STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 22, 2014

Golden Bush ilivyopepetana na timu ya Wizara ya Afya leo Sinza

Golden Bush Veterani 'Wazee wa Dozi' wakijipanga kabla ya kuanza kwa 'game'
Jamani mnaonaje hawa jamaa tuwapige nane? Golden Bush Veterani
Timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakijifua kabla ya kuanza kwa mchezo
Tusipopasha vyema hawa jamaa wanaweza kututia aibu! Afya Fc wakipasha
Mwamuzi Othman Kazi akitetea na mchezaji wa Wizara ya Afya
Waambie wenzenu mjipange hawa jamaa wanapiga nyingi ooh! Refa Kazi akiagana na mchezaji wa Afya FC
 
Kipa wa Golden Bush, Machota akidaka mpiga ulioelekezwa langoni mwake na Afya FC
Hapa kazi tu, msitutanie nyie!
Said Kokoo akipitwa na mchezaji wa Afya Fc huku wachezaji wenzake wakitafakari namna ya kuupata mpira
Wisdom Ndhlovu wa Golden Bush akiuwahi mpira karibu na lango lake
Chupuchupu Golden Bush watunguliwe baada ya mpira wa kona kutoka nje
 

Said Kokoo (26) akitafuta mbinu za kumnyang'anya mpira Ally wa timu ya Wizara ya Afya
Beki wa pembeni wa Golden Bush, Majaliwa akimiliki mpira huku akinyemelewa na mchezaji wa Afya FC
Mimi ndiyo Majaliwa Mwaigaga bana!
Kama Ronaldo vile!
Wazir Mahadh (10) akionyesha vitu vyake

Shomari (9) wa Golden Bush aliyefunga bao pekee la mchezo baina yao na timu ya Wizara ya Afya akichuana kuwania mpira
Sijui nimtoke vipi? Mchezaji wa Afya Fc akitafakari mbele ya Majaliwa
Mchezaji wa Afya Fc Ally akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Golden Bush
 
 
Patashikla langoni mwa Golden Bush
Kipa Machota akionyesha ujuzi wake, huku akifuatwa na mchezaji wa Afya na Majaliwa (17) anayecheza wote timu ya Golden Bush akiwa tayari kutoa msaada
Bonge la 'Mido' Makocha Mayay wa Golden Bush akionyesha 'maujuzi' yake
 

Saidi Kokoo akimtoka mchezaji wa Afya Fc
Peke yetu jamani tutulie, Mandieta, Kokoo na Ticotico wa Golden Bush
Heka heka langoni mwa Golden Bush
Tupozeni makoo tukawafanyie wapinzani! Wachezaji wa Golden Bush wakiwa mapumziko
Dah! Hivi tulikuwa tunacheza na Simba, Yanga au Golden Bush Afya Fc wakiwa wamepumzika
Kocha wa timu ya Afya, Wille (kulia) akiongea na wachezaji wake wakati wa mapumziko
Jamani mbona mnawachelewesha? Kocha Madaraka Suleiman 'Mzee wa Kiminyio' (kushoto) akiongea na wachezaji wake wa Golden Bush huku Herry Morris naye akiwa pembeni ( aliyesimama jezi ya njano) 
 

Makocha Herry Morris na Madaraka Seleman wakitetea na wachezaji wao
Jamani hili jua la leo kama kiama! Marefa wa pambano hilo wakitetea wakati wa mapumziko.
Hekaheka langoni mwa timu ya Afya Fc
Salum Swedi 'Kussi' akionyesha makali yake
Oyaa jikaze mtoto wa kiume! Kipa wa Afya akiwa chini baada ya kuumia huku mwamuzi Othman Kazi akimjulia hali
Kazi imeisha! Othman Kazi akitoka uwanjani baada ya kumaliza pambano la Golden Bush Veterani dhidi ya timu ya Wizara ya Afya ambapo Golden walishinda bao 1-0.

