STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 13, 2013

Azam yaiengua Yanga, Mbeya City moto chini, Mtibwa yaua, Abdalla Juma apiga Hat Trick, Maguri naye kama kawa

Mbeya City

Azam Fc
MABINGWA watetezi Yanga imeenguliwa kwenye  nafasi ya pili na kuporomoka hadi nafasi ya nne kufuatia jioni hii timu za Azam na Mbeya City kupata ushindi katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Azam iliisasambua JKT Ruvu kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Chamazi, huku Mbeya City wakipata pointi tatu katika uwanja wa Mkwakwani kwa kuizabua Mgambo JKT kwa bao 1-0.
Ushindi wa timu hizo umezifanya Azam kurejea kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 17 sawa na za Mbeya City inayokamata nafasi ya tatu ila inawazidi uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam ilipata ushindi wake kwa mabao ya Humphrey Mieno katika dakika 12 kabla ya Erasto Nyoni kufunga bao la pili kwa kichwa dakika ya 32 mabao yhaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kilipoisha.
Bao la tatu lililowanyong'onyesha JKT lilifungwa na kiungo Salum Abubakar Sure Boy dakika ya 90.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Elias Maguri aliendeleza kasi yake ya kufumania nyavu baada ya kuifungia Ruvu Shooting bao pekee katika pambano lao dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi.
Maguri alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati baada ya Aypoub Kitala kurangushwa kwenye lango la Rhino na mfungaji huyo kufunga penati. Hata hivyo Ruvu ilipata pigo baada ya kiungo wake Juma Seif 'Kijiko' kulimwa kadi nyekundu.
Nayo Mtibwa Sugar ikiwa kwenye uwanja wa Manungu iliisambaratisha Oljoro JKT kwa kuifunga mabao 5-2, huku Abdsalla Juma akitupia kimiani mabaop matatu (hat Trick) na kuweka rekodi.
Maao mengi ya Mtibwa yalifungwa na Juma Luizio na kumfanya afikishe jumla ya mabao matano mpaka sasa.
Mabao ya kufutia machozi ya Oljoro yalifungwa na Saidi Nayoka na Amir Omar.

MECHI YA SIMBA, PRISONS YAINGIZA MIL 60/-

Na Boniface Wambura
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Simba na Tanzania Prisons kutoka Mbeya iliyochezwa jana (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 60,521,000.

Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 55 na kushuhudiwa na watazamaji 10,494 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 14,191,002.55 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,232,016.95.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,215,763.96, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,329,458.37, Kamati ya Ligi sh. 4,329,458.37, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,164,729.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,683,678.26.

Mbunge Kigamboni ateta na wapiga kura wake


MBUNGE wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile akihutubia wananchi wa Kijichi wakati wa ziara yake ya kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama chake cha CCM katika kipindi cha uongozi wake. Pia alipata nafasi ya kupokea kero mbalimbali za wananchi.

Mauaji!: Mtangazaj ITV/Radio One apigwa risasi, ampoteza mama mzazi

Ufoo Saro (kulia) aliyepatwa na mkasa hivi punde
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema mtangazaji wa kituo cha ITV, Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa risasi, huku mama yake mzazi akipoteza maisha baada ya mtu anayedakiwa kuwa mchumba wake au mumewe kuwafyatulia risasi katika ugomvi wa kimapenzi.

Taarifa zinasema kuwa mchumba wa mtangazaji huyo aliyetajwa kwa jina la Ansel aliyekuwa nchini Sudan kikazi alitua nchini jana na kufikia kwa Ufoo lakini kukatokea mzozo ambao haukupata suluhisho.

Hivyo wawili hao waliongozana hadi kwa mama wa mtangazaji huyo kutafuta suluhu, asubuhi hii na kwa bahati mbaya hali ilikuwa tete na ndipo kijana huyo alipotoa bastola aliyokuwa nayo na kumtwanga mama mtu risasi ya kichwa iliyomuua papo hapo.

