STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 7, 2014

Messi amjibu Ronaldo, Barca ikiua 5-1 Hispania

Messi akishangilia moja ya mabao yake leo
Suarez na Pique wakishangilia bao la pili la Barcelona
Kabakisha hat trick mbili tu kumkuta Ronaldo
Akipongezwa na Neymar
Bravo Brother!
Utukuzwe uliyenijalia kipaji hiki cha soka
 STRIKA Lionel Messi amejibu hat trick ya Cristiano Ronaldo baada ya kufunga magoli matatu wakati akiisaidia Barcelona wakiiangamiza wapinzani wa Jimbo la Cataluna, Espaniol kwa mabao 5-1 katika mechi ya La Liga usiku huu.
Messi amefunga mabao hayo na kufanya afikishe jumla ya mabao 256 na kuzidi kumuacha mbali Ronaldo aliyefikisha mabao 200 jana usiku.
Wageni Espanol walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya 13 na Sergio García kabla ya Messi kusawazisha kabla ya mapumziko.
Mkali huyo alifunga bao la pili dakika ya 50 akimalizia kazi ya Suarez kabla ya Gerrard Pique kuongeza bao la tatu dakika ya 53 kwa kichwa na Pedro kuongeza la nne dakika ya 77.
Messi alifikisha hat trick ya 21 na hat trick ya tatu katika mechi nne tofauti zilizopita katika dakika ya 81 kwa kazi nzuri ya Pedro na kuifanya Barcelona kufikisha jumla ya pointi 34 na kukwea hadi nafasi ya pili wakiiengua watetezi Atletico Madrid wenye 32.
katika mchezo mwingine mapema, SEvilla ikiwa ugenini ilinyukwa bao 1-0 na Rayo Vallecano.

Rais JK ateua RC mpya, sita awapangua

http://dar24.com/wp-content/uploads/2013/05/rais-jk-kikwete1.jpg
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.
Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.

AC Milan yapigwa kidude ugenini

http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2014/1130/fc_milan_jc_1296x729.jpg&w=738&site=espnfcMABINGWA wa zamani wa Italia na Ulaya, AC Milan jioni ya leo imedonyolewa ugenini bao 1-0 na Genoa katika mfululizo wa Ligi ya Italia Serie A.
Bao pekee lililowazamisha vijana wa Phillip Inzaghi 'Pippo' lilitumbukizwa wavuni katika dakika ya 32 na beki wa Genoa Luca Antonelli.
Kipigo hicho kimeifanya Milan kusalia nafasi ya saba ikiwa na pointi 21 wakati wenyeji wao wakipanda hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 26.
Katika mechi  nyingine zilizochezwa leo Napoli ikiwa nyumbani iling'ng'aniwa na Empoli na kutoka sare ya mabao 2-2, Atalanta ikaifumua Cesena kwa mabao 3-2  na Parma ikakubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Lazio.      