Miaka mi3 Ajali ya Five Star, Hammer Q awakumbuka hivi!


IMG_6620 
JANA ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka mitatu tangu vifo vya wanamuziki wa 5 Star waliokufa kwenye ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha basi lao aina ya Coaster iliyokuwa na namba za usajili T 361 BGE  iliyokuwa imebeba wanamuziki wa bendi hiyo ya Taarabu ya 5 Star wakitokea Kyela-Mbeya kueleka jijini Dar.
hama q 
Ajali hiyo ilitokea March 21 2011 majira ya saa 2 usiku ndani ya hifadhi za wanyama za Mikumi mkoani Morogoro baada ya gari hilo kuligonga kwa nyuma roli aina ya Scania lililokuwa na namba za usajili T 848 APE ambalo lililikua linavuta tela lenye namba za usajili T 559 BDL liliokuwa na mzigo wa mbao.
Sasa ikiwa ni miaka 3 tangu vifo hivyo Msanii Hammer Q miongoni mwa abiria waliyokua na basi hilo kabla ya kushukia njiani mjini Iringa na kuokoka kifo, ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Facebook unaosomeka hivi:
Screenshot_2014-03-21-17-12-17

Chelsea, Arsenal vita tupu England

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEglhD34QM-L5Ccej6DoEdIFU8u3FTU6eFEmwnsnSt25d4p6q70Jgzb0yYlrPRNxeeL2eKkWbIqxJ26_nypsMyZovfE18TFVZq_63rt_liABV6FZuLm-lbVDOVYJUDEO8_ZRXvWFZHF8DxWV/s1600/Chelsea+vs+Arsenal+2013.jpg
PATASHIKA ya Ligi Kuu ya England inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo nane, huku macho na masikio ya mashibiki wa kandanda duniani kote wakifuatilia kwa karibu pambano la vinara wa ligi hiyo Chelsea itakayokuwa darajani kuikaribisha Arsenal.
Pambano hilo linavuta hisia za wengi kutokana na mchuano wao wa kuwania ubingwa msimu huu ambapo Arsenal wapo nafasi ya tatu ikizidiwa pointi nne na Chelsea na pia kuzidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na Liverpool wanashika nafasi ya pili japo wanalingana pointi 62 kila mmoja.
Timu hizo zinakutana huku kukiwa na rekodi za kusisimua baina yao na hasa kwa makocha wao Jose Mourinho wa Chelsea na Arsene Wenger wa Arsenal.
Katika mechi 10 zilizokupita kwa makocha hao kukutana Mourinho amemtambia Wenger ambaye pambano hilo la leo litakuwa ni la 1,000 kwake tangu aanze kuinoa timu hiyo ya London ya Kaskazini.
Chelsea haijapoteza michezo 75 kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Stanford Bridge,  ingawa itaikabili Arsena yenye rekodi nzuri ya kushinda mechi za ugenini ikiwakosa wachezaji wake wa Kibrazil, Willian na Ramires walionyesha kadi nyekundu katika mechi yao iliyopita dhidi ya Aston Villa waliolazwa bao 1-0.
Mechi nyingine za ligi hiyo ni kama ratiba inavyoonyesha hapo chini.
18:00 Cardiff V Liverpool
18:00 Everton V Swansea
18:00 Hull V West Brom
18:00 Man City V Fulham
18:00 Newcastle V Crystal Palace
18:00 Norwich V Sunderland
20:30 West Ham V Man United

Kesho Machi 23
16:30 Tottenham V Southampton
19:00 Aston Villa V Stoke

Simba waidindia TFF faini ya Sh Mil. 5

KLABU ya Simba imegoma kulipa faini ya sh.milioni 5 kwa shirikisho la soka, TFF, ikiwa ni adhabu kwa mashabiki wake kuvunjam iti katika mechi ambayo haikuwa ikicheza uwanjani.
Simba ilitozwa faini ya sh.milioni 5 baada ya TFF kujiridhisha kuwa wapenzi wa soka waliokaa upande wake kwenye Uwanja wa Taifa wakiwa na fulana nyekundu katika mechi ya kimataifa baina ya Yanga na Al Ahly ya Misri ni wapenzi wa timu hiyo.

