STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 20, 2014

Liverpool majanga! Yazamishwa 3-1 na West Ham

Winston Reid (r)
West Ham wakiiadhibu Liverpool

Winston Reid
Bao la kwanza la West Ham likitumbukizwa wavuni na Winston Reid kwa kichwa
Diafro Sakho (second on the left)
West Ham wakishangilia bao lao la pili lililofungwa na Diafro Sakho
Mario Balotelli and Adrian
Balotelli akikoromewa na kipa wa West Ham
Raheem Sterling (l)
Sterling akipongezwa baada ya kufunga bao la kufutia machozi la Liverpool
TIMU ya Liverpool wameendelea kuwa urojo katika Ligi Kuu ya England baada ya mudfa mfupi uliopita kunyukwa mabao 3-1 na West Ham United katika pambano kali lililochezwa Upton Park.
Liverpool ambayo wiki iliyopita ilinyukwa nyumbani na Aston Villa kwa bao 1-0, ilishindwa kupata dawa ya kurejea kwenye makali yake ikiwa haina Luis Suarez baada ya kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1.
Winston Reid aliwaandikia wenyeji bao dakika ya pili tu ya mchezo akimalizia kazi ya Tomkins kabla ya Diafro Sakho kuongeza la pili dakika tano baadaye na kuwapa presha vijana wa Branden Rodgers kuepuka kipigo ugenini.
Juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 26 wakati Raheem Starling kufunga bao la pekee la timu yake, hata dakika za lala salama wenyeji waliandika bao la tatu lililowafanya Liverpool iliyotoka kupata ushindi wa mabao 2-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kushindwa kuepuka kipigo hicho kwa West Ham baada ya  Morgan Amalfitano kusukumua mpira wavuni akimalizia kazi nzuri ya Stewart Downing.

Al Ahly yaifyatua Coton Sport kwao, Sewe, Leopards 0-0

http://english.ahram.org.eg/Media/News/2014/9/20/2014-635468104658720940-872.jpg
Al Ahly
WALIOKUWA mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly ya Misri imeanza vyema mechi yake ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuizabua Coton Sport ugenini kwa  bao 1-0.
Bao pekee lililowazamisha wenyeji mjini Goroua Cameroon liliwekwa kimiani na  Waleed Soliman dakika ya 72. Timu hizi zitarudiana wiki ijayo kujua itakayotinga Fainali ya michuano hiyo.
Katika mechi nyingine ya Kombe hilo timu za Sewe Sport ya Ivory Coast na AC Leopards ya Kongo zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu.

Arsenal yaua ugenini, Welbeck atisha, Cisse aikoa Newcastle, Wanyama aizamisha Swansea akiangusha chozi uwanjani

Arsenal striker Danny Welbeck scores his first goal for the club
Alan Pardew
Kocha Allan Pardew akionyeshwa vipeperushi vya kutaka atimuliwe Newcastle kanbla ya Cisse kumuokoa kwa kufunga mabao mawili na kuambulia sare nyumbani
Papiss Cisse celebrates his second goal
Cisse akishangilia mabao yake jioni ya leo
Victor Wanyama (centre) celebrates his goal at the Liberty Stadium
Victor Wanyama akipongezqwa na wenzaake baada ya kuifungia Southampton bao pekee lililowapa ushindi ugenini dhidi ya Swansea City
ARSENAL wakiwa katika kiwango kizuri kabisa na kusahau kichapo chao cha Ligi ya Mabingwa Ulaya wameisambaratisha Aston Villa nyumbani kwao kwa kuwalaza mabao 3-0, huku Danny Welbeck akifunga moja ya mabao hayo.
Welbeck ambaye alikosa nafasi nyingi za kufungwa wakati Ze Gunners wakifa 2-0 nchini Ujerumani mbele ya Borussia Dortmund, alifunga bao la pili akimalizia pasi ya Mesut Ozil ambaye alitangulia kufunga bao la kwanza katika dakika ya 32.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa toka Manchester United ndiye aliyemtengenezea bao hilo Ozil kabla na yeye kumtengenezea dakika mbili baadaye na kuifanya Arsenal kuwa mbele kwa mabao mawili.
Bao la tatu na la ushindi la vijana wa Arsene Wenger lilitokana na kijifunga kwa mchezaji wa Aston Villa, Ali Cissokho dakika ya 36.
Katika mechi nyingine za Ligi ya Engalnd, QPR ikiwa nyumbani ililazimisha sare ya mabao 2-2 na  Stoke City, sawa  na ilivyokuwa kwa Newcastle United iliyosubiri mtokea benchi Pappis Demba Cisse kufunga mabao mawili na kuepuka kipigi cha nyumbani dhidi ya Hull City, huku mashabiki wa Newcastle wakibeba vipeperushi vikitaka kocha Allan Pardew atimuliwe
Burnley ikiwa nyumbani ililazimishwa suluhu na Sunderland na Swansea ikijikuta ikipokea kipigo cha pili mfululizo baada ya kufungwa na Southampton ikiwa ni wiki moja tangu Chelsea walipowatoa nishai.
Bao pekee lililoizamisha Swansea iliyotoka kunyukwa mabao 4-2 liliwekwa kimiani na Mkenya Victor Wanyama dakia ya 80 huku nyota wa Swanseas Winfried Bony akilimwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi za njano mbili katika pambano hilo.
Ushindi huo umeipaleka Southampton hadi kwenye nafasi ya pili nyuma ya Chelsea itakayoshuka dimbani kesho kuwakabili Manchester City uwanja wa ugenini.

