STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 22, 2014

Golden Bush yaizima timu ya Wizara ya Afya

Kikosi cha Golden Bush Veterani kilichoanza pambano lao dhidi ya Afya FC
Kikosi cha timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kinachoijiandaa na mechi ya Mei Mosi na kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Golden Bush Veterani
Gaga (13) wa Golden Bush akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Afya FC
Sisi siyo wale mliokuwa mkiwapiga 8, sisi tupo fiti!
Mchezaji wa Afya FC akiambaa na mpira huku Onesmo Waziri 'Ticotico' akitafuta mbinu za klumnayng'anya mpira huo

Said Kokoo wa Golden Bush akimtoka mmoja wa wachezaji wa Afya FC huku mwamuzi Othman Kazi 'Collins' akishuhudia na kibendera chake
Mchezaji wa timu ya Wizara ya Afya akiambaa na mpira
MABINGWA wa soka la maveterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani 'Wazee Dozi' leo wameikwanyua kiduchu timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayojiandaa na michuano ya Mei Mosi, itakayofanyika mjini Morogoro kwa kuilaza bao 1-0.
Pambano hilo la kirafiki lililojaa burudani ya aina yake , lilipigwa majira ya asubuhi kwenye uwanja wa TP Afrika, Sinza na kushuhudiwa hadi wakati wa mapumziko timu hizo zikiwa hazijafunga baop lolote licha ya Golden Bush kushambulia kwa muda mrefu.
Kama washambuliaji wa Golden Bush waliokuwa wamejaza nyota wa zamani wa Simba na Yanga kama Abubakar Kombo, Salum Swedi 'Kussi', Thomas Mourice, Wazir Mahadh 'Manideta', Said Koko, Sadick Muhimbo na Wisdom Ndlovu wamekuwa makini wangeondoka na kapu la mabao kutokana na kosa kosa walizokuwa wakifanya langoni mwa Afya Fc.
Mabadiliko machache yaliyofanywa na timu zote mbili katika kipindi cha pili yalileta uhai na kuisaidia Golden Bush kupata bao lake la pekee lililofungwa kwenye dakika ya 77 na Shomari baada ya kutokea purukushani langoni nwa timu ya Afya walionyesha soka safi na kutulia.

No comments:

Post a Comment