STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 5, 2015

Lukas Podolski awashukuru Arsenal akitua San Siro

http://cdn.caughtoffside.com/wp-content/uploads/2014/12/460208232.jpg
Lucas Podolski
MPANGO wa Lukas Podolski kuhamia Inter Milan kwa asilimia kubwa umekamilika kufuatia  mshambuliaji huyo wa Ujerumani kukutana na kocha wa klabu hiyo Roberto Mancini katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Jumamosi.
Nyota huyo ameshaaga Arsenal tayari kuanza maisha mapya katika Ligi ya Italia maarufu kwa jina la Seria A.
“Mshindi huyu wa kombe la dunia alikuwepo Centro Sportivo Angelo Moratti leo (jana) kwa lengo la kufahamu uwanja wake mpya wa mazoezi na alikutana na kocha wa Nerazzurri ,” taarifa ya Inter Milani kwa vyombo vya habari ilieza.
Mshambuliaji huyo wa Gunners amecheza mechi 13 tu za michuano yote msimu huu, hakuna aliyoanzishwa, lakini bado alitumia muda wake kuwashukuru mashabiki kwa sapoti yao kuelekea kuondoka kwake.
“Siwezi kuelezea kwa maneno shukrani yangu kwa mashabiki wa Arsenal kwa yote waliyoyafanya kwangu katika miaka yangu niliyokuwapo London,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.
“Tafadhalini mtambue kuwa moyo wangu daima una nafasi yenu. Natumai nimeacha alama yangu klabuni na kwa mashabiki pia. Natumai tutaonana tena! COYG.”
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Arsenal akitokea FC Koln 2012 na mkataba wake wa sasa na Gunners unamalizika Juni 2016.

Azam yafufuka Zanzibar yainyoa KMKM

AZAM FC imezidnuka kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa wa Zanzibar, KMKM katika mechi iliyochezwa usiku wa jana kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bao pekee la Azam liliwekwa kimiani katika dakika ya 18 kutokana na kujifunga kwa nahodha wa KMKM, Khamis Ali akijaribu kuokoa mpira wa krosi ya Shomari Kapombe.
Ushindi huo umeifanya Azam kufikisha pointi 4 na kulingana na timu ya KCCA waliotoshana nao nguvu katika mechi yao ya kwanza walipofungana mabao 2-2.
Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo ya Kundi C Mafunzo wakivaana na Mtibwa Sugar majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Amaan kabla ya usiku Simba watashuka dimbani kuchuana na JKU.

Fernando Torres atambulishwa Atletico Madrid baada ya kurejea

2
Torres alipotambulishwa klabu ya Atletico Madrid
3456MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Liverpool na Chelsea, Fernando Torres amerejea rasmi kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid ya nchini Hispania.
Torres aliondoka miaka saba iliyopita kwa kujiunga na Liverpool ya England kabla ya kuhamia Chelsea na baadauye kutolewa kwa mkopo AC Milan.
”Nimefurahi sana kurejea klabu yenye nafasi kwenye maisha yangu,niliondoka kwenye klabu hii kwenda kukuza kiwango changu,nafurahi kurejea tena Atletico ikiwa sasa inashindana na vilabu vikubwa ulimwenguni,nimerejea kushinda na mataji na klabu hii niipendayo”.
Hayo yalikuwa maneno ya Torres wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wake uliohudhuliwa na mashabiki zaidi ya 45,000 kwenye dimba la Vicente Calderon jana.