Real Madrid 'yachinja' mtu 8 ugenini La Liga

Real Madrid
James Bond akishangilia moja ya mabao ya Real Madrid
REAL Madrid wamezidnuka kwenye Ligi Kuu ya Hispania baada ya kupata ushindi mnono ugenini wa mabao 8-2  dhidi ya Deportivo la Coruna.
Hat trick ya Cristiano Ronaldo na mabao mawili mawili toka kwa Gareth Bale na Javier Harnandez 'Chicharito na jingine la James Rodgriuez yalitosha kuwapa ushindi huo Madrid dhidi ya wenyeji wao.
Ronaldo alianza kufunga bao dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya Arbeloa kabla ya James Bond kufunga la pili dakika ya 36 akimalizia pande la Karim Benzema na dakika nne kabla ya mapumziko Ronaldo alirudi tena nyavuni kwa kufunga bao la tatu kwa pasi ya Benzema.
Kipindi cha pili ndicho kilichokuwa kiama kwa wenyeji ambao licha ya kupata bao la kujifutia machozi lililofungwa dakika ya 51 na Medunjanin kwa mkwaju wa penti haikusaidia kitu kwani Bale alifunga bao la nne dakika ya 66 na kuongeza jingine dakika nane baadaye.
Ronaldo alitimiza hat trick yake dakika ya 78 kabla ya Toche wa Deportivo kufunga bao la pili dakika ya 84 na mtokea benchi Chicharito kufunga mabao mawili ya haraka haraka dakika za 88 na 90 na kuifanya vijana wa Carlo Ancelont kuvuna ushindi wa mabao 8-2.

Yanga domo tupu yafa Moro, Azam yaua, Ruvu yalala, Ndanda dah!

Jaja hakufua dafu kwa vijana wa Mtibwa kwani alikosa penati

Watetezi Azam walioanza kwa kishindo kwa kuilaza Polisi Moro
Yanga iliyokufa Morogoro na Jaja wao
JKT Ruvu walioanza kwa suluhu dhidi ya Mbeya City
Prisons walioanza kwa ushindi wa mabao 2-0 ugenini mbele ya Ruvu Shooting
IMG-20140920-WA0053
Mbeya City
MSHAMBULIAJI Didier Kavumbagu ameifungia Azam mabao mawili na kuwasaidia mabingwa watetezi hao kuanza vyema Ligi Kuu Tanzania Bara, huku timu yake ya zamani, Yanga ikifa Morogoro kwa mabao 2-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.
Kavumbagu aliyekuwa mfungaji tegemeo wa Yanga kwa misimu miwili akiwa na kikosi hicho alifunga mabao yake katika dakika ya 14 na 90 wakati Azam wakiizamisha Polisi Morogoro kwa mabao 3-1 katika mechi iliyochezwa uwanja wa Chamazi.
Bao jingine la watetezi hao waliotoka kunyukwa mabao 3-0 na Yanga kwenye mechi ya Nago ya Jamii liliwekwa kimiani na nahodha wa zamani wa Azam, Aggrey Morris dakika ya 23 wakati Polisi walipata bao lao la kufutia machozi dakika ya 60.
Katika mechi nyingine iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa nchini iliyochezwa uwanja wa jamhuri, Morogoro, Yanga ilishindwa kutamba mbele ya Mtibwa Sugar kwa kukandikwa mabao 2-0, huku nyota wake mpya, Jaja akikosa penati na mabo mawili ya Yanga yakikataliwa na mwamuzi kwa madai wafungaji Simon Msuva na Mrisho Ngassa wameotea.
Mussa Hassan Mgosi alianza kuitia aibu Yanga kwa kufunga bao la kuongoza dakika ya 16 kabla ya Ame Ali kuongeza bao la pili dakika ya 82 na kuifanya Yanga kushindwa kuamini kama kwa miaka minne mfululizo wameshindwa kupata ushindi kwenye dimba la Jamhuri mbele ya Mtibwa inayonolewa na nahodha wa zamani wa Stars Mecky Mexime.
Mwamuzi Dominick Nyamisana wa Dodoma, alitoa adhabu ya penati kwa Yanga dakika ya 46, lakini Genilson Santana Jaja alikosa baada ya mkwaju wake kupanguliwa na kipa wa zamani wa Yanga, Said Mohammed.
Mwamuzi huyo aliyakataa mabao mawili ya Yanga katika dakika ya 47 na 49 kwa madai washambuliaji wa Yanga Simon Msuva aliyetokea benchi na Ngassa kuotea.
Katika mechi nyingine Mbeya City na JKT Ruvu zimetoshana nguvu kwa kutoka suluhu, huku maafande wa Ruvu Shooting wakifa nyumbani kwao Mlandizi kwa mabao 2-0, huku Ndanda Fc ikianza ligi kwa kishindo kwa kuilaza wageni wenzao Stand United kwa mabao 4-1 mjini Shinyanga.
Nayo Mgambo ilianza vema ligi hiyo kwa kupata ushindi mwembamba nyumbani dhidi ya Kagera Sugar baada ya kuwazamisha wakata miwa hao bao 1-0. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na ramadhani Pela na kuifanya Mgambo kuanza tofauti iliyovyokuwa msimu uliopita ilipopigana kuepuka kushuka daraja.

