STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 22, 2015

Nafasi nyingine kwa Manchester Utd EPL


http://strettynews.com/wp-content/uploads/2015/02/UnitedvPreston.jpg
Mashetani Wekundu ambao wamekuja kivingine msimu huu
Chelsea
Watetezi Chelsea wanaopepesuka
KIVUMBI cha Ligi Kuu England kinaendelea leo kwa michezo kadhaa, lakini mapema saa 8;30 mchana Mashetani Wekundu watakuwa wakisaka nafasi ya kurejea kileleni japo kwa sasa kadhaa wakati watakapovaana na vibonde Newcastle United kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Manchester United yenye pointi sita inaweza kuiengua Man City ambayo yenye itacheza kesho dhidi ya Everton kwa kufikisha pointi 9 kama itashinda huku ikiombea Leicester City ipoteze mchezo wake wa leo dhidi ya Tottenham Hotspur.
Ratiba kamili ya ligi hiyo kwa leo, kesho Jumapili na Jumatatu ambapo Arsenal itakuwa na kibarua kigumu cha kuibakaribisha Liverpool ipo hapo chini jionee mwenyewe;
Leo Jumamosi:
Manchester United     11 : 45    Newcastle United        
Crystal Palace     14 : 00    Aston Villa        
West Ham United     14 : 00    AFC Bournemouth        
Norwich City     14 : 00    Stoke City        
Sunderland     14 : 00    Swansea City        
Leicester City     14 : 00    Tottenham Hotspur        
Kesho Jumapili
West Bromwich Albion 12 : 30    Chelsea        
Everton     15 : 00    Manchester City        
Watford     15 : 00    Southampton        
Jumatatu
Arsenal     19 : 00    Liverpool

PATACHIMBIKA TAIFA, YANGA v AZAM NI SHEEDA!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpjkGwXmOK250PzIJkj4gA7pkZ1mMpkKFXP2MG3mX3y_l3IHb7aHldzJdHcS2u-VTXyZldrrwgZtbd-yV0ndewKQDYjerOJ3aSNEVPxtJHCgeoHY8UgogGyJ-jYXVUU7COyj83XDERC6g/s1600/IMG_8065.JPG
Azam FC
Yanga
MABINGWA wa soka wa Tanzania, Yanga pamoja na Mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam jioni ya leo wanatarajia kuonyeshana undava wakati zitakapokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani.
Mchezo huo maalum kwa ajili ya kuzindua msimu mpya wa Ligi kuu ya Tanzania Bara utapigwa dimba la Taifa, huku timu zote zikitarajiwa kuwakosa baadhi ya nyota wake kutokana na matatizo mbalimbali.
Yanga ambao imeonyesha kuupania mchezo huo hasa baada ya kutolewa nishai na Azma kwenye robo fainali ya Kombe la Kagame, huenda isiwe na Amissi Tambwe aliyekuwa akisumbuliwa na Malaria, japo Donald Ngoma anaweza kucheza akitoka kuuguza maumivu ya nyonga.
Azam wenyewe wanaosaka ushindi wa kwanza wa mchezo huo wa Ngao ya Hisani na pia kujaribu kufuta uteja kwa wapinzani kila wakikitana kwenye pambano hilo inaweza kumkosa Kipre Tchetche.
Hata hivyo vikosi vyote chini ya makocha wao, Stewart Hall kwa Azam na Hans van Pluijm wa Yanga wamenukuliwa wakitamba kuwa leo itakuwa kazi tu, na kuzipa matumiani timu yao kushinda.
"Yanga ni wazuri na ni timu kubwa na unapocheza nao ni kama ina wachezaji 12 kutokana na mashabiki wanaoiunga mkono, lakini tupo tayari na vijana wanagu wana ari ya kushinda," alisema.
Pluijm alisema kuwa ameandaa vijana wake kwa ajili ya kazi moja ya kushinda Taifa, hasa baaada ya kuridhishwa na mabadiliko aliyoyaona kwa safu yake ya mbele wakiwa jijini Mbeya kwenye kambi.
Bila ya shaka mashabiki wa soka watapata uhondo katika mchezo huo utakaochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya baada ya refa wa awali, Israel Nkongo kupatwa na dharura ya kuugua na kuenguliwa.
Rekodi Azam Ngao ya Hisani:
2012: Simba 3-2 Azam
2013 Azam 0-1 Yanga
2014: Yanga 3-0 Azam
2015: Azam v Yanga???