STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 18, 2013

Manyika kuuza sura videoni

Manyika katika pozi za kisanii
KIPA wa zamani wa timu za Sigara, Mtibwa na Yanga, Manyika Peter, amesema video ya wimbo wake unaoendelea kutamba nchini uitwao  'Wololowololo' imekamilika na ataanza kusambazwa wiki hii.
Manyika, kocha wa makipa wa timu za taifa za vijana, aliiambia MICHARAZO kuwa, video hiyo itasambazwa wiki hii ili irushwe hewani na kuwapa burudani mashabiki wake ambao wamekuwa wakiiulizia.
Msanii huyo alisema video hiyo ilichelewa kukamilika kutokana na kutingwa na majukumu, ila anashukuru amefanikiwa kuimaliza na sasa kuwataka mashabiki wake wasubiri kuona 'Wololowololo' videoni.
"Ile video ya wimbo wangu wa 'Wololowololo' imekamilika na natarajia kuanza kuisambaza ili kutuliza kiu ya mashabiki wangu waliokuwa wakiiulizia tangu nilipotangaza kutaka kuitoa," alisema Manyika.
Wimbo huo wa 'Wololowololo' ambao ni wa kwanza kwa Manyika tangu alipotoa kazi yake ya mwisho mwaka 2007, umekuwa ukitamba katika vituo mbalimbnali vya redio nchini tangu alipoutoa mwaka jana.

Manyika katika kazi ya ukocha