STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 11, 2014

Rooney katuponza kwa Bayern-MOyes

Wayne Rooney
KOCHA David Moyes amekiri kwamba alifanya makosa makubwa kumharakisha Wayne Rooney kurejea uwanjani katika kikosi cha Manchester United kilicholala 3-1 dhidi ya Bayern Munich katika mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya England, ambaye aliumia wiki iliyopita, alipasishwa kuchukua namba yake katika kikosi cha kwanza cha Man U, lakini hakuweza kuwasaidia Mashetani Wekundu wasikumbane na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Allianz Arena.
"Kuna wakati nilihisi kwamba anashindwa hata kupiga mpira lakini yeye ni mchezaji muhimu sana kwetu," Moyes aliwaambia waandishi wa habari. "Sikujiwa na fikra kwamba tumeshatoka mchezoni, daima niliamini kwamba tulikuwa na nafasi ya kusonga mbele.
"Ilipokuwa 2-1 tulihitaji kufunga moja ili tuwe 2-2, lakini mambo hayakutuendea vyema. Nadhani ilikuwa ni kukosa bahati kulikotufanya tukafungwa bao lile la tatu.”

No comments:

Post a Comment