Kama hiyo haikutosha inaelezwa jamaa huyo alimtwanga risasi Ufoo kifuani na nyingine mguuni na kudhani amemuua kabla ya yeye mwenyewe kujilipua mwenyewe kwa risasi ya kidevuni na kumuua.

Tayari miili ya watu hao wawili yaani mama yake Ufoo na jamaa huyo imepelekwa Muhimbili sambamba na mtangazaji huyo anayeelezwa yupo katika hali mbaya kwa ajili ya kuhifadhiwa na matibabu zaidi.

Haifahamiki chanzo cha mauaji hayo licha ya kudaiwa huenda ni ugomvi wa kimapenzi na haifahamiki jamaa huyo huko Sudan anakodaiwa kuwa alikuwa akifanya kazi UN alikuwa kama nani japo inaelezwa huenda alikuwa mwanajeshi ambapo kabla ya kwenda huko aliwahi kuwa mpiga picha wa ITV na kufanya kazi Mahakama ya Kimataifa ya Arusha kabla ya kuomba kazi UN.
MICHARAZO inaendelea kufuatia kwa kina taarifa hii na itawafahamisha. Pia inamuombea kila la heri na salama mtangazaji huyo aweze kupona katika mkasa uliopata na kumpoa pole kwa msiba uliompata kwa kumpoteza mama yake mzazi.

Drogba aibeba Ivory Coast, waifyatua Senegal 3-1 WCQ

drog
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa Ivory Coast, Didier Drogba alirejea kwa kishindo katika timu hiyo baada ya kuiongoza kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal katika pambano la kwanza la mtoano wa kuwania nafasi tano za kutinga Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Drogba aliitwa tena katika kikosi hicho baada ya awali kuwekwa kando na kusaidia kufunga bao la penati kabla ya Solomon Kalou kufunga la tatu huku la pili wageni wao wakijifunga wenyewe.
Ivory Coast 'The Elephants' sasa imeingia mguu mmoja ndani kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia ikihitaji sare yoyote katika mechi ya marudiano baadaye kukihakikisha kucheza fainali hizo kubwa duniani.
Mlinzi wa Senegal Ludovic Sane aliizawadia wenyeji bao kabla ya Kalou kufunga bao la tatu na dakika za lala salama Papiss Demba Cisse aliifungia Senegal bao la kufutia machozi ambalo linaweza kuwa msaada kama Senegal itaenda kushinda nyumbani mabao 2-0 katika mechi ya marudiano. Katika pambano jingine Burkina Faso wakiwa kwenye uwanja wao wa Agosti 4 waliwafunga Algeria 3-2 katika mchezo uliokuwa na upinzani wa aina yake .
Mabao ya Burkinabe yalifungwa na Jonathan Pitroipa , Aristide Bance na Djakaridja Kone huku Algeria wakifunga kupitia kwa Soufiane Feghouli na Carl Medjani. Bukinabe sasa wanahitaji sare yoyote katika mechi ya marudiano itakayofanyika ugenini kufuzu fainali hizo ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwao.
Michezo hiyo ya kuwania fainali hizo za Kombe la Dunia hatua ya mwisho kwa nchi za Afrika zitaendelea tena leo kwa mabingwa wa Afrika Nigeria kuwa ugenini mjini Addis Ababa kupepetana na wenyeji wao Ethiopia, wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) huku timu iliyopenya baada ya Cape Verde kuenguliwa kwa udanganyifu Tunisia itaialika Cameroon na keshokutwa Jumanne Ghana watakuwa wenyeji wa Misri.

