STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 7, 2016

Yanga 2 Mtibwa 1, Henry Joseph alimwa red card

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/01/Yanga-vs-Mtibwa-znz-3.jpg
Mtibwa iliyolala kwa Yanga usiku huu
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/01/Yanga-vs-Mtibwa-znz-2.jpg
Yanga iliyomaliza kazi Amaan dhidi ya Mtibwa Sugar
PAMBANO la Yanga na Mtibwa limeisha kwa matokeo ya 2-1, Yanga ikiibuka kidedea dhidi ya Wakata Miwa.
Yanga iliandika bao la pili na la ushindi lililofungwa na mtokea benchi Malimi Busungu aliyemalizia kazi nzuri ya Simon Msuva aliyepiga krosi murua iliyomkuta Busungu pekee yake na kupiga kichwa kilichompita kipa Said Mohammed.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 82 na kuifanya Yanga kuongoza kundi B ikiwa na pointi 7 na Mtibwa kumaliza ya pili na pointi 4 na sasa wanasubiri kujua wanacheza na timu zipi kutoka kundi A ambapo Simba na JKU wataumana usiku wa kesho na mapema jioni, URA ya Uganda itakwaruzana na Jamhuri-Pemba.
Simba ndio inaoongoza kundi hilo kwa sasa ikiwa na pointi 4 ikifuatiwa na JKU kisha URA zote zikiwa na pointi 3 kila mmoja isipokuwa kutofautiana mabao ya kufungwa na kufunga, huku Jamhuri ikiburuza mkia ikiwa na pointi moja iliyotokana na sare dhidi ya Simba.

Bado matokeo ni 1-1

YANGA na Mtibwa zinaendelea kupambana kwenye Uwanja wa Amaan, matokeo yakiwa ni yale yale ya 1-1, huku kila timu ikifanya mabadiliko ya wachezaji katika kuongeza nguvu. Ikiwa ni dakika ya 75 sasa.

Bocco, Mao waomba radhi Azam kuchemsha Mapinduzi Cup


http://cecafafootball.org/wp-content/uploads/2014/03/john-bocco.jpg
John Bocco
Kikosi cha Azam kilichotolewa Mapinduzi Cup jioni ya leo visiwani Zanzibar

NAHODHA wa Azam, John Bocco 'Adebayor' amewaomba radhi mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kwa matokeo mabaya ambayo timu hiyo imeyapata kwa siku za karibuni.
Kupitia akauti yake ya Facebook, Bocco amekiri Azam imekuwa kimeo kwa siku za karibuni na kukiri kwamba watajirejkebisha na kubwa ni kuwamba radhi wote waliokwazwa na matokeo ya timu yao ambayo jioni ya leo iling;olewa rasmi kwenye michunoa ya Kombe la Mapinduzi kwa kucharazwa mabao 2-1 na Mafunzo ya Zanzibar.
Ujumbe wa Bocco ndio huu, usome mwenyewe;
"Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki wote wa Azam Fc kwa performance mbaya tulioonyesha kwenye mashindano ya Mapinduzi na mechi mbili za Ligi kabla ya kuja huku, matokeo ni sehemu ya mchezo inakubalika, lakin kitu kinacho angaliwa ni unapataje matokeo yawe mazuri au mabaya, tumepata matokeo mabaya kutoka kwenye performance mbaya zaidi kuwahi kuiona katika timu yetu tangu nilipoanza kucheza hadi sasa hivi, hivo tunawaomba radhi mashabiki wetu wote na kuwaaidi tutajituma na kupigania club yetu kwa moyo wetu wote."

