STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 12, 2013

Bondia Afa ghafla mazoezini, ni 'Tembo Mtoto'

BONDIA Yohana Mathayo 'Tembo Mtoto' amefariki dunia jioni ya jana akiwa mazoezini kwake eneo la Kigogo Mburahati Dar es Salaam.
Kifo hicho kilimkuta ghafla wakati akifanya mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa uliopangwa kufanyika hivi karibuni.
Taarifa za kifo cha bondia huyo aliyekuwa akizidi kupanda chati nchini miongoni mwa mabondia vijana, zilitolewa na kocha wake Kwame Mkuruma, aliyedai mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Manzese na huenda akasafilishwa kwenda kuzikiwa kwao mkoa wa Tanga.
Mungu ametoa na Mungu ndiye aliyetwaa. Roho yake ilale mahali pema ila Yohana Mathayo 'Tembo Mtoto' utakumbukwa daima na wadau wenzako wa ngumi umetangulia nasi tu nyuma yako.
Bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza michezo 7 ya ngumi za kulipwa akiwa ameshinda mara 4 na kupigwa mara moja na  droo mara mbili.  Marehemu huyo enzi za uhai wake  alijiunga na ngumi za kulipwa mwaka 2011 ambapo mchezo wake wa kwanza kacheza na Seba Temba wa Morogoro ambapo alitoa nae droo na mchezo wake wa mwisho kucheza ni Agosti 9 mwaka huu ambapo alishinda kwa TKO ya raundi ya pili dhidi ya Shujaa Keakea.

SHIWATA YAANZA KUKABIDHI NYUMBA KWA WANACHAMA WAKE< YATOA SHUKRANI MKURANGA

Mchezaji na Kepteni wa zamani wa Timu ya  Taifa Stars, Jella Mtagwa (kushoto) akipokea cheti cha nyumba aliyokabidhiwa na SHIWATA na eneo la robo ekari ambalo anatarajia kujenga nyumba kubwa
Mwanachama huyu wa SHIWATA kulia ameamua kujijengea nyumba yake pole pole hapa akikabidhiwa cheti chake
Mmoja wa wanachama wa SHIWATA, Emmanuel Ntumbii na mkewe wakipokea cheti cha kumilikishwa nyumba yake akishuhudiwa na wanachama wenzake.
Mwandishi wa Habari, Josephine Joseph akionesha cheti alichokabidhiwa na SHIWATA mbele ya nyumba yake katika sherehe ya kukabidhi nyumba za wasanii,Mkuranga.
Mkuu wa wilaya mstaafu, Bw. Henry Clemence akizungumza katika sherehe ya kukabidhi nyumba 38 za wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) katika kijiji cha Mwanzega, Mkuanga.


BAADA ya kukabidhi nyumba kwa wanachama 38, SHIWATA inatoa shukurani kwa viongozi wa kijiji cha Mwanzega Kata ya Mbezi, Tarafa ya Shungubweni,wanavijiji pamoja na viongozi wa wilaya ya Mkuranga akiwepo Mkuu wa wilaya, Mercy Silla kwa kufanisha sherehe ya ugawaji nyumba na vyeti.

Wanachama zaidi ya 70 wamejitokeza kuchangia ujenzi wa nyumba ili wakabidhiwe Desemba 28, 2013 katika sherehe nyingine ya kukabidhi nyumba ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambao waliomba udhuru sherehe ya awali.

SHIWATA inawahimiza wanachama wake wasifanye mzaha na kudharau mpango wa kuchangia ujenzi kwani utawanufaish na kuwamilikisha nyumba zao wenyewe kwa gharama nafuu.

Mtandao wa wasanii unatoa bure viwanja baada ya mwanachama kulipa gharama zote za kujiunga uanachama ambaye ataruhusiwa kujenga mwenyewe au kuchangia ujenzi wa nyumba kwa pamoja.

SHIWATA  inakusudia kujenga Shule ya Msingi, Sekondari na vyuo vya fani za utamaduni, Uandishi wa Habari na michezo mbalimbali ikiwemo soka kwa malengo ya kupata wachezaji bora ambao watanyanyua viwango vya michezo hiyo ndani na nje ya nchi ili kuwapatia vipato zaidi.

Pia inawahitaji wasanii, wanamichezo, wanahabari wenye vipaji na elimu ya juu katika fani zao wajiunge na SHIWATA ili waweze kuwa walimu wa sanaa na michezo mbalimbali ambayo itaanza kufundishwa kutoka ngazi ya Shule ya Msingi, Sekondari hadi Chuo katika kijiji cha Mwanzega.

Shule ya msingi itakapoanzishwa itatoa kipaumbele kwa masomo ya sanaa na michezo ili kupata wasanii na wanamichezo bora katika taifa letu.
SHIWATA pia inatarajia kujenga viwanja vya michezo, kumbi za Maonesho na Studio za kurekodia muziki na filamu zenye ubora ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi.