STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 20, 2014

Real Madrid 'yachinja' mtu 8 ugenini La Liga

Real Madrid
James Bond akishangilia moja ya mabao ya Real Madrid
REAL Madrid wamezidnuka kwenye Ligi Kuu ya Hispania baada ya kupata ushindi mnono ugenini wa mabao 8-2  dhidi ya Deportivo la Coruna.
Hat trick ya Cristiano Ronaldo na mabao mawili mawili toka kwa Gareth Bale na Javier Harnandez 'Chicharito na jingine la James Rodgriuez yalitosha kuwapa ushindi huo Madrid dhidi ya wenyeji wao.
Ronaldo alianza kufunga bao dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya Arbeloa kabla ya James Bond kufunga la pili dakika ya 36 akimalizia pande la Karim Benzema na dakika nne kabla ya mapumziko Ronaldo alirudi tena nyavuni kwa kufunga bao la tatu kwa pasi ya Benzema.
Kipindi cha pili ndicho kilichokuwa kiama kwa wenyeji ambao licha ya kupata bao la kujifutia machozi lililofungwa dakika ya 51 na Medunjanin kwa mkwaju wa penti haikusaidia kitu kwani Bale alifunga bao la nne dakika ya 66 na kuongeza jingine dakika nane baadaye.
Ronaldo alitimiza hat trick yake dakika ya 78 kabla ya Toche wa Deportivo kufunga bao la pili dakika ya 84 na mtokea benchi Chicharito kufunga mabao mawili ya haraka haraka dakika za 88 na 90 na kuifanya vijana wa Carlo Ancelont kuvuna ushindi wa mabao 8-2.

No comments:

Post a Comment