Kadhalika naye Himid Mao aliomba radhi kama ujumbe wake unavyosomeka;
Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki wote wa Azam Fc kwa performance mbaya tulioonyesha kwenye mashindano ya Mapinduzi na mechi mbili za Ligi kabla ya kuja huku, matokeo ni sehemu ya mchezo inakubalika, lakin kitu kinacho angaliwa ni unapataje matokeo yawe mazuri au mabaya, tumepata matokeo mabaya kutoka kwenye performance mbaya zaidi kuwahi kuiona katika timu yetu tangu nilipoanza kucheza hadi sasa hivi, nasikia aibu sana tena zaidi ya sana sina njia ya kuelezea ni kiasi gani najiskia vibaya na aibu naa mini na wachezaji wenzangu wanajiskia vibaya kama nnavyo jiskia mimi.....
I will work as harder as i can to make things better for me & my team
Samahani kwa mara nyingine tena,
Usiku Mwema

Kipidi cha pili Yanga v Mtibwa kimeanza

Kipindi cha kimeshaanza na timu zote zimeanza kwa kasi kusaka bao la pili. Pambano ni gumu  kwa timu zote, kila moja ikishambulia lango la mwenzake, lakini milango bado haijafunguka tena.


Nyota yaanza kumuwakia Samatta mapema...!

Mbwana Samatta (kushoto) alipokuwa akifanya majaribio CSKA Moscow
MANENO ya Wahenga huwa hayapotei. Wanasema dalili njema uanza asubuhi. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameanza kuwakiwa taa ya kijani katika tuzo za Afrika baada ya kutajwa miongoni mwa nyota wa kikosi cha wachezaji 11 Bora wa Caf 2015.
Samatta yupo Nigeria muda huu kwa ajili ya tuzo za Wachezaji Bora wa Afrika 2015 Glo Africa Awards 2015 zinazofanyika katika mji wa Abuja ametajwa kwenye kikosi hicho akiwa na wakali wengine wa dunia akiwa Mfungaji kinara wa mabao wa Bundesliga, Pierre-Emerick Aubameyang.
Wengine waliopo kwenye kikosi hicho ni kipa Robert Kidiaba, Serge Aurier, Aymen Abdennour, Mohammed Meftah, Andre Ayew, Yaya Toure, Sadio Mane, Yacine Brahimi, Aubameyang na Baghdad Bounedjah.
Huenda kwa mara ya kwanza Tanzania tukaandika historia kwa mwanasoka huyo kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Ni Mapumziko matokeo ni bao 1-1

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/01/Kichuya.png
Muuaji wa Mtiobwa, Shiza Kichuya
Mfungaji wa Yanga, Issofou Boubacar 'Diego'
YANGA na Azam zinaenda mapumziko matokeo yakiwa bao 1-1. Wachezaji wanaenda kupewa mawaidha toka kwa makocha wao, kabla ya kurudi uwanjani kwa ngwe ya pili

Yanga, Mtibwa ngoma nzito Amaan

Mtibwa
Yanga
PAMBANO la timu za Mtibwa Sugar na Yanga bado ngoma nzito kwani mpaka sasa dakika chache kabla ya mapumziko, matokeo ni sare ya 1-1.
Mtibwa walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 10 kupitia kwa chipukizi, Shiza Kichuya akimalizia pasi na Vincent Barnabas kabla ya Yanga kuchomboa dakika ya 41 kwa mkwaju wa kiufundi uliofungwa na Issofou Boubacar baada ya Donald Ngoma kuchezewa vibaya na kuwa faulo ambapo Mniger huyo alimtungua kipa Said Mohammed 'Nduda'.
Kabla ya mabao hayo timu zote zilipoteza nafasi nyingi za wazi, huku Yanga ikionekana kuzinduka baada ya kutunguliwa kwa kipa wao Deogratius Munishi 'Dida' ambaye katika mechi sita za nyuma alikuwa hajaruhusu bao kabla ya Azam 'kumtengua udhu' katika sare ya 1-1.