Ashanti United yaona mwezi, yailaza Coastal Union 2-1

 
MABAO mawili yaliyofungwa na Tumba Sued moja likiwa la penati liliisaidia Ashanti United kupata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara na kujinasua mkiani wakiiachia Mgambo JKT ya Tanga.
Ashanti iliipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi kwa kuicharaza Coastal Union ya Tanga mabao 2-1, bao la ushindi likifungwa dakika za jioni na kulalamikiwa na Wagosi wa Kaya.
Tumba Sued beki wa kati mmoja wa wachezaji chipukizi wanaotoka ukoo wa wanasoka kaka zake wakiwa ni Said Swued 'Panucci' na Salum Sued 'Kussi' alifunga bao la kwanza kabla ya Coastal Union kusawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia nahodha, Jerry Santo.
Mchezaji huyo mrefu aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchini China, aliiongezea Ashanti bao la pili dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati na kuifanya Ashanti ifikishe pointi 5 sawa na Mgambo JKT, ambayo leo inashuka dimbani kuvaana na Mbeya City mjini Tanga.
Hata hivyo Ashanti wapo juu ikishika nafasi ya 13 kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa na kuiacha Mgambo ikiburuza mkia kwa sasa.
Matokeo ya mechi za jana pia zilibadilisha msimamo wa ligi kuu ambapo Yanga ilikwea hadi nafasi ya pili ikiwapumulia watani zao watakaovaana nao Jumapili kwenye uwanja wa Taifa, huku Coastal ikijikuta ikiporomoka kwa nafasi moja hadi nafasi ya nane ikiiachia nafasi Ruvu Shooting ambaye hata hivyo jana haikushuka dimbani kwa leo leo itapepetana na Rhino Rangers ya Tabora kwenye uwanja wa Mabatini.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014                                        P  W  D  L    F  A  GD  PTS

1.  Simba                    8    5   3   0   17  5  12  18
2.  Yanga                    8    4   3   1   15   8   7   15
3.  Azam                     8    3   5   0   11   6   5   14
4.  Mbeya City            8    3   5   0   11   7   4   14
5.  JKT Ruvu              8    4   0   4    9    7   2   12
6.  Kagera Sugar         8    3   2   3    9    7   2   11
7.  Ruvu Shooting        8    3   2   3    9    7   2   11
8.  Coastal Union        8    2    5   1    7    5   2   11
9.  Mtibwa Sugar        8    2    4   2    7    9  -2  10
10.Rhino Rangers        8    1    4   3    8   11 -3   7
11.Prisons                   8    1    4   3    4   10 -6   7
12. Oljoro                   8    1    3   4    6   10 -4    6
13.Ashanti                   8    1    2   5    6   16 -10  5
14.Mgambo                 8    1    2   5     2   13 -11  5

Wafungaji:
8-
Tambwe Amisi (Simba
4-
Didier Kavumbagu (Yanga), Peter Michael (Prisons), Kipre Tchetche (Azam), Elias Maguri (Ruvu Shooting)
3- Jerry Tegete, Hamis Kiiza (Yanga), Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Jerry Santo (Coastal Union), Tumba Sued (Ashanti Utd)
2- Haruna Moshi (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya (Mbeya City), Mrisho Ngassa (Yanga), Godfrey Wambura (Kagera Sugar)
1- Abdi Banda, Crispian Odulla,(Coastal Union), Henry Joseph, Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris,  John Bocco, Joseph Kimwaga, Faridi Maliki (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Peter Mapunda (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader, Said Dilunga (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Nditti, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG) (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary, Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)

Ratiba za Ligi Kuu

Leo
Ruvu Shooting vs Rhino Rangers (-)
Mgambo JKT vs Mbeya City (-)
Azam vs JKT Ruvu (-)
Mtibwa Sugar vs Oljoro JKT (-)

Okt 16, 2013

Ashanti Utd vs Prisons (-)

Okt 19, 2013

Kagera Sugar vs Coastal Union (-)
Oljoro JKT vs Azam (-)
Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT (-)
Mbeya City vs JKT Ruvu (-)
Ashanti Utd vs Ruvu Shooting

Okt 20, 2013
Simba vs Yanga