HIVI NDIVYO VUMBI LA LIGI TANO ZA ULAYA LITAKAVYOTIMKA

http://hd.wallpaperswide.com/thumbs/barclays_premier_league_2014_2015-t2.jpghttp://luckybardc.com/files/Soccer-LuckyBar-v2-2013.jpg
LIGI tano zenye mvuto barani Ulaya inatarajiwa kutimka vumbi leo na MICHARAZO inakuletea baadahi ya ratiba zake kwa wikiendi hii na muda wa kurushwa kwa mechi zenye mvuto kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya EPL:
QPR            v Stoke        (8:45) 
Aston Villa    v Arsenal    (11:00) 
Burnley        v Sunderland
Newcastle    v Hull City
Swansea        v Southampton
West Ham        v Liverpool    (1:30)
 
La Liga LEO:
Deportivo    v Real Madrid    (11:00) 
Athletic        v Granada CF
Atletico        v Celta Vigo
Espanyol        v Malaga

Seria A LEO:
Cesena        v Empoli
AC Milan        v Juventus    (3:45)

Bundesliga LEO:  
FC Augsburg    v Werder Bremen
Hamburg SV    v Bayern Munich
Paderborn    v Hanover 96
Schalke 04    v Frankfurt
Stuttgart    v Hoffenheim
Mainz        v Dortmund

Ligue 1 LEO:

Marseille    v Stade Rennes
FC Lorient    v Stade Reims
Metz            v Bastia
Nantes        v Nice
Toulouse        v Caen
Reuters

Kocha Liverpool ajipa matumaini juu ya kikosi chake

http://assets.kompas.com/data/photo/2014/08/31/2107275000-DV1855065780x390.jpgKOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers ametamba kwa kusema kuwa, Liverpool haihitaji fomula maalumu kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Uingereza na wachezaji wake wapya wameanza kuzoea maisha klabuni Anfield.
Baada ya kuvuka matarajio msimu uliopita na kushika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City, Liverpool imeanza kwa kusuasua msimu huu, ikifungwa mechi mbili kati ya nne za ligi kuu.
Lakini ikiwa ilisajili wachezaji wengi katika dirisha lililopita, Rodgers hadhani kama itachukua muda mrefu kabla ya kikosi chake kuzoeana na kuanza kupanda kwenye msimamo wa ligi.
"Siku zote tutaangalia namna tofauti tofauti za kushinda mechi. Hakuna fomula moja ya uhakika, ni kufanyia kazi kila siku kwenye uwanja wa mazoezi," Rodgers aliwaambia waandishi wa habari.
"Mwaka mmoja uliopita ningeweza kufukuzwa kazi, 'Tutakuja kufunga magoli?' na kama mtakumbuka tulimaliza na magoli 101 msimu uliopita.
"Tulilazimika kusajili wachezaji wengi katika dirisha lililopita kwa sababu ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Hili huchukua muda mrefu zaidi kidogo lakini nimeridhishwa na jinsi kila mmoja anavyozoea mazingira. Tuna wachezaji wanaojizoea mazingira ya nchi nyingi tofauti."
Mmoja wa wachezaji wapya wa Rodgers, mshambuliaji Mario Balotelli, aliifungia Liverpool goli lake la kwanza kwenye ushindi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets Jumanne.
Makubwa yanategemewa kutoka kwa Muitalia huyo mwenye hasira za karibu baada ya kuvaa viatu vya mfungaji bora wa msimu uliopita Anfield, Luis Suarez na Rodgers ameridhishwa na ukomavu ambao Balotelli ameonyesha tangu ajiunge kutoka AC Milan.
"Anaifahamu vizuri historia, si tu ya klabu bali ya jiji la Liverpool," Rodgers alisema. "Nitatumia muda mwingi na wachezaji wengi lakini ni kijana mzuri na nadhani unaweza kuona kwamba yupo tayari kwa kazi."
Baada ya kufungwa bila kutarajiwa na Aston Villa mwishoni mwa wiki iliyopita, Liverpool iliyo katika nafasi ya nane ni mgeni wa West Ham United leo ikitaraji kupunguza pengo la pointi sita na viongozi Chelsea.

