| Golden Bush Veterani 'Wazee wa Dozi' wakijipanga kabla ya kuanza kwa 'game' |
| Jamani mnaonaje hawa jamaa tuwapige nane? Golden Bush Veterani |
| Timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakijifua kabla ya kuanza kwa mchezo |
| Tusipopasha vyema hawa jamaa wanaweza kututia aibu! Afya Fc wakipasha |
| Mwamuzi Othman Kazi akitetea na mchezaji wa Wizara ya Afya |
| Waambie wenzenu mjipange hawa jamaa wanapiga nyingi ooh! Refa Kazi akiagana na mchezaji wa Afya FC |
| Kipa wa Golden Bush, Machota akidaka mpiga ulioelekezwa langoni mwake na Afya FC |
| Hapa kazi tu, msitutanie nyie! |
| Said Kokoo akipitwa na mchezaji wa Afya Fc huku wachezaji wenzake wakitafakari namna ya kuupata mpira |
| Wisdom Ndhlovu wa Golden Bush akiuwahi mpira karibu na lango lake |
| Chupuchupu Golden Bush watunguliwe baada ya mpira wa kona kutoka nje |
| Said Kokoo (26) akitafuta mbinu za kumnyang'anya mpira Ally wa timu ya Wizara ya Afya |
| Beki wa pembeni wa Golden Bush, Majaliwa akimiliki mpira huku akinyemelewa na mchezaji wa Afya FC |
| Mimi ndiyo Majaliwa Mwaigaga bana! |
| Kama Ronaldo vile! |
| Wazir Mahadh (10) akionyesha vitu vyake |
| Shomari (9) wa Golden Bush aliyefunga bao pekee la mchezo baina yao na timu ya Wizara ya Afya akichuana kuwania mpira |
| Sijui nimtoke vipi? Mchezaji wa Afya Fc akitafakari mbele ya Majaliwa |
| Mchezaji wa Afya Fc Ally akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Golden Bush |
| Patashikla langoni mwa Golden Bush |
| Kipa Machota akionyesha ujuzi wake, huku akifuatwa na mchezaji wa Afya na Majaliwa (17) anayecheza wote timu ya Golden Bush akiwa tayari kutoa msaada |
| Bonge la 'Mido' Makocha Mayay wa Golden Bush akionyesha 'maujuzi' yake |
| Saidi Kokoo akimtoka mchezaji wa Afya Fc |
| Peke yetu jamani tutulie, Mandieta, Kokoo na Ticotico wa Golden Bush |
| Heka heka langoni mwa Golden Bush |
| Tupozeni makoo tukawafanyie wapinzani! Wachezaji wa Golden Bush wakiwa mapumziko |
| Dah! Hivi tulikuwa tunacheza na Simba, Yanga au Golden Bush Afya Fc wakiwa wamepumzika |
| Kocha wa timu ya Afya, Wille (kulia) akiongea na wachezaji wake wakati wa mapumziko |
| Jamani mbona mnawachelewesha? Kocha Madaraka Suleiman 'Mzee wa Kiminyio' (kushoto) akiongea na wachezaji wake wa Golden Bush huku Herry Morris naye akiwa pembeni ( aliyesimama jezi ya njano) |
| Makocha Herry Morris na Madaraka Seleman wakitetea na wachezaji wao |
| Jamani hili jua la leo kama kiama! Marefa wa pambano hilo wakitetea wakati wa mapumziko. |
| Hekaheka langoni mwa timu ya Afya Fc |
| Salum Swedi 'Kussi' akionyesha makali yake |
| Oyaa jikaze mtoto wa kiume! Kipa wa Afya akiwa chini baada ya kuumia huku mwamuzi Othman Kazi akimjulia hali |
| Kazi imeisha! Othman Kazi akitoka uwanjani baada ya kumaliza pambano la Golden Bush Veterani dhidi ya timu ya Wizara ya Afya ambapo Golden walishinda bao 1-0. |
No comments:
Post a Comment