AZAM HADI AIBU, YATUPWA MAPINDUZI CUP

*YANGA, MTIBWA HAOO NUSU FAINALI

AZAM aibu tupu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mabingwa hao wa Kombe la Kagame  kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 2-1 na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa mwisho wa kundi B.
Kipigo hicho kilichopatikana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar imeifanya Azam kumaliza ikishika mkia wa kundi hilo na kuziacha Yanga na Mtibwa zitakazocheza usiku wa leo zikitinga nusu fainali kilaini na kusubiri tu kujua ipi itakuwa ya kwanza na nyingine ya pili.
Mafunzo ambayo haikupewa nafasi yoyote kwenye michuano hiyio na hasa kundi hilo la kifo, imeshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu, ingawa nayo imeaga michuano hiyo ya mwaka 2016.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 21 kabla ya Mafunzo kurejesha bao hilo dakika ya 35 Rashid Abdallah na kufanya hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini hakukuwa na jipya mpaka kwenye dakika ya majeruhi wakati mpira wa faulo wa Sadick Rajabu ulipotinga wavuni ukimuacha kipa mkongwe, Ivo Mapunda akiwa hana la kufanya langoni mwake.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Azam kwa msimu huu, kwani ilikuwa haijafungwa katika mechi zake 13 za Ligi Kuu Bara na hata kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi kwani ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa na Yanga.
Msimamo
Kundi A
                 P  W  D L  F A Pts
Simba        2   1  1  0 3 2  4
JKU            2   1  0  1 4 3  3
URA           2   1  0  1 3 2  3
Jamhuri      2   0  1  1 2 5  1

Kundi B
                 P  W  D L F A Pts
Yanga        2   1  1  0 4  1  4
Mtibwa       2   1  1  0 2  1  4
Mafunzo     3   1  0  2 2  5  3
Azam         3   0  2  1  3 4  2

Wafungaji:
2-Donald Ngoma (Yanga)
   Awadh Juma (Simba)
   Villa Oromuchan (URA)
   Mohammed Abdallah (JKU)
    Kipre Tchetche (Azam)
1-Paul Nonga (Yanga)
  Hussein Javu (Mtibwa)
  John Bocco (Azam)
  Oscar Aggaba (URA)
  Emmanuel Martin (JKU)
  Said Bahanuzi (Mtibwa)
  Vincent Bossou (Yanga)
  Mwalimu Khalfan (Jamhuri)
  Ammy Bangaseka (Jamhuri)
  Nassor Juma             (JKU)
  Ibrahim Ajib             (Simba)
  Rashid   Abdallah (Mafunzo)
  Sadick Rajabu     (Mafunzo)

UTAMU WA LIGI DARAJA LA KWANZA UMEKAA HIVI!

Benchi la Ufundi la Africans Lyon

Wachezaji wa Akiba wa Ashanti Utd
LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) inatarajiwa kuingia kwenye ngwe nyingine wikiendi hii kwa mkichezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti nchini.
Timu za Ruvu Shooting, Oljoro JKT na Ashanti United zimeonyesha dhamira ya kurejea tena Ligi Kuu
kutokana na kuongoza kwenye makundi yao.
MICHARAZO inakuletea ratiba ya mechi zilizosalia za ligi hiyo ambayo inashirikisha jumla ya 24 zinazowania nafasi tatu za kupanda kwa ajili ya Ligi Kuu msimu wa 2016-2017. Sambamba na hilo pia unaweza kuchungulia msimamo wake kujua ligi hiyo muelekeo wake ukoje kwa timu shiriki, ingawa ndio kwanza imeanza ngwe ya duru la pili wiki mbili zilizopita.

Kundi A:
African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam),

Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma),

Polisi Dar es Salaam na Polisi Dodoma.

Kundi B:
Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC (Iringa),

Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting (Pwani).

Kundi C:
Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC

(Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).

