STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 20, 2014

Kocha Liverpool ajipa matumaini juu ya kikosi chake

http://assets.kompas.com/data/photo/2014/08/31/2107275000-DV1855065780x390.jpgKOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers ametamba kwa kusema kuwa, Liverpool haihitaji fomula maalumu kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Uingereza na wachezaji wake wapya wameanza kuzoea maisha klabuni Anfield.
Baada ya kuvuka matarajio msimu uliopita na kushika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Manchester City, Liverpool imeanza kwa kusuasua msimu huu, ikifungwa mechi mbili kati ya nne za ligi kuu.
Lakini ikiwa ilisajili wachezaji wengi katika dirisha lililopita, Rodgers hadhani kama itachukua muda mrefu kabla ya kikosi chake kuzoeana na kuanza kupanda kwenye msimamo wa ligi.
"Siku zote tutaangalia namna tofauti tofauti za kushinda mechi. Hakuna fomula moja ya uhakika, ni kufanyia kazi kila siku kwenye uwanja wa mazoezi," Rodgers aliwaambia waandishi wa habari.
"Mwaka mmoja uliopita ningeweza kufukuzwa kazi, 'Tutakuja kufunga magoli?' na kama mtakumbuka tulimaliza na magoli 101 msimu uliopita.
"Tulilazimika kusajili wachezaji wengi katika dirisha lililopita kwa sababu ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Hili huchukua muda mrefu zaidi kidogo lakini nimeridhishwa na jinsi kila mmoja anavyozoea mazingira. Tuna wachezaji wanaojizoea mazingira ya nchi nyingi tofauti."
Mmoja wa wachezaji wapya wa Rodgers, mshambuliaji Mario Balotelli, aliifungia Liverpool goli lake la kwanza kwenye ushindi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Ludogorets Jumanne.
Makubwa yanategemewa kutoka kwa Muitalia huyo mwenye hasira za karibu baada ya kuvaa viatu vya mfungaji bora wa msimu uliopita Anfield, Luis Suarez na Rodgers ameridhishwa na ukomavu ambao Balotelli ameonyesha tangu ajiunge kutoka AC Milan.
"Anaifahamu vizuri historia, si tu ya klabu bali ya jiji la Liverpool," Rodgers alisema. "Nitatumia muda mwingi na wachezaji wengi lakini ni kijana mzuri na nadhani unaweza kuona kwamba yupo tayari kwa kazi."
Baada ya kufungwa bila kutarajiwa na Aston Villa mwishoni mwa wiki iliyopita, Liverpool iliyo katika nafasi ya nane ni mgeni wa West Ham United leo ikitaraji kupunguza pengo la pointi sita na viongozi Chelsea.

No comments:

Post a Comment