STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 11, 2014

Tumebahatisha kuifunga Kagera Sugar-Ngassa


Mrisho Ngassa (kulia) akiwa na wachezaji wenzake Simon Msuva na Didier Kavumbagu wakishangilia bao lao la kwanza dhidi ya Kagera lililofungwa na Kavun\mbagu (kati)
WINGA hatari wa Yanga, Mrisho Ngasa ameimwagia sifa timu ya Kagera Sugar huku akiweka wazi kwamba timu yake imebahatisha kupata ushindi dhidi ya timu hiyo katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa juzi.
Ngasa aliyasema hayo katika mahojiano mara tu baada ya mechi hiyo raundi ya 24 waliyoshinda 2-1 huku akitoa pasi ya mwisho ya goli la kwanza lililofungwa na mshambuliaji Mganda Hamis Kiiza na kupika pia la pili lililopachikwa na straika Mrundi Didier Kavumbagu.
“Ilikuwa mechi ngumu sana, Kagera ni wazuri na walitawala mchezo hasa kipindi cha pili, ni bahati tu iliyotusaidia wasipate magoli mengi zaidi,” alisema Ngassa.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya hasa katika mechi zilizobaki ukizingatia bado hatujacheza dhidi ya Simba ambao mara nyingi wamekuwa wakitukamia sana.”
Ngasa, mchezaji wa zamani wa Kahama United, Kagera Sugar, Simba na Azam FC, alianza katika mechi ya juzi kabla ya kumpisha mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Hussein Javu katika dakika ya 63.
Winga huyo tegemeo katika kikosi cha Mholanzi Hans van der Pluijm cha Yanga, alifunga goli la kwanza katika ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera Oktoba 12 mwaka jana
NIPASHE

Wigan yaichimba mkwara Arsenal

MABINGWA watetezi wa Kombe la FA, Wigan Athletic wamesema hawatakuwa tayari kuona kombe hilo likitoweka mikononi mwao hususan watakapocheza mechi ya nusu fainali dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Wembley Jumamosi.
Wigan iliutwaa ubingwa huo msimu uliopita baada ya kuifunga Manchester City katika mechi ya fainali.
Hull City, ambayo haijawahi kufika nusu fainali, huku ikitinga hatua hiyo baada ya miaka 85 iliyopita, itacheza nusu fainali nyingine dhidi ya Sheffield United Jumapili.
Arsenal itavaana na watetezi hao wa FA wakiwa wanauguza kipigo cha aibu walichopewa na Everton katika pambano lao la mwisho la Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton waliowatambia kwa kuwalaza mabao 4-0