WEMA SEPETU KATIKA TUHUMA NZITO

TUKIO:Wapigwa na kuvuliwa nguo nyumbani kwa Wema
MSANII Mwema Sepetu 'Madame' ametupiwa tuhuma nzima kutokana na tukio lililotokea nyumbani kwake kwa watu wawili wanaodaiwa kuwa mafundi, kupigwa na kudhalilishwa kwa kuachwa uchi wakidaiwa kuhusika na wizi.
Wema akiwa ndani
Kwa mujibu wa Bongo5.com ambao walizungumza jana na jirani wa Wema aliyetambulika kwa jina la Mama Steve, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.
“Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea Wema nyumba yake,” amesema mama huyo. “Sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani, ndo mtiti ukaanza.”
“Petit akatumwa akachukue mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki mpaka mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani. Sasa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia mtu analia sana ikambidi akachungulie ndo akamkuta fundi watu wawili wamelazwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa! Ndo yule jamaa kwakuwa alikuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafungue lakini hawajafungua geti. Tukawa tunasikia sauti ya Wema ikisema ‘jamani waacheni hao mtawaua’ lakini anasema hivyo wakati yeye inaonyesha ndo alikuwa kinara wa matukio hayo. Wema na ana roho ya kikatili sana. Amefanya matukio mengi lakini hivyo hapana! Yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyika tukio la kinyama sana,” ameongeza mama huyo.
“Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia na kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali. Sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha Mabatini na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia ndo wakawakamata baadhi ya watu na kuondoka nao. Hilo ndo tukio alilolifanya mwanadada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania,” alisema Mama Steve.
Pia shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mama Samira, alisema amesikitishwa na tukio hilo la kinyama. “Hii ni tabia yake, hata wafanyakazi wake wa ndani anao kaa nao saa zingine anawapiga makofi! Kwakuwa ni ndani kwa ndani sisi majirani hatufuatilii, lakini kwa hilo na sauti yake tumeisikia japo watu wake wanadai hakuwepo,” alisema.
Kwamujibu wa Bongo5.com,mjumbe wa nyumba kumi, Mwarami  alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai hataki kuliongelea sana kwakuwa limeshafika katika kituo cha polisi Mabatini.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Mabatini hakupatikana ilikuthibitisha na kutujuza kile kinachoendelea katika sakata hili.
Mtu wa karibu wa Wema, Petit Man aliyetajwa kuhusika kwenye tukio hilo, aliiambia Bongo5.com kuwa watu hao walipigwa lakini hawakuvuliwa nguo. “Yeah kuna tukio limetokwa,lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo,” alisema Petit na baada ya hapo alikata simu.

Shamsa Ford kufungua mwaka na 'Mama Muuza'

http://4.bp.blogspot.com/-3kB3Z0OrELQ/ULm-iBl9ybI/AAAAAAAADiY/rNnPTAHQ3yU/s1600/After+Death.JPG
Shamsa Ford katika pozi
 BAADA ya kuteka nyoyo za mashabiki kwa mwaka 2014 kupitia filamu yake mwenyewe iitwayo 'Chausiku', muigizaji nyota wa filamu nchini, Shamsa Ford anatarajiwa kuufungua mwaka mpya na 'Mama Muuza'.
Akizungumza na MICHARAZO, Shamsa alisema kama ilivyokuwa kwa 'Chausiku', filamu ya 'Mama Muuza', pia  ameiandika mwenyewe na kutamba itakuwa kali na 'funika bovu' kuliko kazi hiyo ya awali.
Shamsa alisema ndani ya filamu hiyo ambayo ndiyo itakayomfungulia mwaka 2014 ameigiza na wasanii mbalimbali akiwamo Baba Haji ambaye pia alikuwamo katika 'Chausiku'.
http://www.bongocinema.com/images/casts/Shamsa_Ford_03.jpg
Mkali Shamsa Ford
"Baada ya Chausiku kunifungia mwaka 2014, natarajia kuufungua mwaka mpya wa 2015 na kazi mpya iitwayo 'Mama Muuza' ambayo humo nimefanya makubwa kuliko hata yale ya 'Chausiku'," alisema.
Katika filamu ya 'Chausiku' moja kati ya filamu mbili alizocheza mwaka huu, nyingine ikiwa 'Hukumu ya Ndoa Yangu', Shamsa amecheza kama 'demu mcharuko' na kustaajabisha wengi tofauti na haiba yake ya upole.
http://2.bp.blogspot.com/-XgahLzr7LHs/UxrQOWVNkUI/AAAAAAAAAWU/MP54yq4WFHo/s640/1.jpg
Shamsa Ford
Shamsa alidokeza filamu hiyo imesharekodiwa na kukamilika na kwa sasa inawekwa kwenye foleni kwa ajili ya kuingia mtaani mwakani na kuwataka mashabiki wake kusubiri uhondo huo