Binti wa miaka 14 akamatwa akitaka kujilipua bomu

Binti Zahrau akihojiwa
BINTI mmoja aliyefahamika kwa jina la Zahrau Babban Gida (14) ameshikiliwa na jeshi la polisi nchini Nigeria baada ya kukamatwa akiwa katika harakati za kulipua bomu kwa kujitoa mhanga. 
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii, Msichana Zahrau amekamatwa wakati alipokuwa amejifunga mabomu mwili mzima tayari kwa kufanya maangamizi na alichokuwa akikisubiri ni kuripuka tu. na kama angefanikiwa basi angeweza kutoa uhai wa watu zaidi ya 1000 kwa dakika moja tu. 
Zuhrau amezungumza na vyombo vya habari akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi la nchini humo na kusema kuwa, amejiunga na kundi la Bokoharamu kutokana na msukumo kutoka kwa baba yake mzazi ambaye ndiye aliyemlazimisha kujiunga na kundi hilo. 
Zahrau ameongeza kuwa alipofika huko kwenye kambi ya Bokoharam aliwakuta wasichana wengi ambao wamepewa mafunzo ya kujitoa mhanga. 
Uchunguzi umebainisha kwamba Bokoharam wameamua kutumia watoto wadogo katika kujitoa mhanga kwasababu watu wazima wamekuwa wakishitukiwa kirahisi katika harakati zao. 
Chanzo: Nigernews

Kachumbari kuzikwa kesho Goba, Dar es Salaam

10898226_10152990764907888_9161307175547706048_n
Flowin Kachumbari
MWANAMUZIKI mpiga drum wa miaka mingi ambaye hivi karibuni alikuwa na bendi yake African Chacha Band, Kachumbari aliyefariki jana anatarajiwa kuzikwa kesho Goba, pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Frowin ambaye ni mwenyeji wa mikoa ya Kusini alianzisha bendi yake hii akawa akipiga muziki wa mahadhi ya kwao na kuwa na tenda nyingi katika mahoteli mbalimbali. Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya uti wa mgongo yaliyokuwa yakimsababishia maumivu ya miguu.(Picha kwa Hisani ya William Kaijage)

Barcelona yagongwa na Moyes, yashindwa kuing'oa Real Madrid

Real Sociedad's Xabier Prieto (right) attempts to claim the goal after Alba's header on two minutes
Real Sociedad wakishangilia bao la kujifunga la Barcelona
Former Liverpool striker  Suarez (left) competes with Real Sociedad's Alberto de la Bella as Barcelona chase the game
Suarez akichuana na mchezaji wa Real Sociedad
Barcelona enforcer Javier Mascherano (left) holds off Canales of Real Sociedad during the first half
Javier Mascherano akiwania mpira katika pambano ambalo Barcelona ililala bao 1-0
BAO la kujifunga la dakika ya pili lililotumbukizwa wavuni na Jordi Alba kwa kichwa katika harakati za kuokoa mpira zimeikwamisha Barcelona kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya Real Sociedad inayonolewa na kocha David Moyes.
Barcelona walikuwa na nafasi ya kuiengua Real Madrid waliofungwa mabao 2-1 ugenini na Valencia, walishtukizwa na kipigo hicho ambacho na hasa baada ya kuwaanzisha benchi nyota wake Lionel Messi, Neymar na wengine kabla ya kuwaingia ili kuibeba biola mafanikio.
Kwa kipigo hicho Barcelona imesaliwa na pointi 38 ikishika nafasi ya pili nyuma ya Real Madrid yenye pointi 39 ikiwa na mchezo mmoja mkononi, huku Atletico Madrid ikiwa na pointi 38 wakishika nafasi ya tatu.
Ligi hiyo ya Hispania itaendelea leo kwa pambano moja litakalowakutanisha timu zaCardoba itakayoikaribisha Granada.