Msimamo Kundi A
                                   P W  D  L   F   A  Pts
Ashanti Utd                  9  5  3  1   13  5  18
Kiluvya Rangers            9  4  4  1   9   4  16
Africans Lyon                9  4  2  2   10 6  14 
Friends Rangers            9  2  5  1   9   4  14
KMC FC                        9  3  3  3   6   7  12
Polisi Dar                      9  2  5  2   5   6  11
CDA                             9   2  2  5   7  12  8
Polisi Dom                     9  1  0  8  4   18  3

Msimamo Kundi B
                                    P  W  D  L   F  A  Pts
Ruvu Shooting              9   7   1  1   21 5  22
Njombe Mji                   9   5   1  3   10 8  16
Kurugenzi                     9   4   2  3   10 9  14
JKT Mlale                      9   3   4  2   10 7   13
Polisi Moro                    9   3   2  4   8  11  11
Lipuli Fc                        9   2   4  3   6  11 10
Kimondo                       9   3   1  5   5  12 10
Burkina Faso                 9   0   3  6   6  13  3

Msimamo Kundi C
                              P W  D  L  F   A  Pts
Oljoro JKT               9   5   3  1  9   7   18
Polisi Tabora            9   5   2  2  12  4  17
Geita Gold               9   4   4  1  13  6  16
Mbao FC                  9   3   3  3  11  15  12
Panone                   9   3   2   4  10 8  11
Rhino Rangers         9   1   6   2  4  7   9
Polisi Mara               9   1   5   3  6  9   8
JKT Kanembwa        9  0  3   6   4 13   3

Ratiba
Jan 9, 2016
Panone FC     v     JKT Kanembwa    
Polisi Mara     v     JKT Oljoro    
Rhino Rangers     v     Geita Gold FC    
Mbao FC       v     Polisi Tabora    
Mji Mkuu     v     Ashanti United    
Kiluvya United     v     Polisi Dar    
African Lyon     v     Friends Rangers    
Kiluvya United     v     Polisi Dar    
Polisi Morogoro     v     Lipuli FC                      
JKT Mlale     v     Kimondo FC    
Kurugenzi FC     v     Ruvu Shooting    
Njombe Mji     v     Burkinafaso FC    

Jan 16, 2016
Polisi Dodoma     v     KMC FC                      
Mji Mkuu     v     African Lyon    
Polisi Dar     v     Ashanti United    
KMC FC                       v     Kiluvya United    
Polisi Dodoma     v     Friends Rangers    
Njombe Mji     v     Kimondo FC    
Lipuli FC                       v     Kurugenzi FC    
JKT Mlale     v     Polisi Morogoro    
Rhino Rangers     v     JKT Kanembwa    
Mbao FC                       v     JKT Oljoro    
Panone FC     v     Geita Gold FC    
Polisi Mara     v     Polisi Tabora    

Jan 17, 2016
Ruvu Shooting     v     Burkina Faso

Jan 30, 2016
Polisi Morogoro     v     Kimondo FC    
Kurugenzi FC     v     Burkinafaso FC    
Lipuli FC        v     Ruvu Shooting    
Panone FC     v     Mbao FC      
Polisi Mara     v     Rhino Rangers    
Polisi Tabora     v     Geita Gold FC    

Feb 5, 2016
Polisi Dar     v     Mji Mkuu    
Ashanti United     v     Polisi Dodoma    

Feb 6, 2016
Kiluvya United     v     Polisi Dodoma    
Friends Rangers     v     Mji Mkuu    
Polisi Morogoro     v     Kurugenzi FC    
Kimondo FC     v     Burkinafaso FC    
Ruvu Shooting     v     Njombe Mji    
Lipuli FC                       v     JKT Mlale    
JKT Kanembwa     v     Mbao FC                      
Geita Gold FC     v     Polisi Mara    
JKT Oljoro     v     Rhino Rangers    
Polisi Tabora     v     Panone FC    

Feb 7, 2016
African Lyon     v     Kiluvya United    
KMC FC                       v     Friends Rangers    
Friends Rangers     v     Mji Mkuu    