Kumekucha Tamasha ya Dar Filamu 2014

http://2.bp.blogspot.com/-ZRYCVfIiuiM/VDqOF7T8m3I/AAAAAAAAcug/4O4mMaWXSWo/s1600/unnamed%2B(4).jpgTAMASHA la pili la Filamu la Dar es Salaam (Dar Filamu Festival 2014) linaratajiwa kufanyika kati ya Desemba 19-21 jijini Dar es Salaam na washiriki waliokuwa hawajajitokeza kuomba kushiriki wanatakiwa kufanya hivyo kabla ya kesho saa 10 jioni.
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo ambalo ni maaluma kwa kutangaza kazi za wadau mbalimbali wa filamu mbali na semina mbalimbali zinazoendeshwa juu ya namna ya kuzalisha filamu bora, Myovela Mfaiswa aliliambia MICHARAZO kuwa tamasha lao litafanyikaia viwanja vya Chuo cha Posta, KIjitonyama.
Mfaiswa alisema walitoa muda mrefu kwa washiriki kujitokeza kwa ajili ya ushiriki wa tamasha hilo na mwisho ni kesh Desemba 8 kabla ya kupangwa ratiba ya namna tamasha hilo litakavyoendeshwa kwa siku hizo tatu mfululizo.
"Tamasha leo linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kati ya Desemba 19-21 na siku ya Jumatatu (kesho) ndiyo mwisho wa washiriki kujitokeza kama tulivyoanisha njia mbalimbali za kujiandikisha kwa kujaza fomu iliyopo kwenye mtandao wa www.filamucentral.co.tz na kwingineko," alisema Mfaiswa.
Mfaiswa alisema tamasha la mwaka huu pia litakuwa na mabalozi wake kama ilivyokuwa mwaka jana kwa waigizaji nyota, Vincent Kigosi 'Ray' na Elizabeth Michael 'Lulu' waliobeba jukumu hilo.

Man United yamhakikisha LVG fedha za usajili mpya zipo

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02911/Louis_van_Gaal_2911698b.jpgKOCHA wa klabu ya Manchester United, Louis Van Gaal amehakikishiwa kupewa fedha za kufanya usajili kwenye kipindi cha Majira ya Kiangazi ili kuimarisha kikosi chake.
Uongozi wa klabu hiyo wamemueleka LVG kuwa pesa siyo tatizo kama akiamua kuimarisha kikosi chake katika kipindi cha majira ya kiangazi. 
Van Gaal alitumia kitita cha paundi milioni 150 katika majira ya kiangazi, ukiwemo usajili uliovunja rekodi Uingereza wa paundi milioni 59.7 kwa ajili ya Angel Di Maria lakini bado wanaburuzwa na vinara Chelsea kwa tofauti ya alama 11 katika msimamo wa Ligi Kuu. Kiungo wa ulinzi Kevin Strootman na mabeki Mats Hummels na Diego Godin wote wako katika rada za United. 
Hata hivyo, Ofisa Mkuu wa United Ed Woodward tayari ameshweka wazi kuwa hatataka kuchukua mchezaji kwa mkopo katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari. 
Woodward alibainisha mwezi uliopita kuwa tayari wana wachezaji waliowalenga kwa ajili ya usajili ujao wa majira ya kiangazi ila yoyote atakayeweza kupatikana Januari watafanya mipango ya kumchukua.