Bondia Omar Kimweri kuja kufunza ngumi, Super D achekelea

Na Mwandishi Wetu
NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.
Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
Kwa hapa nchini, wapo mabondia waliojitengenezea majina wakiwamo Emmanuel Mlundwa, Habibu Kinyogoli 'Masta' Michael Yombayomba, Stanley Mabesi 'Ninja' Rashid Matumla, Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  na wengineo wengi.
Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Mayweather, akifuatiwa na mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.
Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya nne, huku wa tano akiwa ni mkali wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant.
Pamoja na mafanikio hayo katika ndondi, Tanzania imeonekana kuzidi kulala usingizi wa pono katika suala zima la kuvumbua na kuendeleza vipaji vya mchezo huo kama sehemu ya kutatua tatizo sugu la ajira linaloitesa nchi yetu kwa sasa.
Unapopita huko mitaani, unaweza kukutana na vijana wadogo wakiwa wanafanya mazoezi ya ngumi kwa kutumia vifaa visivyo rasmi ambavyo mwisho wa siku, huishia kuwadumaza badala ya kuwajenga kama walivyotarajiwa.
Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia mchezo huo, zikiwamo kumbi na hata wataalam wa kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufikia mafanikioi ya akina Mayweather.
Ni kwa kufahamu hilo, wapo wadau wa ndondi ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia vipaji vya ndondi hapa nchini, miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Kimataifa wa Ndondi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’.
Bondia huyo wa zamani, ameshawahi kufanya jitihada kadha wa kadha kuendeleza ndondi hapa nchini, ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana chini ya klabu yake ya Ashanti Boxing Club na kupitia DVD zake zenye mapambano makali yaliyowahi kufanyika hapa nchini na duniani kwa ujumla, yakiwahusisha mabondia nyota.
Katika kuonyesha jinsi anavyoguswa na ndondi, Februari mwaka huu Super D atakuwa na ugeni mkubwa wa bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri ambaye anatua nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanamasumbwi wa Tanzania.
Akizungumza Dar es salaam jana, Super D anasema kuwa ujio wa Kimweri ni fursa nyingine adimu kwa mabondia wa Tanzania katika kuona ni vipi wanaweza kutimiza ndoto zao za kutoka kimaisha kupitia mchezo huo.
Anasema kuwa Kimweri atatua akiwa na vifaa mbalimbali vya masumbwi ambapo pia atatoa mafunzo na mbinu mpya zinazotumiwa na mabondia wa nje kwa mabondia pamoja na kushuhudia mapambano kadhaa yatakayofanyika kwa kipindi atakachokuwapo hapa nchini.
“Kimweri anakuja akiwa na msafara wa watu kadhaa, akiwamo mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. Akiwa hapa nchini, Melanie atapata fursa ya kukutana na wanasoka wa kike wa hapa , kwani amechezea timu nyingi za Ulaya,  Hispania,” anasema Super D.
Anasema kuwa ujio wa Kimweri umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na promota wake, Brian Amatruda ambaye ni miongoni mwa mapromota maarufu nchini kwao Australia, akiwa amekubali kutoa baadhi ya vifaa vya kisasa kutoka Hispania na Marekani kwa ajili ya ziara hiyo.
Super D anasema kuwa Kimweri ambaye ni bingwa wa WBO, atatua nchini akiwa na mikanda yake yote aliyowahi kutwaa, ukiwamo wa ubingwa wa Australia, lengo likiwa ni kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujikita zaidi katika ndondi.
“Nimezungumza na Kimweri na ameonyesha kuwa na uchungu wa kuwainua mabondia wa hapa nchini ili waweze kutimiza ndoto zao na anafanya hivyo chini ya mradi wake wa ‘Kimweri Project’ na atakuwa hapa nchini kwa wiki moja,” anasema.
Anasema kuwa ujio wa bondia huyo uliochagizwa na Super D Boxing Coach and Promotion, umelenga kuwahamasiaha mabondia kucheza mara kwa mara ili kupandisha viwango vyao kwani hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanamasumbwi wengi duniani.
Mbali ya mafunzo kutoka kwa Kimweri, pia katika ziara zake zote sehemu mbalimbali nchini, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Super D zenye lengo la kutoa mafunzo kupitia mapambano ya mabondia maarufu duniani, akiwamo Floyd Mayweather,Manny Paquaio, Mohamerd Alli, na wa hapa nchini kama Mbwana Matumla, Francis
Miyeyusho, Ibrahimu Class' King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa WPBF Africa na wengineo.