Mabingwa wa Serie A Juventus wao watawakaribisha Borussia Dortmund huku mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakicheza na Shakhtar Donetski, Arsenal wenyewe watacheza na Monaco na Porto watakwaana na FC Basel. 
Timu ambazo zilimaliza katika nafasi ya pili katika hatua ya makundi zitacheza mechi zao za kwanza nyumbani kati ya Februari 17/18 na 24/25 huku zile za marudiano zikitarajiwa kuchezwa kati ya Machi 10/11 na 17/18.

Liverpool wapewa Waturuki, Ligi Ndogo ya Ulaya

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/Andre+Wisdom+BSC+Young+Boys+v+Liverpool+FC+DEcmweK_E8Sl.jpg 
KLABU ya Liverpool ambayo ilichemsha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepewa timu ya  Besiktas ya Uturuki katika hatua ya timu 32 bora ya michuano hiyo kwenye ratiba iliyopangwa leo. 
Timu zingine zilizoondoshwa katika michuano hiyo ni pamoja na Ajax Amsterdam ambao wamepangiwa kucheza na Legia Warsaw, Anderlecht wao wakipangwa na Dinamo Moscow huku Sporting Lisbon wao wakiwa wenyeji wa Wolfsburg. 
Katika mechi zingine zitazikutanisha timu za AS Roma dhidi ya Feyenoord, Inter Milan wao watacheza na Celtic, Tottenham Hotspurs dhidi ya Fiorentina wakati Athletic Bilbao wao watakuwa wenyeji wa Torino. 
Mechi za mkondo wa kwanza za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Februari 19 huku zile za marudian zikitarajiw akuchezwa Februari 26.

Breaking News! Amissi Tambwe atua Yanga

tambwe yanga
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa dakika chache zilizopita ni kwamba klabu ya Yanga imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Emerson Oliveira wa Brazil aliyetemwa kwa kukosa ITC.
Tambwe ametua Yanga ikiwa ni siku chache baada ya Mganda Hamis Kiiza kuachwa na klabu hiyo na kukimbilia URA ya Uganda baada ya Kpeh Seen Sherman wa Liberia kupewa kandarasi ya kuichezea timu hiyo.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
Yanga imekamilisha usajili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa leo na TFF.