STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 18, 2013

Fike, J-Plus sasa wanasa kwa Jamali

Fike Wilson akiwa na mkewe Irene Wambura
BINGWA wa zamani wa kutunisha misuli nchini, Fike Wilson 'Wild Cat', amevunja ukimya kwa kuibuka na filamu mpya iitwayo 'Jamali'.
Filamu ya Fike inakuja baada ya kupita miaka karibu miwili tangu msanii huyo alipofyatua kazi yake ya mwisho iitwayo 'Lost Dream'.
Fike alisema kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho kabla ya kuiachia mtaani filamu hiyo ambayo imewashirikisha wasanii kadhaa nyota.
"Nipo katika maandalizi ya kuiachia sokoni filamu yangu mpya iitwayo 'Jamali' ambayo ilikamilika tangu mwaka jana ila nilichelewa kuitoa,": alisema.
Fike alisema katika filamu hiyo ya 'Jamali', ameigiza na wasanii kadhaa wanaotamba nchini kama Jimmy Mponda 'J Plus', Ahmed Olotu 'Mzee Chillo', Mobby Mpambala na Irene Wambura 'Maurine'.
"Ni filamu tangu pengine kuliko kazi zangu zote za nyuma kama Power of Love, Lost Dream na nyingine, kutokana na wasanii walioshiriki katika filamu hiyo mpya ya Jamali," alisema Fike.
Fike alisema wakati akijiandaa kuiingiza mtaani filamu hiyo tayari ameshakamilisha kazi nyingine mpya ambayo hata hivyo aliomba isitajwe kwa sasa ili awashtukize mashabiki wake baadaye atakapoitoa.

 

No comments:

Post a Comment