KLABU ya Simba imegoma kulipa faini ya sh.milioni 5 kwa shirikisho la
soka, TFF, ikiwa ni adhabu kwa mashabiki wake kuvunjam iti katika mechi
ambayo haikuwa ikicheza uwanjani.
Simba ilitozwa faini ya sh.milioni 5 baada ya TFF kujiridhisha kuwa
wapenzi wa soka waliokaa upande wake kwenye Uwanja wa Taifa wakiwa na
fulana nyekundu katika mechi ya kimataifa baina ya Yanga na Al Ahly ya
Misri ni wapenzi wa timu hiyo.
Akizungumza jana jijini, Msemaji wa Simba Asha Muhaji alisema timu yake
haitolipa adhabu hiyo kwa sababu TFF imeionea na ni kinyume na kanuni
zake lenyewe.
Asha alisema kanuni za TFF zinasema "timu mwenyeji ndiyo inayopaswa
kubeba dhamana endapo patatokea uharibifu wa mali uwanjani wakati wa
mechi."
Alisema mwaka 2012, katika mechi ya Kombe la Shirikisho la klabu za
Afrika baina ya Simba na Kiyovu kwenye uwanja huo, mashabiki wa Yanga na
wa Simba walifanya uharibifu lakini faini ilililipwa na wao pekee.
TFF iliitoza Yanga jumla ya sh. milioni 20 katika faini na fidia na
Simba faini ya sh. milioni 5 katikati ya wiki kutokana na uharibifu wa
viti uliofanyika katika pambano la kwanza la raundi ya kwanza ya Ligi ya
Klabu Bingwa Afrika mwanzoni mwa mwezi.
Alipulizwa juu ya malalamiko hayo ya Simba jana, Msemaji wa TFF Boniface
Wambura alisema timu hiyo haipswi kugomea adhabu hiyo kwa sababu
imetolewa baada ya uchunguzi wa kina.
“Tumefanya uchunguzi na kugundua kuwa mashabiki wa Simba na Yanga
walishiriki kufanya uharibifu na ndiyo maana tukaamua kuwapiga faini
wote.
“Tumetumia ushahidi wa video na kuamua kutuoa adhabu kali kwa klabu ili kukomesha vitendo hivi katika mechi zijazo."
Nipashe
No comments:
Post a Comment