Feb 13, 2016
Mji Mkuu     v     Ashanti United
Kiluvya United     v     Polisi Dar    
African Lyon     v     Friends Rangers    
Polisi Dodoma     v     KMC FC                      
Polisi Morogoro     v     Lipuli FC                      
JKT Mlale     v     Kimondo FC    
Kurugenzi FC     v     Ruvu Shooting    
Njombe Mji     v     Burkinafaso FC    
Panone FC     v     JKT Kanembwa    
Polisi Mara     v     JKT Oljoro    
Rhino Rangers     v     Geita Gold FC    
Mbao FC           v     Polisi Tabora    

Feb 20, 2016
Mji Mkuu     v     African Lyon
Polisi Dar     v     Ashanti United
KMC FC                      v     Kiluvya United
Polisi Dodoma     v     Friends Rangers
Njombe Mji     v     Kimondo FC    
Lipuli FC        v     Kurugenzi FC    
JKT Mlale     v     Polisi Morogoro    
Rhino Rangers     v     JKT Kanembwa    
Mbao FC      v     JKT Oljoro    
Panone FC     v     Geita Gold FC    
Polisi Mara     v     Polisi Tabora    

Feb 21, 2016
Ruvu Shooting     v     Burkina Faso FC

Feb 27, 2016
Polisi Dodoma     v     African Lyon
Kiluvya United     v     Mji Mkuu
Friends Rangers     v     Ashanti United
Polisi Dar     v     KMC FC       
Polisi Morogoro     v     Kimondo FC    
Kurugenzi FC     v     Burkinafaso FC    
JKT Mlale     v     Njombe Mji    
Lipuli FC       v     Ruvu Shooting    
Panone FC     v     Mbao FC     
Polisi Mara     v     Rhino Rangers    
Polisi Tabora     v     Geita Gold FC    
JKT Oljoro     v     JKT Kanembwa    

Mar 5,2016
African Lyon     v     Polisi Dar
Ashanti United     v     KMC FC   
Polisi Morogoro     v     Njombe Mji
Kurugenzi FC     v     JKT Mlale    
Burkinafaso FC     v     Lipuli FC      
Kimondo FC     v     Ruvu Shooting    
Rhino Rangers     v     Mbao FC     
Polisi Mara     v     Panone FC    
Geita Gold FC     v     JKT Oljoro    
JKT Kanembwa     v     Polisi Tabora    

Mar 12, 2016
Polisi Dar     v     Polisi Dodoma    
Mji Mkuu     v     KMC FC                      
African Lyon     v     Ashanti United    
Friends Rangers     v     Kiluvya United    
Mbao FC      v     Polisi Mara    
Polisi Tabora     v     JKT Oljoro    
JKT Kanembwa     v     Geita Gold FC    
Rhino Rangers     v     Panone FC    

Mar 13, 2016
Kimondo FC     v     Kurugenzi FC    
Njombe Mji     v     Lipuli FC      
Ruvu Shooting     v     Polisi Morogoro    
Burkinafaso FC     v     JKT Mlale    

Liverpool kuingia sokoni kusaka vifaa vipya

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/styles/story_large/public/thumbnails/image/2015/10/31/14/CSpmUSYVAAAD4IX.jpg
Jurgen Klopp
HANA Ujanja. Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiri atalazimika kuingia sokoni ili kusajili wachezaji wapya kutokanana matatizo ya majeruhi kuzidi kuiandamana timu yake iliyopita ushindi juzi wa mkondo wa kwanza wa Nusu fainali ya michuano ya Kombe la Ligi (Capital One).
Liverpool iliikwanyua Stoke City kwa bao 1-0, huku nyota wake Philippe Coutinho na Dijan Lovren wakitolewa nje kutokana na majeraha ya msuli ya paja na Kolo Toure naye alimaliza mchezo huo akionekana kuwa na tatizo kama hilo.
Mara kadhaa Klopp amekuwa akidai kuwa hatanunua mchezaji mpya katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo. Lakini kutokana na majeruhi kuzidi kuongezeka, kocha huyo amefichua kuwa, anadhani anaweza kulazimika kuongeza nguvu katika kikosi chake.
Kuumia kwa Toure na Lovren kunaifanya Liverpool kukosa beki wa kati aliye fiti kwani Martin Skrtel na Mamadou Sakho nao pia ni majeruhi