Akizungumza jana jijini, Msemaji wa Simba Asha Muhaji alisema timu yake haitolipa adhabu hiyo kwa sababu TFF imeionea na ni kinyume na kanuni zake lenyewe.

Asha alisema kanuni za TFF zinasema "timu mwenyeji ndiyo inayopaswa kubeba dhamana endapo patatokea uharibifu wa mali uwanjani wakati wa mechi."
Alisema mwaka 2012, katika mechi ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika baina ya Simba na Kiyovu kwenye uwanja huo, mashabiki wa Yanga na wa Simba walifanya uharibifu lakini faini ilililipwa na wao pekee.

TFF iliitoza Yanga jumla ya sh. milioni 20 katika faini na fidia na Simba faini ya sh. milioni 5 katikati ya wiki kutokana na uharibifu wa viti uliofanyika katika pambano la kwanza la raundi ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwanzoni mwa mwezi.

Alipulizwa juu ya malalamiko hayo ya Simba jana, Msemaji wa TFF Boniface Wambura alisema timu hiyo haipswi kugomea adhabu hiyo kwa sababu imetolewa baada ya uchunguzi wa kina.

“Tumefanya uchunguzi na kugundua kuwa mashabiki wa Simba na Yanga walishiriki kufanya uharibifu na ndiyo maana tukaamua kuwapiga faini wote.

“Tumetumia ushahidi wa video na kuamua kutuoa adhabu kali kwa klabu ili kukomesha vitendo hivi katika mechi zijazo."

Nipashe

Golden Bush yaizima timu ya Wizara ya Afya

Kikosi cha Golden Bush Veterani kilichoanza pambano lao dhidi ya Afya FC
Kikosi cha timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kinachoijiandaa na mechi ya Mei Mosi na kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Golden Bush Veterani
Gaga (13) wa Golden Bush akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Afya FC
Sisi siyo wale mliokuwa mkiwapiga 8, sisi tupo fiti!
Mchezaji wa Afya FC akiambaa na mpira huku Onesmo Waziri 'Ticotico' akitafuta mbinu za klumnayng'anya mpira huo

Said Kokoo wa Golden Bush akimtoka mmoja wa wachezaji wa Afya FC huku mwamuzi Othman Kazi 'Collins' akishuhudia na kibendera chake
Mchezaji wa timu ya Wizara ya Afya akiambaa na mpira
MABINGWA wa soka la maveterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani 'Wazee Dozi' leo wameikwanyua kiduchu timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayojiandaa na michuano ya Mei Mosi, itakayofanyika mjini Morogoro kwa kuilaza bao 1-0.
Pambano hilo la kirafiki lililojaa burudani ya aina yake , lilipigwa majira ya asubuhi kwenye uwanja wa TP Afrika, Sinza na kushuhudiwa hadi wakati wa mapumziko timu hizo zikiwa hazijafunga baop lolote licha ya Golden Bush kushambulia kwa muda mrefu.
Kama washambuliaji wa Golden Bush waliokuwa wamejaza nyota wa zamani wa Simba na Yanga kama Abubakar Kombo, Salum Swedi 'Kussi', Thomas Mourice, Wazir Mahadh 'Manideta', Said Koko, Sadick Muhimbo na Wisdom Ndlovu wamekuwa makini wangeondoka na kapu la mabao kutokana na kosa kosa walizokuwa wakifanya langoni mwa Afya Fc.
Mabadiliko machache yaliyofanywa na timu zote mbili katika kipindi cha pili yalileta uhai na kuisaidia Golden Bush kupata bao lake la pekee lililofungwa kwenye dakika ya 77 na Shomari baada ya kutokea purukushani langoni nwa timu ya Afya walionyesha soka safi na kutulia.