Tanzania yazidi kuporomoka FIFA, Cameroon yapaa

http://imikinonews.com/files/news_images/1596757601114051870520140716101415.jpgTANZANIA imeendelea kuporomoka tena kwenye viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya kuanguka kwa nafasi tano katika viwango vipya vilivyotolewa.
Tanzania, ambayo ilifungwa 2-0 na Burundi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopita, sasa inakamata nafasi ya 115 duniani na 33 barani Afrika ikiwa nyuma ya Uganda wanaoongoza Afrika Mashariki wakiwa nafasi ya 79 duniani na 19 Afrika, Rwanda walioko nafasi ya 93 duniani na 25 Afrika na Kenya walioporomoka kwa nafasi saba wakiwa nafasi ya 30 Afrika na 111 duniani.
Aligeria waliopanda kwa nafasi nne, wanaongoza barani Afrika wakiwa nafasi ya 20 duniani wakifutwa na Ivory Coast walioshuka kwa nafasi tatu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Cameroon waliopanda kwa nafasi 12 na kukamata nafasi ya nane Afrika na 42 duniani.
Nafasi ya tatu barani Afrika inakaliwa na Tunisia (31) wakipanda kwa nafasi 11 wakifuatwa na Ghana (33), Senegal (36), Nigeria (37) na Cape Verde (41). Guinea waliopanda kwa nafasi 16 wanakamata nafasi ya tisa barani Afrika na 48 duniani huku Burkina Faso waliopanda kwa nafasi 10 wakifunga pazia la 10 bora barani Afrika wakifungana na Guinea katika nafasi ya 48 duniani.
Uganda pia ni wa kwanza katika Ukanda wa Cecafa wa Afrika Mashariki na Kati wakifuatwa na Rwanda, Kenya, Tanzania, Burundi, Ethiopia (39, 132), Sudan (40, 133), Shelisheli (47, 172), Sudan Kusini (50, 185), Eritrea (52, 202), Somalia (53, 204) huku Djibouti wakifunga mlango Cecafa na Afrika wakiwa 54 Afrika na 205 duniani.
Mabingwa wa dunia, Ujerumani wanaongoza 10 bora ulimwenguni wakifuatwa na Argentina, Colombia waliopanda kwa nafasi moja wakiwashusha Uholanzi, Ubelgiji, Brazil, Uruguay, Hispania, Ufaransa na Uswis.

Spurs walalamikia ubaguzi, wenyeji wao waomba radhi

Roberto Soldado
Patashika baina ya Spurs na Partizan

partizan banner
Bango lililoibua hisia za kibaguzi ambalo Spurs wamelalamikia UEFA
Jan Verthongen (R) challenges Partizan Belgrade"s Danko Lazovic UONGOZI wa klabu ya Tottenham Hotspurs limepeleka malalamiko yao Shirikisho la Soka la Ulaya, UEFA kufuatia kuonyeshwa kwa mabango yenye kulenga ubaguzi na mashabiki wa Partizan Belgrade. 
Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino ameelezea bango hilo kama jambo lisilokuwa na heshima na lisilokubalika. 
Spurs walishindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa suluhu na wenyeji wao katika Uwanja wa Partizani, nchini Serbia.
Maofisa wa Spurs waliwataarifu UEFA juu ya uwepo wa bango hilo kabla ya mapumziko na wajumbe wake walilipiga picha kama ushahidi baada ya mchezo huo. 
Mwaka 2007, Partizan walitolewa katika michuano ya Kombe la UEFA na kutozwa faini kwa vurugu wakati wa mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano hiyo dhidi ya Zrinjski Mostar.
Tayari uongozi wa klabu ya Partizan imeomba radhi kwa kitendo hicho kilichofanywa na mashabiki wao kupitia mabango hayo.