Beki kisiki Juma Nyosso hatimaye atua Mbeya City

http://1.bp.blogspot.com/-R068-dDaE2c/UIfJtqfAmqI/AAAAAAAAU8E/JxO1rjYx81c/s640/NYOSSO.JPG
Juma Nyosso enzi akiichezea Simba
HATIMAYE beki kisiki wa zamani wa Simba na Coastal Union, Juma Said Nyosso amejiunga na kikosi cha Mbeya City ya Mbeya kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza mara baada ya kuisaini mkataba huo kwenye ofisi za timu zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini Mbeya, Nyoso aliyewahi kucheza pia Ashanti United, alisema amekubali kujiunga na City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa imani kuwa utatosha kuushawishi uongozi wa timu kumpa mkataba mrefu zaidi mara baada ya huu wa sasa.
Kariobu nusu msimu beki huyo wa kati alikuwa hana timu yoyote anayoichezea tangu aachwe na Coastal mapema mzimu huu.
“City ni timu nzuri na imekuwa hivyo toka ilipoanzishwa miaka minne iliyopita, matokeo yaliyoo sasa ni sehemu ya soka ambayo timu yoyote inaweza kuyapata, nimekubari kujiunga na timu kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa sababu naamini uwezo wangu uwanjani utawashawishi viongozi kunipa mkataba mrefu zaidi pindi huu utakapo malizika na nina amini hili linawezekana kwa sababu nataka kukaa kwenye timu hii mpaka mpira wangu utakapoisha” alisema Nyosso
Akiendelea zaidi beki huyo aliyewahi pia kucheza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ alisema kuwa mafanikio iliyopata Mbeya City msimu uliopita yamekuwa sababu kubwa ya yeye kukubari kujiunga na City huku akiamini kuwa amekuja kuongeza nguvu kwenye timu bora ili kuhakikisha mafanikio ya msimu uliopita yanafanikiwa tena.
K wa upande wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe alimshukuru Nyosso kwa kukubari kujiunga na timu hii huku akiamini kuwa uzoefu alionao mchezaji huyo utasaidia kuimarisha safu ya ulinzi kwenye kikosi cha City.
“Tunamshukuru kukubari kujiunga nasi, imani yetu kubwa kwamba uzoefu alionao utasaidia kuimarisha safu yetu ya ulinzi, hasa ukizingatia matokeo tuliyopata katika michezo saba ya mwanzo wa Ligi hii” alisema Kimbe huku kauli yake hiyo ikiungwa mkono na Kocha Mkuu Juma Mwambusi.
Kwa sasa Nyosso tayari yuko na kikosi cha City kilichosafiri kwenda mjini Songea kwa ajiri ya michezo ya kirafiki.

Ronaldo afikisha mabao 200, sasa kinara wa hat trick La Liga

Cristiano Ronaldo celebrates his clinical hat-trick that sent records tumbling during a 3-0 victory at the Bernabeu
Ronaldo alishangilia moja ya mabao yake jana
Cristiano Ronaldo
Akiendelea kufunga
Cristiano Ronaldo
jamaa huyu balaa!
Real Madrid v Celta Vigo
Akishangilia na wenzake ushindi wa nyumbani Santiago Bernabeu
MWANASOKA Bora Duniani, Cristiano Ronaldo usiku wa jana alifikisha bao lake la 200 katika Ligi Kuu ya Hispania, baada ya kupiga 'hat trick' wakati Real Madrid ikiiangamiza 'Celta Vigo kwa mabao 3-0 katika mfululizo wa ligi hiyo.
Hat trick hiyo ni ya 23 kwa Mreno huyo na kumfanya kuwa mchezaji anayeongoza kwa hat trick nyingi katika La Liga kwa sasa, licha ya kukamata nafasi ya 9 ya wachezaji wenye magoli mengi katika ligi hiyo akiwa nyuma ya mabao 53 dhidi ya  'hasimu' wake, Lionel Messi mwenye mabao 253.
Mabao hayo yamemfanya mchezaji huyo kufikisha mabao 200 katika mechi 178 za La Liga kwa misimu wake wa sita nchini humo na pia ni bao la 23 katika mechi 13 za msimu huu, kiasi ambacho ukichukua mabao ya hasimu wake na ya mshambuliaji mwingine nyota wa Barecelona, Neymar hayafikii idadi hiyo ya mabao.

Ronaldo ambaye hakuwepo katika mechi ya Kombe la Mfalme wakati Real Ikishinda mabao 5-0 dhidi ya Cornellà, alianza kuandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 36.
Katika kipindi cha pili mkali huyo aliongeza tena mabao mawili katika dakika ya 65 na na 81 alipomaliza kazi nzuri ya Marcelo na kuifanya Real kuzidi kujichimbia kileleni na kuikimbia Atletico.
Ushindi huo umeifanya Real kufikisha pointi 36 wakati wapinzani wao ambao pia ndio mabingwa watetezi wakiwa na 32.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo jana Athletico Bilbao ililala nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Cordoba na leo kutakuiwa na michezo mingine kadhaa likiwamo pambano la Barcelona dhidi ya wapinzani wao wa Jimbo la Cataluna, Espaniola.
Wakali wa Hat Trick wa Muda wote La Liga Hawa Hapa:
23- CRISTIANO RONALDO 
22- Di Stéfano and Zarra 
20- Messi
19- Mundo 
16- César
13 Lángara