STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 22, 2014

Kivumbi cha Ligi Kuu kuendelea leo Yanga wapo Tabora

KIVUMBI cha Ligi Kuu kinatarajiwa kuendelea tena leo kwa mabingwa watetezi ambao bado hawajakaa sawa tangu watoke Misri, watakuwa ugenini kuvaana na Rhino Rangers.
Mechi hiyo ni kati ya mbili zinazochezwa leo ambapo nyingine ni ile itakayochezwa Chamazi kati ya wenyeji JKT Ruvu dhidi ya Mbeya City.
Yanga iliyong'olewa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penati na Al Ahly, imetoka sare mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Mtibwa Sugar na Azam na itahitaji ushindi leo ili kuifukuzia Azam kileleni.
Rhino wakijifua tayari kuwavaa Yanga leo
Katika mechi yao ya leo itakayopigwa uwanja wa Ali Hassani Mwinyi, viingilio vimepangwa kati ya Sh 5,000 kwa jukwaa Kuu na Sh 3,000 kwa mzunguko Kivumbi cha ligi hiyo inayoelekea ukingoni kwa sasa kitaendelea kesho kwa mechi nne ambapo Simba itacheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Vinara wa ligi hiyo Azam itaikarfibisha Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex na mechi hizo mbili zitaonyeshwa 'live' na kituo cha Azam TV.
Mechi nyingine za Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.


No comments:

Post a Comment