STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 21, 2014

Ajali! Watu 20 wapoteza maisha katika ajali Simiyu


WATU zaidi ya 20 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya wilayani Busega Mkoani Simiyu leo asubuhi kufuatia ajali ya Bus la kampuni ya Luhuye iliyopasuka mpira, kuacha njia na kugonga nyumba.

Mbunge wa Jimbo la Busega ambaye pia ni Waziri wa uvuvi na maendeleo ya Mifugo Dakta Titus Kamani ameiambia Blog hii kwa njia ya Simu kwamba ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sogesita wilayani humo.

Dakta Kamani amesema basi hilo lilikuwa likielekea Jijini Mwanza ndipo lilipopasua mpira wa mbele na kupinduka huku likigeukia lilikotoka kabla ya kuacha njia na kugonga nyumba kwenye kaya moja kijijini hapo.

Amesema, idadi kamili ya waliopoteza maisha na hali za majeruhi itafahamika baadaye 

Chanzo:farajimfinanga.com