STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 7, 2013

PAMBANO LA ZAM, BYC LAINGIZA MIL.44

 
Na Boniface Wambura
MECHI ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana (Aprili 6 mwaka huu) imeingiza sh. 44,229,000.

Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi.

Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212.

Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 28,990,500.

Mechi iliyopita ya raundi ya awali ya mashindano hayo kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 16 mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.

TFF YAPONGEZA WAANDISHI WALIOSHINDA TUZO YA EJAT


Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapongeza waandishi watatu wa habari za michezo kwa kushinda Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) inayotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Waandishi hao walioshinda katika kategori ya michezo na utamaduni ni Abdul Mohammed wa The African kwa upande wa magazeti na Abdallah Majura wa redio ABM kwa upande wa redio.

TFF tunawapongeza kwa ushindi huo uliotokana na makala zao ambazo zina mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu, lakini pia ni changamoto kwa waandishi wengine ambao hawakufanikiwa kushinda.

Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika ustawi wa michezo ukiwemo mpira wa miguu, kwani katika nchi nyingine vimefichua rushwa. Ni matarajio yetu kuwa vyombo vya habari nchini navyo vitakuwa mstari wa mbele katika kufichua na kupambana na rushwa katika mpira wa miguu.

PICHA PARTY YA KAJALA ALIPOKARIBISHWA TENA 'URAIANI"


 wema, kajala n friend wakishow love..
best friends forever inshaallah mwenyez mungu awaweke
hapa wakiingia ukumbini..
wema, dj fetty n kajala..
  
  keki..
hayaweee mambo JD hayooo...
  
akizungumza machache kabla ajakata keki..
  
wema na yeye akiongea machache,,, kajala dont cry bhanaa...
  
keki hizooo..
  
yumm!!
tamani mie hapa..
maraiki mbalimbali wakilishwa keki..
aunt n kajala..
  
bilali mashauzi, bilal wa A akila keki na yeye..
hapo chacha!! kajala akimlisha petit man keki..
 yvone nae akila keki..
  
**WELCOME BACK KAJALA**
From: zeddylicious