Rafa Benitez hana kinyogo na Real Madrid

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01682/SNF0108A---_1682580a.jpg
Kocha Rafa Benitez
LICHA ya kumtimua kazi, Meneja wa zamani wa Real Madrid, Rafael Benitez ametoa ya moyoni kwa kuishukuru klabu hiyo kwa kumpa nafasi na kumtakia kila la kheri mrithi wake Zinedine Zidane. 
Benitez alitimuliwa Jumatatu  ikiwa ni miezi sba tu tangu alipokabidhiwa timu hiyo na nafasi yake kuchukua nguli wa klabu hiyo Zidane ambaye alikuwa akikinoa kikosi B cha Castilla. 
Kuanza kampeni za msimu huu kwa kusuasua kikiwemo na kipigo cha mabao 4-0 kutoka mahasimu wao Barcelona kulichangia kwa kiasi kikubwa kutimuliwa kwa Benitez, huku mgomo baridi katika vyumba vya kubadilishia nguo nao ukitajwa kuchangia pia. 
Lakini katika taarifa yake aliyotoa katika matandao wake, Benitez amewahakikishia kuwa hana kinyongo chochote kufuatia kutimuliwa kwake.  
Kocha huyo amesema imekuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi ya kuinoa klabu hiyo hivyo anawashukuru viongozi, wafanyakazi, wachezaji na mashabiki kwa kumuunga kwao mkono katika kipindi chote alichokuwepo Santiago Bernabeu.
Chini ya Benitez, Real Madrid ilishindwa kupata ushindi katika mechi nane, saba zikiwa za La Liga na moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sare ya 2-2 dhidi ya Valencia ilikuwa tiketi yake ya kutimuliwa klabuni hapo.

Tanzania yapanda nafasi 6 Fifa, Uganda noma!

Wachezaji wa Taifa Stars katika moja ya mechi zao za kimataifa
TANZANIA imepanda kwa nafasi sita kwenye msimamo wa Orodha ya Viwango vya Soka vya Dunia, ikishika nafasi ya 126 kutoka ile ya 132 iliyoshikilia Desemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa orodha mpya iliyotolewa leo Alhamisi, Uganda imeweka rekodi ya kushika nafasi ya 62 ikiwa nafasi ya juu zaidi kuwahi kushikwa na taifa hilo la Afrika Mashariki ikipanda nafasi moja juu. Desemba ilikuwa nafasi ya 63, huku Rwanda, Kenya, Burundi na Ethiopia zikiifuata nchi hiyo katika orodha hiyo kwa nchi za ukanda huo wa Afrika Mashariki.
Ivory Coast, Algeria zimeendelea kukomaa kwenye nafasi zao mbili za juu sawa na ilivyo kwa Ghana na Cape Verde kwa upande wa Afrika zikishika nafasi ya 19, 28, 33 na 39 duniani, huku Ubelgiji anapotaka kwenda kucheza soka la kulipwa nyota wa Afrika na Tanzania, Mbwana Samatta ikiendelea kuongoza orodha hiyo ya ubora dunia wakifuatiwa na Argentina, Hispania na Ujerumani katika nafasi nne Bora.

Top 10 ya Dunia:

1. Ubelgiji
2. Argentina
3 Hispania
4. Ujerumani
5. Chile
6. Brazili
7.Ureno
8. Colombia
9.England
10. Austria

Top 10 ya Afrika:

1. Ivory Coast
2. Algeria
3. Ghana
4. Cape Verde
5. Tunisia
6. Senegal
7. Congo
8. Guinea
9. Cameroon
10. Misri

Top 10 ya Cecafa:

1. Uganda
2. Rwanda
3. Kenya
4. Burundi
5. Ethiopia
6. Tanzania
7. Sudan
8. Sudan Kusini
9. Djibout
10. Eritrea